Tizama wanaotakiwa kuwa na kitambulisho cha Magufuli, hii ni baada ya kushindwa kugawa mil 50 kila kijiji wanakusanya 20,000 kwa walala hoi

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,547
2,000
MTANZANIA FIKIRI TOFAUTI.

CCM imeshindwa kugawa milioni 50 kila kijiji Kama walivyotuahidi, cha ajabu wameamua kukusanya shilingi elfu 20,000/= kwa kila mtanzania kwa kile kinachoitwa KITAMBULISHO CHA MJASIRIAMALI. Hiyo ndiyo zawadi ya CCM kwa watanzania wanyonge, walalahoi na wavuja jasho wa nchi hii wanaoteseka kwa kudunduliza kwenye biashara zao ndogo ndogo kila siku.

Juzi tu tumeskia serikali kupitia mkuu wa mkoa wa Ruvuma mh sofia Mndeme akitangaza kwa wananchi kuwa HATA WAOKOTA MAKOPO NI LAZIMA WAPEWE VITAMBULISHO,, kwa Mujibu wa Mh rais wakati anazindua vitamvulisho hivo alisema ni kwaajili ya Machinga ili wafanye kazi yao bila kusumbuliwa sasa inakuwaje inageuka kuwa njia ya kudai kodi kwa lazima kwa kila mtanzania hasa wafanyabiashara mpaka Wale walio na mfumo rasmi kutakiwa kuwa na vitambulisho. Hivi tatizo ni nini?

Huku hayo yakiendelea tunashuhudia Mbunge wa mbeya mjini Joseph Mbilinyi "Sugu" akishikiliwa na polisi kwa mahojiano mara baada ya kusambaa video clip ikimuonesha mbunge huyo akizungumza na kusikiliza kero za wananchi wa Jimbo lake kuhusu vitambulisho vya mjasiriamali, kwa mujibu wa mh Sugu alisema vitabulisho hivo ni kwajili ya wamachinga na wafanya biashara wasio na mfumo rasmi, mama ntilie wana mfumo rasmi ndio maana mabwana afya wanawakagua. Pia ili kuondoa utata kuhusu ugawaji wa vitambulisho hivo kuhusu nani anatakiwa apate na nani hatakiwi kupewa kitambulisho hicho, aliwaahidi wananchi kuwa ataenda kuuliza bungeni ili kupata ukweli halisi. Swali langu ni je nini sababu ya kukamatwa kwa mbunge huyo au mbunge kutatua kero za wapiga kura wake imekuwa tatizo??

Serikali ya wanyonge inawekeza nguvu nyingi sana kudai kodi mpaka kwa wanyonge badala ya kutoa fursa kwao ili waweze kulipa kodi kutokana na vipato wanavyopata.

Kumbuka kuwa wanyonge hawa hawa ndio ambao serikali iliwaahidi kununua korosho zote na kuwalipa kwa wakati lakini mpaka sasa kuna wakulima hawajalipwa, serikali inashindwa kuwa mkweli kwa wapiga kura wake alafu wakati huo huo inataka iaminiwe kwenye uchaguzi, There is no such Ignorant Citizens any more!

Serikali hii hii ya CCM kupitia mwenyekiti wake ambaye ni mh rais Magufuli October 28 2018 aliahidi kuwa serikali itanunua korosho zote za wakulima lakin serikali ile ile leo February 2019 , inawaita tena wafanyabiashara ambao iliwakataa awali nakusema kuwa itanunua korosho zote na pesa zipo. HAWA SIO WATU WAKUWAAMINI HATA KIDOGO.

serikali inatakiwa kujitafakari sana kwa hili.

Godwin Mrina
Mwananchi wa kawaida
FB_IMG_1550826149625.jpg
 
whizkid

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
344
250
Kama nakumbuka vizuri, lengo lilikuwa kwa wafanyabiashara wenye annual revenue ya milioni 4, yaani kama 11,000 kwa siku. Kwenye hiyo list wengi wanavuka na tayari wapo kwenye taratibu vingine. Mfano, kwenye list za viwanda za wizara utashangaa pia kuwakuta mafundi welding, mafundi seremala, washonaji n.k. kuwa nao ni viwanda vidogo na huko wana taratibu zao za usajili na kodi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kinyungu

JF-Expert Member
Apr 6, 2008
9,401
2,000
Magufuli aliahidi mil 50 kila kijiji ili ziwasaidie wachuuzi na wenye hali ngumu sasa naona kawageuka anataka wao ndiyo wamchangie Magufuli ili awapelekee maisha bora. Kweli kuwa uyaone!
 
