TLP Kutoka Chama Cha Upinzani mpaka Sauti ya Wananchi

Masokotz

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
3,494
5,529
Safari ya Chama cha TLP(Tanzania Labour Party) chini ya Mwenyekiti wake Ndugu Augustine Lyatonga Mrema ni ya muda mrefu na iliyokuwa na mapito mengi magumu.TLP ambacho ndicho cha pekee kilichoasisiwa hapa Tanzania ambacho kina itikadi inayoegemea katika upande wa wafanyakazi na ambacho kina amini katika siasa za mageuzi zinazozingatia Uhuru na Usawa.

Chama Cha TLP sio cha kikabaila wala kibepari,kinahubiri siasa ya Ujamaa wa Kidemokrasia ambayo ni moja kati ya aina ya siasa ambazo ni Progressive katika ulimwengu wa leo.Aina hii ya siasa inalenga zaidi kumpa nguvu mwananchi mmoja mmoja na kumjengea uwezi katika kujitegemea yeye mwenyewe na zaidi kumjengea uwezo wa kufanya maamuzi na kushiriki katika hatua zote za maamuzi.

Kabla ya kuendelea nifafanue zaidi kuhusu siasa za SOCIAL DEMOCRATS au DEMOKRASIA YA KIJAMII, Mrengo wa siasa unaongozwa na kanuni inayouliza maswali yafuatayo:
"Kuna sababu ya kumpa mtu haki kama humpatii uwezo wa kuitumia haki hiyo?"
"Kuna sababu gani ya mtu kuwa huru iwapo haiheshimu mipaka ya uhuru wa mwenzake?"
Kuna sababu gani ya kumpa mtu madaraka kama hana uwezo wa kuyatumia?

Maswali haya pamoja na mengine mengi ni maswala ambayo jamii nyingi zinajaribu kutafuta suluhu yake kikiwamo chama cha TLP.TLP inahubiri uhuru unaoheshimu mipaka,Haki ambazo watu wanajengewe uwezo wa kuzitumia"Vyama vya Social Democrat vinapinga kabisa matumizi mabaya ya madaraka na kuhamasisha uwajibikaji.Social Democrat wanahubiri mabadili bila kuwa na fujo au vurugu.Vyama vya Social Democrat vinaamni katika mabadiliko yanayopatikana kwa kushirikiana watawala katika kuleta mabadiliko hatua kwa hatua na kwa kadiri bila kugombana kuzozana,kutukanana,kebehi,matusi,kejeli na dharau.

Baada ya Maelezo hayo napenda sasa nieleze kwa nini TLP sasa ndio sauti ya Wananchi?
  1. Chama cha TLP hakina ubaguzi wa kiitikadi,kiimani,kiuchumi.Ndani ya TLP wanachama wote ni sawa na wana haki sawa.
  2. Chama cha TLP kinaamini katika uwezeshaji wa wananchi katika ujumla wake ikiwamo kuwapatia elimu,na rasilimali zingine zitakazowawezesha kujitegemea na kumudu maisha yao
  3. Chama Cha TLP ndio chama pekee ambacho kina uongozi ambao unao ujasiri wa kukemea pale jambp linapokuwa haliko sawa na wakati huo huo kuunga mkono pale jambp linapokuwa sahihi
  4. TLP ni chama chenye siasa za kistaarabu,kuelimishana na kushauriana katika hali ya staha bila kujali,hali ya mtu
  5. TLP ni chama ambacho kina uwezo wa kuwasemea wananchi katika masuala mbalimbali ambayo yanahitaji kusemwa kwa watawala kwa ujasiri ni bila kubagua
Kwa wanasiasa TLP ni jukwa bora kabisa la kujifunza,kujijenga na kukua katika misingi ya uongozi wa kizalendo na kujali watu.Unapojiunga na TLP unapata fursa ya kuona kwa hakika nafasi yako katika ujenzi wa Taifa na kupata ujasiri wa kusimama na kufanya jambo kwa ajili ya TAIFA lako.

Karibuni tujadi hasa kuhusu SIASA za DEMOKRASIA ya UJAMAA hasa katika kipindi hiki cha uchaguzi na Nafasi ya TLP katika ujenzi wa Jamii mpya ya Watanzania ambao ni Wazalendo na Wachapakazi.
 
Ndiyo maana mwenyekiti wenu na Katibu Mkuu wote Wachagga wa Kiraracha. Bure kabisa nyie.
 
Umeshakunya leo? Kama unafamilia waonyeshe hili bandiko lako alafu watazame nyuso zao.
 
Back
Top Bottom