TLP: Tunampongeza Rais Samia kwa kuondoa VRF ya 6% kwenye HESLB pamoja na mkopo wa bilioni 106 kwa wanafunzi elfu 10 walionyimwa

Ze Bulldozer

JF-Expert Member
Jun 12, 2020
999
520
Ndugu Wananchi wenzetu,

Mpaka Rais Samia anaingia madarakani zaidi ya watoto wa masikini elfu 10 hawakupewa mikopo,

Leo tayari ameongeza Tshs 106BL sawa na 23% yaani kutoka Tshs 464BL FY2020/21 hadi 570BL FY2021/22

Kwa Sasa,kila mtoto wa masikini aliyefaulu kwenda chuo kikuu kupatiwa mkopo bila kujali historia ya alikosomea shule za chini,

Lakini pia amefuta kabisa ile 6% ya ada ya thamani ya mkopo ( Value Retention Fee-VRF ) kwenye mikopo hiyo na Sasa wanufaika watakatwa 9% ( single digits) FY2021/22 kutoka 15% ya FY2020/21.

Take home za watu hawa zimepaa kwa 6% ,hongereni Sana Mhe Rais.

TLP ni akina nani hata tusione haya na kupongeza na hii ndio maana ya Siasa safi.

Mama chapa kazi tupo na wewe.

TLP Tanzania kwanza,
 
Daaah,

Naona sasa TLP mmeamua kumaliza mchezo,

Ila kama haya yote huyu Mama anafanya basi yeye ni zaidi ya bwana Mkaidi,

Binafsi navutiwa sana na mipango yake mizuri,

Pesa mtaani imeanza kurudi angalau vimiamia tunapata,
 
Aliyewanyima hiyo mikopo alitaka wakajiuze ili wapate kuishi?

Hiyo HESLB nayo ilikuwa kichomi ,

PAYE 9%
HESLB 15%
NHIF 1%
Wafanyakazi 2%

unakatwa karibu 27% kwa mwezi,

Ukirudi nyumbani nikutupa ngumi tu kwa watoto kwa hasira,

Asante sana Rais Samia kura yangu unayo 2025.
 
Nashangaa kelele wanazopiga watu, Mama anafanya vizuri sana tatizo huyu mama sio muuza Sura kama hayati ndio maana wanaona gape,

Mama chapa kazi
 
Na vyama vingine waungeni Mkono TLP kumuunga mkono Rais,

Kazi anazozifanya anahitaji kutiwa moyo,
 
" Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni mama deserves better Wazalendo wote tumtie moyo, mpaka mwaka 2030 tutashuhudia maajabu, Tuombe uzima Tu"
 
Back
Top Bottom