Tizama wanaotakiwa kuwa na kitambulisho cha Magufuli, hii ni baada ya kushindwa kugawa mil 50 kila kijiji wanakusanya 20,000 kwa walala hoi

MTANZANIA FIKIRI TOFAUTI.

CCM imeshindwa kugawa milioni 50 kila kijiji Kama walivyotuahidi, cha ajabu wameamua kukusanya shilingi elfu 20,000/= kwa kila mtanzania kwa kile kinachoitwa KITAMBULISHO CHA MJASIRIAMALI. Hiyo ndiyo zawadi ya CCM kwa watanzania wanyonge, walalahoi na wavuja jasho wa nchi hii wanaoteseka kwa kudunduliza kwenye biashara zao ndogo ndogo kila siku.

Juzi tu tumeskia serikali kupitia mkuu wa mkoa wa Ruvuma mh sofia Mndeme akitangaza kwa wananchi kuwa HATA WAOKOTA MAKOPO NI LAZIMA WAPEWE VITAMBULISHO,, kwa Mujibu wa Mh rais wakati anazindua vitamvulisho hivo alisema ni kwaajili ya Machinga ili wafanye kazi yao bila kusumbuliwa sasa inakuwaje inageuka kuwa njia ya kudai kodi kwa lazima kwa kila mtanzania hasa wafanyabiashara mpaka Wale walio na mfumo rasmi kutakiwa kuwa na vitambulisho. Hivi tatizo ni nini?

Huku hayo yakiendelea tunashuhudia Mbunge wa mbeya mjini Joseph Mbilinyi "Sugu" akishikiliwa na polisi kwa mahojiano mara baada ya kusambaa video clip ikimuonesha mbunge huyo akizungumza na kusikiliza kero za wananchi wa Jimbo lake kuhusu vitambulisho vya mjasiriamali, kwa mujibu wa mh Sugu alisema vitabulisho hivo ni kwajili ya wamachinga na wafanya biashara wasio na mfumo rasmi, mama ntilie wana mfumo rasmi ndio maana mabwana afya wanawakagua. Pia ili kuondoa utata kuhusu ugawaji wa vitambulisho hivo kuhusu nani anatakiwa apate na nani hatakiwi kupewa kitambulisho hicho, aliwaahidi wananchi kuwa ataenda kuuliza bungeni ili kupata ukweli halisi. Swali langu ni je nini sababu ya kukamatwa kwa mbunge huyo au mbunge kutatua kero za wapiga kura wake imekuwa tatizo??

Serikali ya wanyonge inawekeza nguvu nyingi sana kudai kodi mpaka kwa wanyonge badala ya kutoa fursa kwao ili waweze kulipa kodi kutokana na vipato wanavyopata.

Kumbuka kuwa wanyonge hawa hawa ndio ambao serikali iliwaahidi kununua korosho zote na kuwalipa kwa wakati lakini mpaka sasa kuna wakulima hawajalipwa, serikali inashindwa kuwa mkweli kwa wapiga kura wake alafu wakati huo huo inataka iaminiwe kwenye uchaguzi, There is no such Ignorant Citizens any more!

Serikali hii hii ya CCM kupitia mwenyekiti wake ambaye ni mh rais Magufuli October 28 2018 aliahidi kuwa serikali itanunua korosho zote za wakulima lakin serikali ile ile leo February 2019 , inawaita tena wafanyabiashara ambao iliwakataa awali nakusema kuwa itanunua korosho zote na pesa zipo. HAWA SIO WATU WAKUWAAMINI HATA KIDOGO.

serikali inatakiwa kujitafakari sana kwa hili.

Godwin Mrina
Mwananchi wa kawaidaView attachment 1028841
Eti wachinjaji kuku!😳 serikali imefilisika hii si bure! Hakuna cha dona kantre kwa style hii!
 
Mkuu samahani Naomba Uthibitishe hii habari yako, Je kama Umejiandikia na Uka Print,Sema Source yake ni wapi?
2.Hata Kama ni Kweli Itasaidia wengine kulipa Makodi makubwa,Instead unalipa 20,000 tuu kwa Mwaka!
MTANZANIA FIKIRI TOFAUTI.

CCM imeshindwa kugawa milioni 50 kila kijiji Kama walivyotuahidi, cha ajabu wameamua kukusanya shilingi elfu 20,000/= kwa kila mtanzania kwa kile kinachoitwa KITAMBULISHO CHA MJASIRIAMALI. Hiyo ndiyo zawadi ya CCM kwa watanzania wanyonge, walalahoi na wavuja jasho wa nchi hii wanaoteseka kwa kudunduliza kwenye biashara zao ndogo ndogo kila siku.

