DiasporaUSA
JF-Expert Member
- Aug 27, 2016
- 23,381
- 29,627
Nn
Mbowe alipe kodi yetu ya Hai. Arejeshe mkopo wa Twiga bank, deni nhc, nkSHILINGI INAPOTAFUTA MILANGO YA KWENDA KUZIMU KWA KASI
Thamani ya shilingi ya Tanzania inazidi kuporomoka kwa kasi kulinganisha na dola ya Marekani.Dola 100 ya Marekani imenunuliwa kwa shilingi 224,500 wakati wiki mbili zilizopita dola hio hio ilinunuliwa kwa shilingi 217,000 ongezeko la asilimia 3.45. Kushuka kwa thamani ya shilingi(Depreciation) kuna madhhara makubwa matatu:
Kwanza, swali linakuja Je nchi inaagiza malighafi nyingi kutoka nje? Kama inaagiza hizo malighafi kwa ajili ya viwanda basi thamani ya sarafu yetu ikishuka na gharama za uzalishaji wa bidhaa ya mwisho itaongezeka.Obvious hata nchi lazima iondoke kwenye ushindani wa soko la dunia. Kwa mfano kama kiwanda cha kuzalisha sukari cha mtibwa kinategemea malighafi nyingi kutoka nje basi hata gharama za uzalishaji zitaongezeka kwa kasi ile ambayo sarafu ya shilingi inashuka. Mfano:Kama Tani moja ya miwa ilinunuliwa kwa $100 ambayo ni sawa na 217,000 kwa wiki mbili zilizopita na leo tani ile ile itanunuliwa kwa $100 sawa na shilingi la 224,500 ongezeko la shilingi 7500 au $3.34 kwa tani ile ile.
Pili, kinachoangaliwa ni je nchi imekopa sana fedha za kigeni au sarafu ya shilingi? Hii ina maana kama Tanzania imekopa deni lake lote kwa dola au hata paundi basi hata deni la taifa ukilikokotoa kwa shilingi kulingana na thamani yya shilingi inavyoshuka thamani. Kwa mfano kama shilingi imeporomoka thamani kwa asilimia 30 basi hata deni la taifa litaongezeka kwa asilimia hizo hizo 30,Hivyo kupelekea watu wengi kuendelea kuogelea kwa dimbwi kubwa la madeni ambayo yamesababishwa na sarafu kushuka thamani(Currency depreciation) Na pia uwezekano upo kwa makampuni mengi kuathiriwa na mtikisiko katika uendeshaji wao.
Tatu, Tunaangalia ni kwa namna gani sarafu kuporomoka thamani inapelekea mfumuko wa bei za bidhaa na huduma (Inflation). Kihistoria inaonyesha mataifa mengi yanayoagiza bidhaa nyingi kutoka nje kama chakula na nishati ya mafuta, Sarafu ya ndani ya nchi husika ikiporomoka basi hata mfumuko wa bei unakua mkubwa kuliko ilivyokua mwanzo. Hii ina maana hata bei ya hizi bidhaa ikiongezeka watu hawawezi kusitisha kununua bidhaa hizi kwa sababu ni muhimu kwa jamii. Hivyo basi Inflation(Mfumuko wa bei za bidhaa) hua unapelekea mtikisiko kwenye mzunguko wa fedha( Financial instability). Hapa mashirika ya kifedha hasa hasa benki za biashara yataathirika moja kwa moja,Watu wataathirika moja kwa moja, Shughuli za kiuchumi zitaathirika pia. Jitihada za dhati zinatakiwa kuwekezwa na benki kuu ili kuweza kuinusuru shilingi yetu isiendelee kupotea yasije yakatukuta kama yaliowakuta Wazimbabwe.
Acha theory za kufikirika ndugu, Tanzania tuna export nini cha maana kusema etu tufurahie dola kupanda? Kupanda kwa dola kuna madhara makubwa kwa watu wa chini kuliko faida ukizingatia hili tishio la njaa na dola inapanda ina maana itakuwa expensive kuagiza chakula kama ikihitajika.Analysis yako ingekamilika tu kama ungetuambia pia Impact ya currency depreciation kwenye ku-stimulate exports ambazo zinaweza ku offset madeni na hivyo kuleta maendeleo katika nadharia yake.
Athari za kushuka kwa thamani ya sarafu katika uchumi haziwezi kuelezewa kwa urahisi kama ulivyojaribu. Lazima, ili ueleweke na wachumi itabidi utupe ufafanuzi wa pande chanya (export gains from depreciation) na upande hasi (costs/losses due reduced purchasing power for imports), kisha uweke kwenye mizani faida na hasara hizo uone ni upande upi ni mzito. Ukiongelea upande moja Tu analysis yako inakuwa nyepesi na incomplete, watu watadhani niya kisiasa zaidi.
Acha theory za kufikirika ndugu, Tanzania tuna export nini cha maana kusema etu tufurahie dola kupanda? Kupanda kwa dola kuna madhara makubwa kwa watu wa chini kuliko faida ukizingatia hili tishio la njaa na dola inapanda ina maana itakuwa expensive kuagiza chakula kama ikihitajika.
