Tizama uchumi unavyokuwa toka awamu ya Nyerere hadi Magufuli, CCM wako vizuri

Mkapa aliipokea ikiwa 500 akaondoka ikiwa 1050 ...alieipokea 1050 kaondoka ikiwa 2210 kuna mtu ataondoka ikiwa 4200
 
Usiongee kibashite bashite tangu tulipopata Uhuru mpaka vita vya Idd Amin uchumi ulikuwa unakuwa kila mwaka.Miaka hiyo aliweza kujenga viwanda,vufuo umeme,kutoa matibabu na elimu bila malipo.Kukua huko kwa uchumi kiliwezesha kuajiriwa kila muhitimu wa kuanzia kidato cha nne.
Unawezeje kufananisha na uhabithi na komedi ya 7% unaondelea sasa?
Na kwa umuhimu zaidi ukuaji uliweza kuwagusa wakulima ambao ndiyo wengi zaidi. Uwepo wa processing industries, agro cooperatives na hata tume ya bei ya mazao ulihakikisha mkulima anafaidika moja kwa moja na nguvu zake.

Ninaamini kama Mwalimu asinge bow down kirahisi dhidi ya uliberali mamboleo, basi nchi yetu ingekuwa level za Malaysia, Singapore, Taiwan na hata South Korea. Yaani tulikuwa on the right track. Mpaka IMF na sera zao za kipuuzi walipokuja, ndipo tukapoteza mwelekeo.

Sasa tunahitaji mawazo mbadala na kwa umuhimu zaidi chama mbadala. Tuondokane na maCCM, ndipo tunaweza kuwa na mwelekeo tena.
 
Report za WB kuhusu -ve growth awamu ya Nyerere ni propaganda za kuondoa ujamaa. Wazungu ni waongo na walaghai, uchumi wa Tanzania kukua (GDP) inachangiwa na wawekezaji kutoka nje kwa asilimia nyingi.

Mfumo wa thamani ya TZS - USD ni siasa tusizozijua mpaka sasa, ila tunajua kidogo sana kwamba "demand and supply" ya inachangia kupanda na kushuka kwa "exchange rates"
 
Katika watu wasiotumia ubongo wao vizuri ni wewe.Enzi za JKN Taifa lilikuwa na Viwanda vya nguo,viatu,ngozi,nyama,maziwa,matairi.

Kulikuwa na bank ya nyumba,NBC,Bank ya ushirika,RTC,NIC,State Travelling corp..............duh leo tuna kitu gani??

Tuanshindwa hata kutengeneza wembe.kama hujui sema hujui uelimishwe.
Asilimia 90% ya ulivyovitaja mpaka Mwinyi anaingia NBC pekee ndio ilikuwa ikipata faida. Mengine yalikuwa yakipata hasara na kuendshwa kwa ruzuku ya serikali kupitia kodi na miaada ya maendeleo na mikopo.
Nenda kapate elimu ya namna uchumu ulivyokuwa kabla ya ubinafsishaji kwa Dr Charles Kimei utaelewa.
 
Kushusha thamani ya shilingi ni kuongeza mzigo mkubwa wa gharama za maisha kwa Watanzania.

Exchange ya Tsh 2200 kwa $1 ingekuwa ni faida kwetu kama tungekuwa na vitu vya kuuza nje.

Wakati mwingine benki kuu inaweza ikashusha thamani ya fedha ili kuhamasisha wanunuzi wa kigeni kununua bidhaa kwa wingi (purposefully the centeral bank decides to depreciate the currency to boost importation)
 
Exchange ya Tsh 2200 kwa $1 ingekuwa ni faida kwetu kama tungekuwa na vitu vya kuuza nje.

Wakati mwingine benki kuu inaweza ikashusha thamani ya fedha ili kuhamasisha wanunuzi wa kigeni kununua bidhaa kwa wingi (purposefully the centeral bank decides to depreciate the currency to boost importation)
Mkuu watu hawalijui hilo kuna siku Nyerere alihutubia pale Mang'ula alipoalikwa kufungua karakana ya mataluma alimpiga vijembe mwinyi na serikali yake baada ya kukimbilia kushusha thamani ya pesa alisema " Ninyi watanzania mnashusha thamani ya pesa kwa manufaa ya nani? Marekani wakiona wamezalisha vitu vingi na havinunuliki ndani wanashusha thamani ya dola ili watu kutoka nje wanunue mali yao ya ndani vile vile wakiona wnataka kuagiza mali kutoka nje wanapandisha thamani ya dola yao. Sasa ninyi watanzania na hiyo shilingi yenu mnamsaidia nani kushusha thamani ya dola????" watu hawaelewi kabisa hii dhana ya thamani ya shilingi yetu...
 
Kushusha thamani ya shilingi ni kuongeza mzigo mkubwa wa gharama za maisha kwa Watanzania.
Yes kama tu wananchi wanategemea kuagiza bidhaa wanazotumia kila siku kutoka ng'ambo
 
Tatizo la nchi hii wenye akili nyingi wamekaa kimya, wenye akili kidogo wanapuyanga miaka nenda rudi. Kutawala imekuwa dili kuliko kila kitu. Wacha watawale, labda ngoja tuone JPM.
 
Katika watu wasiotumia ubongo wao vizuri ni wewe.Enzi za JKN Taifa lilikuwa na Viwanda vya nguo,viatu,ngozi,nyama,maziwa,matairi.

Kulikuwa na bank ya nyumba,NBC,Bank ya ushirika,RTC,NIC,State Travelling corp..............duh leo tuna kitu gani??

Tuanshindwa hata kutengeneza wembe.kama hujui sema hujui uelimishwe.
Kubali tu kwamba wewe ni kiazi, uchumi wa ncho haulinganishwi kwa kutumia currency'
 
lakini pia tukumbuke wakati wa mwinyi..IMF na world bank walitoa sharti la kudevaluate currency yetu ili tuweze kupata mikopo kutoka kwao.
 
Lakini tulikuwa na minus economic growth kwa kipindi chote, na masikini walikuwa wengi kuliko kipindi chochote ktk Historia ya Tanzania, Tanzania yetu imeanza kukua Kiuchumi kipindi cha Mzee Mwinyi, ndiyo tukaanza kuwa na positive economic growth ambayo imeendelea mpaka leo hii!


Kwa uongo ulioandika nimekudharau sana, kumbe wewe unama.. kichwani eti
 
Back
Top Bottom