Tizama Nigeria uchaguzi huru na haki, kura zinahesabiwa kweupe raia wakishuhudia, sio kwetu mkakae nyumbani mita 1,000. Kwa hii CCM hawatakubali kamwe

Hivi zihesabiwe live hivyo khali siitakuwa sio khaki
Acha bhana unaona mgombea wako anavyogalagazwa. Utaokota mawe
 
Nimeipenda sana hii na kuifuatilia "Live on Al Jazeera, CNN, and BBC". Kwa uchaguzi wetu huu wa akina Jecha and Co. tunachoma pesa za wananchi masikini bure tu.

Afadhali hizi pesa tunazoharibu kwenye hizi tunazoita chaguzi tungeongezea vyumba vya madarasa watoto wetu wasomee, tungehesabu.
 
Muda mwengine mabadiliko yanaanza na wewe,kama hadi leo bado kuna watu wanapigia kura ccm tena wana mapenzi ya damu na ccm,kwa hali hiyo hata wangekuwa viongozi wazungu wangefanya kama wafanyavyo ccm.
 
Kabla ya election kufanyika serikali Ilijaribu kutoa tamko linalo wataka wananchi kurudi nyumbani mara moja baada ya kuwa wameshapiga kura

Wanaharakati wakaijia serikali juu " na davido alikuwepo kwenye huo mumbo-jumbo aliiponda sana serikali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom