TLP Tanzania: Tunaungana na Watanzania kumpongeza Rais Samia kwa kununua Pamba "Cash" na kuongeza bei kwa 125% FY2021/22

BEI YA PAMBA JUU,TOKA TZS 810 FY2020|21 HADI TZS 1,800 FY2021|22,KILA KONA YA NCHI NI SAMIA SAMIA|SAMIA,NASISI TLP TUNAUNGANA NA WATU HAWA,

Ndg Wananchi,

Bei ya Pamba Tanzania imepanda kutoka Tshs 810/kg FY 2020|21 mpaka Tshs 1,720-1,800/kg FY2021|22 kwa kilo,Hii ni sawa na ongezeko chanya la 125% licha ya awali bei hiyo kuzinduliwa kuwa Tshs 1.050/kg FY2021/22,Kwalugha rahisi kama sio Mama Samia bei ya Pamba leo ingekuwa ni Tshs 1,050/kg,Nidhahiri hapa Mama Samia kapindua Meza,Kasi hii ya Rais Samia Watoto wa Mjini wanaiita "Utajua Hujui" kwa muda huu mfupi wa Mama Samia bei ya Mbaazi, Kawaha, Alizeti, Korosho, Chai zote ziko juu na malipo yote yanafanyika mkono kwa mkono tena by " Cash money" Huko nyuma hawa wakulima wa Pamba Pamoja na kupewa bei ndogo ya Pamba yao bado Watoto hawa wa Masikini waliuza Pamba yao kwa Mkopo,Yaani " Masikini anamkopesha Tajiri " ( this could only happen in Tanzania) huwezi kukuta utaratibu huu popote duniani ila sasa "Mama hataki dhuluma, tumwombee na tumuunge mkono kwa Umoja wetu"

Sisi ni nani tusione haya na kupongeza,

Tunafahamu, Rais Samia amefanya mambo matatu makubwa ambayo TLP tumeyapigania kwa muda mrefu,

1. Kuondoa Urasimu pamoja na jumla ya tozo 232 kwa Wafanya biashara wote wakiwemo hawa wa Pamba,

2. Amepunguza faida kwa Wanunuzi wa Pamba,

3. Ameongeza Wanunuzi Wa Pamba kufikia 30.

TLP - Tanzania Kwanza






" Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni mama deserves better Wazalendo wote tumtie moyo, mpaka mwaka 2030 tutashuhudia maajabu, Tuombe uzima Tu"
 
..kama madai yako ni ya kweli kwanini Mataga na Sukuma Gang wanalaumu kwamba Maza ameshindwa kazi?

..Yani CCM wanashindwa kumtetea mwenyekiti na amiri jeshi mkuu na kazi hiyo sasa inafanywa na wababaishaji wa TLP?
 
Mbona msimu wa pamba ulishapita, au bei ya mwakani? Ila bei ya pamba inategemea soko la dunia
 
MAMA WE LOVE YOU

IMG-20210910-WA0025.jpg
 
Rais Samia ni mpango halisi wa Mungu,Mungu wetu hakawii wala hawai ni huyuhuyu tumepewa tumlinde,
 
Watanzania wengi ni vichwa boga. Current issues zote bado zinatokana na impact ya miaka kadhaa nyuma period . Tangu mwaka juzi waziri mkuu anafanyia KAZI suala la pamba
Huyo ndio aliharibu kabisa na ule mfumo wake wa kumpa mtu kununua mazao
 
Rais Samia ni mpango halisi wa Mungu,Mungu wetu hakawii wala hawai ni huyuhuyu tumepewa tumlinde,
 
Back
Top Bottom