So acha kabisa kusifia hii kitu
[HASHTAG]#Busara[/HASHTAG] za Naantombe 2017
Acha theory za kufikirika ndugu, Tanzania tuna export nini cha maana kusema etu tufurahie dola kupanda? Kupanda kwa dola kuna madhara makubwa kwa watu wa chini kuliko faida ukizingatia hili tishio la njaa na dola inapanda ina maana itakuwa expensive kuagiza chakula kama ikihitajika.
So acha kabisa kusifia hii kitu
[HASHTAG]#Busara[/HASHTAG] za Naantombe 2017
Sasa nikuelewe mara ngapi mkuu? Point yako kubwa ni kwamba kukitokea Currency devaluation itavutia exportation zaid na kudiscourage imports ambayo itasababisha account za kibiashara za Tanzania ziimarike......... au nieleweshe zaidi kama labda nimeelewa vingineLabda ungeelewa kwanza point yangu ndipo uchangie. Kama hujaelewa uliza, sijafurahia kupanda wala kushuka kwa thamani ya sarafu, na mleta mada hajanishawishi nifurahie wala kuchukia kushuka kwa thamani. Jitahidi kwanza kuelewa kinachosemwa ndipo uchangie.
Hivi ni kweli usemavyo kuwa Tanzania hatuuzi kitu chochote cha maana? Kwa hiyo hizo dola tunazipataje?
sasa kama mpaka sasa tuna negative balance of trade utajisifu vipi kwamba unauza vitu nje? halafu unaanza kufurahia depreciation of currency?Hivi ni kweli usemavyo kuwa Tanzania hatuuzi kitu chochote cha maana? Kwa hiyo hizo dola tunazipataje?
Sasa nikuelewe mara ngapi mkuu? Point yako kubwa ni kwamba kukitokea Currency devaluation itavutia exportation zaid na kudiscourage imports ambayo itasababisha account za kibiashara za Tanzania ziimarike......... au nieleweshe zaidi kama labda nimeelewa vingine
Bado una feli sana.. mimi nimekubali na ninaelewa theory behind depreciation kwenye imports na export.. ila nimeenda upande wa uhalisia kwamba, tanzania tuna export kitu gani cha maana? Usichukue tu theory ukai fit kila maali penda kuangalia na uhalisia wa mambo.. sio tu ukisikia depreciation basi unadhani lazima iwe na impact kwenye export na importBado unashindwa kunielewa. Narudia. Depreciation inasababisha mambo mawili kwa wakati moja, jambo la kwanza ina stimulate export kwa kuzifanya bidhaa zetu nje zinunulike kwa wingi maana zimepungua bei. Lakini jambo la pili linafanya imports zetu ziwe za bei mbaya na hivyo tukashindwa kumudu mahitaji. Sasa ukitaka kujuwa kama depreciation ina faida au hasara lazima uweke mambo haya mawili kwenye mizani ili uone upande gani unazidi mwingine. Sijasema upande wa faida (exports) unazidi upande wa hasara (imports). Mleta uzi ametupa upande moja tu, na ndio nikasema elezea na upande wapili kisha weka mizani ndipo ueleweke vizuri. Hiyo ndio point yangu.
sasa kama mpaka sasa tuna negative balance of trade utajisifu vipi kwamba unauza vitu nje? halafu unaanza kufurahia depreciation of currency?
Ndugu, unajua huu uchumi nacheza nao kila siku na uhalisia wa haya mambo nayaelewa vema.. wew sasa naona umeamua tu kuwa mbishi halafu unaanza kuandika na hoja nyingine ambazo ziko questionable kama nilivozi bold. Sasa mfano hili suala la mshahara wa baba limeingia vipi hapo???? Kama sio tu umeamua kuwa mbishi? ... currency depreciation na mshahara wa baba.. reallllllyyyyy aisee kwaheri sikujibu tena, we ni mbishi mno mkuuNegative terms of trade ni kawaida sana kwa nchi za ulimwengu huu. Na ndio maana international monetary funds iliundwa. Na kama ilivyo kwa depreciation positve balance of payments nayo ina madhara yake kwa uchache wake. Hivyo wala isikufanye kwamba Tz hatuna exports za maana, kumbuka upande moja wa balance sheet ya terms of trade kuna imports ambazo ni function ya mahitaji ya kila namna ya nchi. Ni sawa tu pale mshahara wa baba usipokidhi mahitaji ya familia, huwezi kusema hafanyi kazi ya maana. Ni kwasababu there is limited resources trying to serve unlimited needs.
Bado una feli sana.. mimi nimekubali na ninaelewa theory behind depreciation kwenye imports na export.. ila nimeenda upande wa uhalisia kwamba, tanzania tuna export kitu gani cha maana? Usichukue tu theory ukai fit kila maali penda kuangalia na uhalisia wa mambo.. sio tu ukisikia depreciation basi unadhani lazima iwe na impact kwenye export na import
Ndugu, unajua huu uchumi nacheza nao kila siku na uhalisia wa haya mambo nayaelewa vema.. wew sasa naona umeamua tu kuwa mbishi halafu unaanza kuandika na hoja nyingine ambazo ziko questionable kama nilivozi bold. Sasa mfano hili suala la mshahara wa baba limeingia vipi hapo???? Kama sio tu umeamua kuwa mbishi? ... currency depreciation na mshahara wa baba.. reallllllyyyyy aisee kwaheri sikujibu tena, we ni mbishi mno mkuu