Juzi tu tumeskia serikali kupitia mkuu wa mkoa wa Ruvuma mh sofia Mndeme akitangaza kwa wananchi kuwa HATA WAOKOTA MAKOPO NI LAZIMA WAPEWE VITAMBULISHO,, kwa Mujibu wa Mh rais wakati anazindua vitamvulisho hivo alisema ni kwaajili ya Machinga ili wafanye kazi yao bila kusumbuliwa sasa inakuwaje inageuka kuwa njia ya kudai kodi kwa lazima kwa kila mtanzania hasa wafanyabiashara mpaka Wale walio na mfumo rasmi kutakiwa kuwa na vitambulisho. Hivi tatizo ni nini?

Huku hayo yakiendelea tunashuhudia Mbunge wa mbeya mjini Joseph Mbilinyi "Sugu" akishikiliwa na polisi kwa mahojiano mara baada ya kusambaa video clip ikimuonesha mbunge huyo akizungumza na kusikiliza kero za wananchi wa Jimbo lake kuhusu vitambulisho vya mjasiriamali, kwa mujibu wa mh Sugu alisema vitabulisho hivo ni kwajili ya wamachinga na wafanya biashara wasio na mfumo rasmi, mama ntilie wana mfumo rasmi ndio maana mabwana afya wanawakagua. Pia ili kuondoa utata kuhusu ugawaji wa vitambulisho hivo kuhusu nani anatakiwa apate na nani hatakiwi kupewa kitambulisho hicho, aliwaahidi wananchi kuwa ataenda kuuliza bungeni ili kupata ukweli halisi. Swali langu ni je nini sababu ya kukamatwa kwa mbunge huyo au mbunge kutatua kero za wapiga kura wake imekuwa tatizo??

Serikali ya wanyonge inawekeza nguvu nyingi sana kudai kodi mpaka kwa wanyonge badala ya kutoa fursa kwao ili waweze kulipa kodi kutokana na vipato wanavyopata.

Kumbuka kuwa wanyonge hawa hawa ndio ambao serikali iliwaahidi kununua korosho zote na kuwalipa kwa wakati lakini mpaka sasa kuna wakulima hawajalipwa, serikali inashindwa kuwa mkweli kwa wapiga kura wake alafu wakati huo huo inataka iaminiwe kwenye uchaguzi, There is no such Ignorant Citizens any more!

Serikali hii hii ya CCM kupitia mwenyekiti wake ambaye ni mh rais Magufuli October 28 2018 aliahidi kuwa serikali itanunua korosho zote za wakulima lakin serikali ile ile leo February 2019 , inawaita tena wafanyabiashara ambao iliwakataa awali nakusema kuwa itanunua korosho zote na pesa zipo. HAWA SIO WATU WAKUWAAMINI HATA KIDOGO.

serikali inatakiwa kujitafakari sana kwa hili.

Godwin Mrina
Mwananchi wa kawaidaView attachment 1028841

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waandamanaji wa kuunga juhudi bila kutafakari madhara ya baadae ya kile wanachokiunga mkono kwa sasa watakuwa wanajutia maamuzi yao ya kukurupuka kuunga mkono kitu ambacho hujui matokeo yake ya baadae yatakuaje,ili mradi aliyesema ni fulani basi wewe bila hata hujatafakari uko barabarani kuandamana kuunga mkono juhudi zake unapaparika kama kuku aliyekatwa kichwa, mazingira kama haya ndiyo yanayozidi kumuweka Lissu katika chati ya juu kuwa ndiye mtu wa tofauti anayeweza kulipokea jambo kwa kulitafakari na kujua faida zake na hasara zitakazo kuja baadae.
 
#ccm ni jinamizi... #ccm ni genge hatari sana dhidi ya wananchi wa Tanzania..
Tatizo wananchi wengi nao mlinga mlinga tu; hawaoni wala hawasikii..!!
Kinachoudhi zaidi hawajui walipo wala wanapotaka kwenda..!!
 
Familia hujengwa na wanafamilia vivyo hivyo nchi hujengwa na wananchi, ukusubiri vya kuletewa huambatana na masimango na masharti mengine ya kudhalilisha utu wako.
 
Wauza karanga... kitammbulisho elfu20, mtaji elfu5... hii inaitwa nguvu zako ndiyo mtaji wao...

Naona ma- house girl wamepona...

Cc: mahondaw
 
Hadi wapaka kucha??
Sasa hao vibanda vya mpesa na tgpesa ni wanalipa kodi na wana leseni za biashara?
 
Inamana ukiwa na hivyo vitambulisho. Kwa hayo makundi mf no 11 inamana hulipi Tena Kodi TRA? Then hivyo vitambulisho baada ya kununua utahitajika Tena kuvilipia ama??!! Full mikanganyo loh!!
 
Back
Top Bottom