TLP: Tunampongeza Rais Samia kwa kuondoa VRF ya 6% kwenye HESLB pamoja na mkopo wa bilioni 106 kwa wanafunzi elfu 10 walionyimwa

Mtoto wa Samia

JF-Expert Member
May 27, 2020
325
250
Ndugu Wananchi wenzetu,

Mpaka Rais Samia anaingia madarakani zaidi ya watoto wa masikini elfu 10 hawakupewa mikopo,

Leo tayari ameongeza Tshs 106BL sawa na 23% yaani kutoka Tshs 464BL FY2020/21 hadi 570BL FY2021/22

Kwa Sasa,kila mtoto wa masikini aliyefaulu kwenda chuo kikuu kupatiwa mkopo bila kujali historia ya alikosomea shule za chini,

Lakini pia amefuta kabisa ile 6% ya ada ya thamani ya mkopo ( Value Retention Fee-VRF ) kwenye mikopo hiyo na Sasa wanufaika watakatwa 9% ( single digits) FY2021/22 kutoka 15% ya FY2020/21.

Take home za watu hawa zimepaa kwa 6% ,hongereni Sana Mhe Rais.

TLP ni akina nani hata tusione haya na kupongeza na hii ndio maana ya Siasa safi.

Mama chapa kazi tupo na wewe.

TLP Tanzania kwanza,

" Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni mama deserves better Wazalendo wote tumtie moyo, mpaka mwaka 2030 tutashuhudia maajabu, Tuombe uzima Tu"
 

eddy

JF-Expert Member
Dec 26, 2007
14,084
2,000
Tunaondoa tozo kwa watu wenye vipato vya uhakika tena walisoma kwa fedha za kununulia vifaa vya kujifungulia waja wazito, halafu munaweka tozo kwa watu wanao tumiwa nauli na yakutolea
 

CM 1774858

JF-Expert Member
May 29, 2021
1,599
2,000
Rais Samia ni mpango halisi wa Mungu,Mungu wetu hakawii wala hawai ni huyuhuyu tumepewa tumlinde,
 

CM 1774858

JF-Expert Member
May 29, 2021
1,599
2,000
Rais Samia ni mpango halisi wa Mungu,Mungu wetu hakawii wala hawai ni huyuhuyu tumepewa tumlinde,
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom