Elections 2010 TLP isiingie kwenye kambi ya upinzani

Mwanamayu

JF-Expert Member
May 7, 2010
11,329
6,447
Kama Chadema watawakaribisha wapinzani wengine kwenye kambi hiyo Bungeni basi TLP iachwe kabisa kwani ni hatari kama UKIMWI. Mrema amekuwa akimpigia kampeni JK kwenye jimbo lake badala ya aliyekuwa mgombea Urais kupitia TLP.

Kumweka Mrema kwenye kambi hiyo mambo hayatakwenda kama itakavyokuwa inapangwa.
 
Correct!!

Acha Mrema arudi CCM ingawa alipata kura yangu mwaka 1995. Kam walivyo watu wa CCM wote, yeye pia anatanguliza ubinafsi kuliko utaifa. CCM wamatufundisha kuwa wanachotaka ni ushindi hata kwa kubomoa umoja wa taifa hili kwa kutumia misingi ya udini. Huo ni ubinafsi wa hali ya juu kuliko utaifa.
 
Kama Chadema watawakaribisha wapinzani wengine kwenye kambi hiyo Bungeni basi TLP iachwe kabisa kwani ni hatari kama UKIMWI. Mrema amekuwa akimpigia kampeni JK kwenye jimbo lake badala ya aliyekuwa mgombea Urais kupitia TLP.

Kumweka Mrema kwenye kambi hiyo mambo hayatakwenda kama itakavyokuwa inapangwa.

Mwanamayu nakuunga mkono kwa hilo huyo jamaa ni hatari sana Chadema wakimkaribisha tu ataomba awe kiongozi wa upinzani bungeni anapenda sana cheo na atavuruiga kila kitu hapo katika kambi ya upinzani.
 
madhara ya kuchanganyikiwa kwa "msee wa inji hii"
mana kapoteza uelekeo.. alisema "biashara ya jumla imemshinda hivyo akawaomba ccm wamuunge mkono kwenye biashara ya jumla
 
Atatumiwa sana na ccm kama agent wa kuvujisha siri kwa fedha!...Ni wa kumkwepa sana huyu!
 
Naunga mkono hoja, huyu jamaa hastahili kabisa kuwa katika kambi ya Upinzani
 
Wakuu tusipoteze muda kujadili TLP na hasa chini ya Mrema. Tawi la mwembe hata siku moja haliwezi kuwa mchungwa. Sasa TLP itaingiaje kambi ya upinzani wakati ni tawi la ccm?
 
Mzee wa kiraracha ni mgonjwa hata kumwingiza kwenye kambi ya upinzani ni kumwonea kwani yeye ni mwana ccm mwadilifu.
 
Yule babu anayesema dr.slaa/chadema akubali matokeo sababu jeykey anakubalika!?? Uyu si mpinzani ni kipandikizi. Chadema mukimbie mbali na kichaa aliyepewa rungu la Vunjo!
 
Nilikua natafakari kwa nini wana Vunjo walimuacha mgombea wa CCM na CHADEMA wakamchagua Mrema ambaye ni kada wa CCM , bali sijapata jibu sahihi ila ukweli ni kwamba Mrema akiingia kambi ya Upinzani ataleta shida kubwa sana ila kwasababu tuna vijana makini na viongozi makini wa upinzani tunaamini wiki ijayo Mambo yatakua vizuri na tutapata jibu bila shaka

Mzee GOMEZI
 
Alipigiwa kura za huruma, si mnamuona alivyojichokea, huruma tu !!!!!!!
 
Nilikua natafakari kwa nini wana Vunjo walimuacha mgombea wa CCM na CHADEMA wakamchagua Mrema ambaye ni kada wa CCM , bali sijapata jibu sahihi ila ukweli ni kwamba Mrema akiingia kambi ya Upinzani ataleta shida kubwa sana ila kwasababu tuna vijana makini na viongozi makini wa upinzani tunaamini wiki ijayo Mambo yatakua vizuri na tutapata jibu bila shaka

Mzee GOMEZI

Kwenye mkutano wa ccm pale chimwaga alipokaribishwa kutoa salam aliwaomba ccm wamsaidie kushinda ubunge vunjo huku yeye akiwasaidia kampeni za JK jimboni humo, kwahiyo ccm vunjo wametekeleza makubaliano waliyokuwa nayo na mzee wa kiraracha.
 
Mimi sijui tunajifunza nini kila tunapomuona Mrema! Mkumbuke ndio huyu aliyekuwa anatoa siku saba kila kitu. Kweli amechoka!! Bado somo haliningii kila nikitaka kumsoma.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom