Uchaguzi 2020 TLP na UDP zajiondoa kumpigia debe Magufuli

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,271
22BFED35-E9EB-4834-A3F1-0D06F10FB4CA.jpeg

======

Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini imesema vyama vya Tanzania Labour (TLP) na United Democratic (UDP) ambavyo vilitangaza kumuunga mkono mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, John Magufuli, vilisitisha mpango huo kwa sababu vilikuwa havijafuata kanuni na sheria za uchaguzi.

Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa, Sity Nyahoza, alisema hayo jana wakati akihojiwa na Radio One kwenye kipindi cha Kumepambazuka.

Mapema mwaka huu, Mwenyekiti wa Taifa wa TLP, Augustino Mrema, na Mwenyekiti wa UDP, John Cheyo, kwa nyakati tofauti, walitangaza kuwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu, vyama vyao havitaweka wagombea urais badala yake vitamuunga mkono mgombea wa CCM.

Hata hivyo, Nyahoza jana alisema katika uchaguzi wa mwaka huu, viko vyama ambavyo vilishawahi kupewa onyo na vikarekebishika.

"Mfano kuna Chama cha UDP na TLP walitangazaga kwamba wanamuunga mkono mgombea wa CCM, tukawaambia kuna utaratibu wake, hivyo hamjafuata inabidi mfuate. Wakaona hawajafuata utaratibu ikabidi wakae kimya, sasa hivi unawasikia tena?" Alihoji.

Alisema hivi sasa UDP baada ya kuelezwa walielewa na wanaendelea na kazi zao za kampeni na wana wagombea wao ambao wanaendelea kutangaza sera za chama chao.

Nyahoza alisema TLP kwa upande wake kiliweka hadi na bango na baada ya kuelezwa hakijafuata utaratibu, kiliyatoa sasa wanaendelea na kampeni zao.

"Kwa hiyo vyama ni sikivu, vile ambavyo siyo sikivu wawe wasikivu na kuzingatia sheria na kanuni maana kama mgombea wa chama chako msipokuwa wasikivu ukishinda kwenye uchaguzi itakuwaje," alisema.

Aidha, Nyahoza alisema vyama lazima vitambue kuwa kama huna amani na utulivu huwezi kuwa na uchaguzi.

"Unapokaa jukwaani ukaongea ukanadi sera yako au hata ukaongea mambo yako yawe ya ovyo au ya msingi ujuwe unaongea sababu kuna amani, huwezi kwenda kukaa sehemu risasi zinapigwa, vurugu watu wanafukuzana utapataje muda wa kukaa," alisema.

Aliongeza kuwa msajili wa vyama vya siasa ambaye kisheria ndiye msimamizi na mlezi wa vyama vyote vya siasa, ataendelea kuvishauri na kuvionya vile ambavyo vinakiuka sheria na kanuni.

"Msajili ni mlezi wa vyama vya siasa hivyo inapotokea mtu amekiuka sheria taratibu kwenye kampeni wajibu wake kama mlezi ni kumuonya kwamba unachofanya siyo sahihi, akiendelea kufanya unamuonya tena si unajua mambo ya ulezi tena na ndiyo maana unaona tunawaandikiaga barua sana vyama vya siasa vile ambavyo vinakiuka taratibu na sheria," alisema.
 


Huu ni uthibitisho kuwa political strategist wa CHADEMA na ACT wana akili kuwazidi wa CCM!

CHADEMA na ACT walipita mulemule walipopita TLP na UDP. Na uzuri ni kuwa Si Tume wala Msajili wa vyama waliongea wala kuwakanya.

Sasa wanakumbuka shuka wakati kumeshakucha tayari . It’s too late

Hongereni sana CHADEMA na ACT
 
Back
Top Bottom