Return Of Undertaker
JF-Expert Member
- Jun 12, 2012
- 4,572
- 26,868
MTANZANIA FIKIRI TOFAUTI.
CCM imeshindwa kugawa milioni 50 kila kijiji Kama walivyotuahidi, cha ajabu wameamua kukusanya shilingi elfu 20,000/= kwa kila mtanzania kwa kile kinachoitwa KITAMBULISHO CHA MJASIRIAMALI. Hiyo ndiyo zawadi ya CCM kwa watanzania wanyonge, walalahoi na wavuja jasho wa nchi hii wanaoteseka kwa kudunduliza kwenye biashara zao ndogo ndogo kila siku.
Juzi tu tumeskia serikali kupitia mkuu wa mkoa wa Ruvuma mh sofia Mndeme akitangaza kwa wananchi kuwa HATA WAOKOTA MAKOPO NI LAZIMA WAPEWE VITAMBULISHO,, kwa Mujibu wa Mh rais wakati anazindua vitamvulisho hivo alisema ni kwaajili ya Machinga ili wafanye kazi yao bila kusumbuliwa sasa inakuwaje inageuka kuwa njia ya kudai kodi kwa lazima kwa kila mtanzania hasa wafanyabiashara mpaka Wale walio na mfumo rasmi kutakiwa kuwa na vitambulisho. Hivi tatizo ni nini?
Huku hayo yakiendelea tunashuhudia Mbunge wa mbeya mjini Joseph Mbilinyi "Sugu" akishikiliwa na polisi kwa mahojiano mara baada ya kusambaa video clip ikimuonesha mbunge huyo akizungumza na kusikiliza kero za wananchi wa Jimbo lake kuhusu vitambulisho vya mjasiriamali, kwa mujibu wa mh Sugu alisema vitabulisho hivo ni kwajili ya wamachinga na wafanya biashara wasio na mfumo rasmi, mama ntilie wana mfumo rasmi ndio maana mabwana afya wanawakagua. Pia ili kuondoa utata kuhusu ugawaji wa vitambulisho hivo kuhusu nani anatakiwa apate na nani hatakiwi kupewa kitambulisho hicho, aliwaahidi wananchi kuwa ataenda kuuliza bungeni ili kupata ukweli halisi. Swali langu ni je nini sababu ya kukamatwa kwa mbunge huyo au mbunge kutatua kero za wapiga kura wake imekuwa tatizo??
Serikali ya wanyonge inawekeza nguvu nyingi sana kudai kodi mpaka kwa wanyonge badala ya kutoa fursa kwao ili waweze kulipa kodi kutokana na vipato wanavyopata.
Kumbuka kuwa wanyonge hawa hawa ndio ambao serikali iliwaahidi kununua korosho zote na kuwalipa kwa wakati lakini mpaka sasa kuna wakulima hawajalipwa, serikali inashindwa kuwa mkweli kwa wapiga kura wake alafu wakati huo huo inataka iaminiwe kwenye uchaguzi, There is no such Ignorant Citizens any more!
Serikali hii hii ya CCM kupitia mwenyekiti wake ambaye ni mh rais Magufuli October 28 2018 aliahidi kuwa serikali itanunua korosho zote za wakulima lakin serikali ile ile leo February 2019 , inawaita tena wafanyabiashara ambao iliwakataa awali nakusema kuwa itanunua korosho zote na pesa zipo. HAWA SIO WATU WAKUWAAMINI HATA KIDOGO.
serikali inatakiwa kujitafakari sana kwa hili.
Godwin Mrina
Mwananchi wa kawaida