Tishio la Wana CCM kukimbilia CHADEMA limeugeuza moyo wa Farao | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tishio la Wana CCM kukimbilia CHADEMA limeugeuza moyo wa Farao

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Apr 28, 2012.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Apr 28, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]

  Tangu kuibuka kwa wimbi la mkaguzi wa mahesabu ya serikali kuanika hadharani uvujaji wa pesa za umma serikalini, hali iliyosababisha wabunge kuivimbishia mishipa serikali wakiongozwa na wabunge wa upinzani kinara akiwa Zito kabwe, ambaye amezua mtafaruku mkubwa ndani ya CCM kwa kuanzisha mchakacho wa kukusanya sahihi za wabunge wasiopungua sabini ikiwa ni asilimia 20 ya wabunge kujenga hoja ya kupiga kura ya siri ya kutokuwa na imani na Waziri mkuu, kwa lengo la kushinikiza mabadiliko ya baraza la mawaziri kumechafuka vibaya ndani ya CCM.

  Pamoja na ajenda ya kujadili na kuridhia mabadiliko ya baraza la mawaziri, CCM imeonja joto la jiwe kwa wimbi kubwa ambalo limetikisa si umoja wa vijana tu, ila hata vikongwe ambao walikuwa damudamu na CCM kuanza kuikimbia Jembe na nyumba na kujiunga na Chadema.

  Ajenda kuu ya Kamati Kuu ya CCM ilikuwa kujadili hali ya kukimbiwa na wanachama ambayo imekuwa ni ajenda ya siri, na hii ya kuridhia hoja ya wabunge kushinikiza mabadiliko ya baraza la mawasili ni kuridhia kwa ajili ya kujinasua na mtego wa kukimbiwa na wanachama wake.
   
 2. Mkirua

  Mkirua JF-Expert Member

  #2
  Apr 28, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 5,667
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Ni upepo tu....utapita.... acha nende mazishini nikirudi mambo yatakuwa yametulia.....weweeeee...unachezea pipoz power??... Na bado ngoja arudishe vibonde wake kwa ajili ya uswahiba aone kama bunge la budgeti hakijawaka...Mwalimu aliasa jamani Ikulu chungu..
   
 3. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #3
  Apr 28, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Umenivunja mbavu zangu. Siasa si mchezo wa kuigiza, yataka moyo.

  Angalia vizuri picha hiyo unaweza kusoma kitu kwenye nyuso za wajumbe wa kamati kuu. People's powe si lele mama.
   
 4. kilght

  kilght JF-Expert Member

  #4
  Apr 28, 2012
  Joined: Feb 11, 2012
  Messages: 626
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  wala mshangaike na vyama vya msimu watanzania vinapita hivi maneno ya jk leo yanamtokea puani
   
 5. r

  rogersic New Member

  #5
  Apr 28, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hawa tunawalea vibay, ikulu sio sehemu ya kufanyia shughuri za chama, hii inaonesha wasivyokuwa serious
   
 6. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #6
  Apr 28, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  mdharau mwiba mguu huota tende.
   
 7. N

  Njele JF-Expert Member

  #7
  Apr 28, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 275
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Watu wamelalamika, naona wao wanaendelea kuongeza pamba masikioni mwao
   
 8. LEGE

  LEGE JF-Expert Member

  #8
  Apr 28, 2012
  Joined: Oct 14, 2011
  Messages: 4,914
  Likes Received: 5,351
  Trophy Points: 280
  Chadema inabidi iwe macho sana na hawa hama hama wa ccm wanao toka ccm na kuingia chadema mim nahisi hawana nia njema kabisa.

  Kiukweli hawa hama hama wanakuja kukiharibu chadema.

  Kwanza inaonyesha wazi wanahamia chadema kwaajiri ya kutaka kugombea uongozi 2015.
  Na hawa wakipewa uongozi ndani ya chadema wataleta madudu yao na uchafu wan walio toka nao ccm.
   
 9. Kinyungu

  Kinyungu JF-Expert Member

  #9
  Apr 28, 2012
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 4,381
  Likes Received: 3,341
  Trophy Points: 280
  Hivi kikao kama hiki huwa kinaisha bila kutaja CHADEMA kweli?
   
 10. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #10
  Apr 28, 2012
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  hapa simuoni katibu wa itikadi na uenezi wa chama au yupo bechi la mwisho
   
 11. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #11
  Apr 28, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  Hamna ki2 hapo
   
 12. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #12
  Apr 28, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Ni upepo unaovuma kwa muda, utatulia wenyewe
   
 13. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #13
  Apr 28, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  wa nne kutoka kwa Pinda
   
Loading...