TLP Arusha wamtimua Mwenyekiti na Katibu wa mkoa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TLP Arusha wamtimua Mwenyekiti na Katibu wa mkoa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by JamiiForums, May 17, 2012.

 1. JamiiForums

  JamiiForums Official Robot Staff Member

  #1
  May 17, 2012
  Joined: Nov 9, 2006
  Messages: 5,100
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Posted by Kabonde | May 15, 2012

  Wanachama wa TLP mkoa wa Arusha wamemtimua Mwenyekiti wa mkoa Bwana Leonard Makanza na Katibu wa Mkoa Bi Mwamvua Wahanza kwa makosa ya kuyumbisha chama na kukisababishia hasara kubwa.

  Bwana Makanza na Bibi Wahanza pia wanashutumiwa kwa kitendo cha kumchagua mgombea ubunge wa jimbo la Arumeru Mashariki ambaye si mwanachama wa TLP na kuambulia kura 18 tu huku rasilimali za chama fedha, gari la matangazo na viongozi wa chama makao makuu wakiambulia aibu kubwa.

  Mgombea wa TLP Bwana A Chipaka mkazi wa Sekei mkabala na Hotel ya Mount Meru ni mwanachama wa CHADEMA hata nyumbani kwake bendera ya CHADEMA inapepea iweje agombee kupitia TLP mwenyekiti na katibu walikuwa wapi?.

  Bwana Abrahamu Chipaka alipanda mara kadhaa katika jukwaaa la CHADEMA na kumnadi mgombea wa CHADEMA huku akisisitiza kura zisigawanywe.

  Bwana Leonard Makanza amekaimu nafasi ya mwenyekiti wa mkoa kwa zaidi ya miaka mitano bila kuitisha uchaguzi wowote.Pia anatuhumiwa kwa kutoitisha mikutano ya ndani na nje na kujenga makundi miongoni mwa wanachama.

  Tayari Mwenyekiti wa Taifa Bwana A L Mrema amejulishwa na amebariki hatua ya wanachama wa TLP mkoa wa Arusha
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 2. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #2
  May 17, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,250
  Likes Received: 3,854
  Trophy Points: 280
  Hiki ni chama au NGOs ya Mrema inayofadiriwa kwa hisani ya watu wa ccm?
   
Loading...