adakiss23

JF-Expert Member
Jan 23, 2011
3,561
2,000
Hii kitu ni hatari sana. Kama unaweza kutamka kuwa tanzania ni donor country that means raia wako wanaweza kujimudu kwa kuwawezesha wewe na serikali yako. Kuwatoza kodi raia wako wa chini (according to aina ya kazi wanazofanya) ni kuwahadaa na kuwaumiza raia wako.
Ni bora ukawaambia ukweli wa hali ya nchi ilivyo watoe hiyo tozo kwa moyo m1 wakijua nchi inahitaji pesa kujiendesha.
 
deonova

JF-Expert Member
Apr 22, 2013
742
500
Kwa hiyo wamehalalisha biashara ya Kuburn CD? manake hapo namba 19 wamewaweka wakati huku wasanii wanalia na Piracy dhidi ya kazi zao za sanaa. Ukishampa Kitambulisho huyu wa kuburn CD mtaani ndo umesharasimisha kazi yake ya Piracy so hata COSOTA hawamwambii kitu oote
 
Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
76,125
2,000
MTANZANIA FIKIRI TOFAUTI.

CCM imeshindwa kugawa milioni 50 kila kijiji Kama walivyotuahidi, cha ajabu wameamua kukusanya shilingi elfu 20,000/= kwa kila mtanzania kwa kile kinachoitwa KITAMBULISHO CHA MJASIRIAMALI. Hiyo ndiyo zawadi ya CCM kwa watanzania wanyonge, walalahoi na wavuja jasho wa nchi hii wanaoteseka kwa kudunduliza kwenye biashara zao ndogo ndogo kila siku.

Juzi tu tumeskia serikali kupitia mkuu wa mkoa wa Ruvuma mh sofia Mndeme akitangaza kwa wananchi kuwa HATA WAOKOTA MAKOPO NI LAZIMA WAPEWE VITAMBULISHO,, kwa Mujibu wa Mh rais wakati anazindua vitamvulisho hivo alisema ni kwaajili ya Machinga ili wafanye kazi yao bila kusumbuliwa sasa inakuwaje inageuka kuwa njia ya kudai kodi kwa lazima kwa kila mtanzania hasa wafanyabiashara mpaka Wale walio na mfumo rasmi kutakiwa kuwa na vitambulisho. Hivi tatizo ni nini?

Huku hayo yakiendelea tunashuhudia Mbunge wa mbeya mjini Joseph Mbilinyi "Sugu" akishikiliwa na polisi kwa mahojiano mara baada ya kusambaa video clip ikimuonesha mbunge huyo akizungumza na kusikiliza kero za wananchi wa Jimbo lake kuhusu vitambulisho vya mjasiriamali, kwa mujibu wa mh Sugu alisema vitabulisho hivo ni kwajili ya wamachinga na wafanya biashara wasio na mfumo rasmi, mama ntilie wana mfumo rasmi ndio maana mabwana afya wanawakagua. Pia ili kuondoa utata kuhusu ugawaji wa vitambulisho hivo kuhusu nani anatakiwa apate na nani hatakiwi kupewa kitambulisho hicho, aliwaahidi wananchi kuwa ataenda kuuliza bungeni ili kupata ukweli halisi. Swali langu ni je nini sababu ya kukamatwa kwa mbunge huyo au mbunge kutatua kero za wapiga kura wake imekuwa tatizo??

Serikali ya wanyonge inawekeza nguvu nyingi sana kudai kodi mpaka kwa wanyonge badala ya kutoa fursa kwao ili waweze kulipa kodi kutokana na vipato wanavyopata.

Kumbuka kuwa wanyonge hawa hawa ndio ambao serikali iliwaahidi kununua korosho zote na kuwalipa kwa wakati lakini mpaka sasa kuna wakulima hawajalipwa, serikali inashindwa kuwa mkweli kwa wapiga kura wake alafu wakati huo huo inataka iaminiwe kwenye uchaguzi, There is no such Ignorant Citizens any more!

Serikali hii hii ya CCM kupitia mwenyekiti wake ambaye ni mh rais Magufuli October 28 2018 aliahidi kuwa serikali itanunua korosho zote za wakulima lakin serikali ile ile leo February 2019 , inawaita tena wafanyabiashara ambao iliwakataa awali nakusema kuwa itanunua korosho zote na pesa zipo. HAWA SIO WATU WAKUWAAMINI HATA KIDOGO.

serikali inatakiwa kujitafakari sana kwa hili.

Godwin Mrina
Mwananchi wa kawaida View attachment 1028841
Noma sana !
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom