Tishio la pesa za digitali: Je, Serikali zitabaki na Bunduki tu?

LuteganoC

New Member
Dec 1, 2019
0
19
Wazee tunaikumbuka hii? Ilianza kama utani, c lakini sio utani kwa akili ya mwanzilishi mwenyewe wa pesa za digitali. Lengo la Satoshi Nakamoto mwanzilishi wa pesa ya digitali ya bitcoin ni kuleta dunia yenye pesa ambayo haiko chini ya chombo chochote au serikali duniani. Kusudi lingine ni kuondoa kabisa madalali (middle men) kwa maana ya pesa izunguke miungoni mwa watu bila uhitaji wa mabenki. Pesa itoke kwa Musa kwenda kwa Baraka moja kwa moja bila kuguswa na mtu yeyote katikati, kwa maana kwamba hakuna haja ya benki, au huduma za kutuma pesa za simu au Western Union. Satoshi Nakamoto mvumbuzi wa pesa hizi za digitali bado ni hadithi tu, mpaka leo hajulikani wala kutambulika.

Utendaji wa pesa hizi za digitali kwa mfano rahisi fikiria vile unamtumia mtu pesa kwa njia ya simu, lakini badala ya hiyo pesa kupitia kwa mitambo ya mtandao husika mfano Vodacom kwa ajili ya kuidhinishwa, au muamala kuthibitishwa, pesa hiyo inaenda moja kwa moja na kumfikia mpokeaji na haipotei. Sasa ni miaka 10 baadaye toka izaliwe bitcoin tayari tishio la pesa hizi za digitali kwa serikali za mataifa duniani limeanza kudhihirika na hatimaye linaenda kutimia kusudi la mwasisi kwa kile kinachoitwa freedom of money (uhuru wa kifedha).

Imekuwa kama utani lakini haikuwa utani kwa mwasisi, ambaye bila shaka aliona mbali vile teknolojia yake italeta shida kwa mataifa ndio maana hajulikani mpaka leo, isipokuwa andiko lake na matokeo ya kazi yake ndio huzidi kusambaa kwa kasi duniani. Sifa kuu tano ya pesa hii ni; uwazi, kutokuwa na mipaka, kuwa mikononi mwa watu, haina mdhibiti na haiegamii mamlaka yoyote. Kwa sifa hizi haistajabishi kwamba ilijipatia wafuasi haraka sana.

Japo ilizaliwa kwa nia njema lakini mpaka kufikisha umri wa miaka 10 pesa hii imepitia mtikisiko mkubwa sana. Sehemu kubwa ya mtikisiko ni kuchafuka kwa jina. Watu wengi walipoiona inatija sio tu walijikusanyia akiba bali ni wimbi la biashara halamu zilizofanyika kwa malipo ya bitcoin. Biashara kubwa ambayo ikaja kufumuliwa na FBI ya Marekani iliitwa Silk Road. Katika biashara hiyo kulikuwa kuna kuuziana kila aina ya bidhaa halamu ikiwemo madawa ya kulevya, silaha na kuwalipa magaidi wa kujitoa muhanga. Sehemu ya pili ya hisotria chafu ya bitcoin ni biashara za utapeli (scams). Baada ya watu wengi kuona faida ya muda mfupi kwa kununua na kuuza bitcoin basi wengine wakawa tayari kama mamba aliyejiandaa kunasa windo. Tovuti na mitandao mbalimbali ikaazinshwa ikidai kuuza bitcoin kwa bei nzuri, au kuahidi watu kupanda mbegu kwa kiasi kidogo cha pesa na kupewa faida kubwa baada ya kuwekeza kwenye bitcoin. Matokeo yake ikaishia kilio kwa watu wengi kupoteza pesa zao.

Sehemu ya tatu ni kubadilika kwa thamani ya bitcoin. Sifa kubwa ya bitcoin kuendana na dola ni kupanda haraka na baadaye kushuka. Idadi kubwa ya watu ambao kwa kukosa ufahamu waliingia kichwa kichwa, wakanunua wakati bei iko juu kwa tarajio kwamba itaendelea kupanda. Ghafla wakajikuta bei ya bitcoin katika dola imeshuka toka dola $ 20,000/= ya Disemba 2017 mpaka $3,100/= ya Disemba 2018 na kulazimika kuuza kwa hasara. Waliyotapeliwa na waliyouza kwa hasara wote hawana uhusiano mzuri na bitcoin. Japo ukweli ni kwamba toka historia ya nyuma bitcoin ikishuka haijawahi kamwe kurudia kiwango chake cha chini kilichowahi fikiwa kabla (lowest low). Maana yake ni kwamba bitcoin safari yake ni thamani kupanda hadi kulinganishwa na dhahabu na kupewa jina la dhahabu ya digitali (digital gold).

Sasa baada ya kuangalia historia iliyoitia doa bitcoin tujadili kwa nini bitcoin ni tishio. Ujio wa bitcoin unatisha watu matajiri waliyoneemeka na mfumo wa pesa za makaratasi, mabenki, serikali na karibu nchi nyingi duniani. Sifa hizi ni uhuru wa kutosimamiwa au kudhibitiwa na chombo chochote, sifa ya kupanda thamani, sifa ya kuleta faida kuyazidi masoko ya hisa, sifa ya kutumika mahali popote bila mipaka na urahisi wa kutuma na kufika kwa mtu yeyote duniani ndani ya muda mfupi sana, na zaidi ni teknolojia yake yenye uwezo wa kutunza miamala toka ilivyoanza, na usalama wa kutoweza ingiliwa kabisa. Vyote hivi vimefanya bitcoin na teknolojia yake ya blockchain kuwa kimbilio la utafiti, uwekezaji na malipo.

Awali makampuni makubwa na wana uchumi maarufu kama Nouriel Roubin (maarufu kwa kutabiri mtikisiko wa uchumi wa mwaka 2008), waliibeza kwamba haina thamani na haifiki popote. Lakini sasa wameanza kusalimu amri, akiwemo mtendaji mkuu wa benki kubwa Marekani ya J.P Mogan, wengine ni kampuni ya Facebook na mradi wake kwa ushirika wa makampuni mengine 27 yakiwemo Visa, PayPal, MasterCard, ebay, Vodafone na Uber. Mradi huo wa pesa ya digitali ya Facebook na washirika hao huitwa Libra. Una lengo la kutumika katika mitandao ya Facebook na Whatsapp kama chombo cha malipo na kutumiana pesa.

Hivyo basi nguvu iliyokuja nayo pesa hii ya Facebook imekoleza mara dufu tishio la bitcoin ambapo mabenki duniani, benki kuu na serikali za nchi zimejitokeza waziwazi kuelezea hofu ya mradi huo wa facebook. Ya kwanza ni Marekani yenyewe ambapo kamati maalumu ya pesa ya bunge la Marekani imetoa sitisho kwa Facebook kuendelea na mradi huo mpaka ambapo tathimini ya mradi huo itakuwa imekamilika. Kwingineko Ufaransa agizo limetolewa kwa benki kuu kupima na kuchunguza mradi huo wa facebook na athari zake kwa hofu kwamba Facebook yenye watu karibu bilioni 2.3 wanaotumia mitandao yake duniani kote mbali na kwamba imeshutumiwa kwa kuvujisha taarifa za watumiaji wake lakini ni tishio kwa mstakabali wa mabenki pale ambapo idadi hiyo ya watu wanaotumia Facebook wanaweza anza kutumia pesa hiyo ya digitali Libra.

Mvutano huu umeibua watu wengi katika mitandao ya kijamii kwamba sio tu utasaidia kufumua fumua mifumo ya utajiri na pesa iliyopo duniani bali pia utasaidia kuitanganza zaidi bitcoin ambayo haina mwenye nayo na ndio itaibuka mshindi. Wengine wakienda mbali kwamba serikali zitashindwa kwa sababu ya nguvu ya watu waliyo nyuma ya mradi wa Facebook. Na pia kwamba ili kukwamisha mpango huo labda uzimwe kabisa mtandao wa intaneti duniani kote. Kitu ambacho sio rahisi, na hata ikiwezekana bado kutakuwa na mtandao tu kupitia satelaiti ya StarLink iliyorushwa na mkurugenzi mkuu wa kampuni ya kutengeneza magari yasio na dereva Tesla bwana Elon Musk. Starlink inakusudia kuleta mfumo wa intaneti yenye kasi zaidi duniani.

Maoni mengine yamehusu ipi itabaki kuwa nguzo na nguvu za serikali duniani. Na majibu yakibaki kuwa huenda serikali zitabaki na nguvu ya bunduki tu. Kwa sababu tishio la pesa za digitali ni kuondoa moja ya nguvu kubwa za serikali duniani ambayo ni kuhodhi mfumo wa pesa. Wengine wakitabiri mbali zaidi kwamba nguvu ya bunduki nayo itaja kuondoka baada ya ujio wa maroboti ya kivita yanayotumia teknolojia ya artificial inteligency (AI).
 
Mi kila nikitafakari hii biticoin naishia kuumia kichwa kwa maswali yafuatayo:

1. Wanasema inakuja kuua sekta za mabenki wakati huo huo ili uweze kuuza na kununua Bitcoin lazima uwekeze pesa ambayo ni hizi hizi hela za kawaida na lazima utumia account ya benki! Sasa hapo benki zinakufaje?

2. Pili ili utumie pesa uliyoivuna kwa kuuza biticoin lazima uilete kwenye pesa ya kawaida kupitia benki! Au unataka kusema kwamba itafikia mahali tutafanya malipo kwa biticoin badala ya malipo ya hizi hela za kawaida!

3. Halafu naomba kueleweshwa, hivi unaweza kumiliki biticoin kama hauna account ya benk? Unaweza kumiliki biticoin kama hauna hela benk?

Naomba ufafanuzi wa hayo
 
hayo mapesa siyataki kabisa na haytaendelea asilani
kwani kila mwaka watu wanapigwa na hawasikii
tumeshapigwa na ONTARIO, D9
hatusikii nimeamua kuchimbia kweye kibubu basi
 
Mi kila nikitafakari hii biticoin naishia kuumia kichwa kwa maswali yafuatayo:

1. Wanasema inakuja kuua sekta za mabenki wakati huo huo ili uweze kuuza na kununua Bitcoin lazima uwekeze pesa ambayo ni hizi hizi hela za kawaida na lazima utumia account ya benki! Sasa hapo benki zinakufaje?

2. Pili ili utumie pesa uliyoivuna kwa kuuza biticoin lazima uilete kwenye pesa ya kawaida kupitia benki! Au unataka kusema kwamba itafikia mahali tutafanya malipo kwa biticoin badala ya malipo ya hizi hela za kawaida!

3. Halafu naomba kueleweshwa, hivi unaweza kumiliki biticoin kama hauna account ya benk? Unaweza kumiliki biticoin kama hauna hela benk?

Naomba ufafanuzi wa hayo
Unaweza kumiliki Bitcoin bila kuwa na Account Bank wala pesa Bank!
 
kuna baadhi ya sehemu kwa sasa wanapokea malipo kwa njia ya bitcoin
 
Pesa za digitali ni mpango wa muda mrefu wa kuipeleka dunia kusimamiwa na dola moja (New World order) huku third world countries tunapokea tu na kutumia hii kitu ilikuwa ngumu kuzitawala nchi zote ikiwa zinajitegemea na kutengeneza fedha zao ndio mchakato wa mlungula ukaamza kufanyika tunahamishwa kidogo kidogo bila kujijua na tunapokea na kuyaita maendeleo na mabadiliko.

Zamani tulibadilishana vitu (batter trade) tukaletewa fedha,tukawa tunazitunza kwenye magunia na chini ya mito,tukaletewa benki ambapo badala ya kuzitunzia kwenye magunia peleka huko na wao wanakupa kadi tu inayokuwezesha kuzimiliki fedha zako lakini ishu ikawa bado fedha inashikika,tukaenda hatua nyingine ya mobile money haushiki pesa ila unafanya mahitaji ambapo mwisho wa siku hela inapotea kwenye mikono ya watu ila inabaki thamani yake tu..taratibu ndio imekuja na pesa za digitali hii inatusogeza zaidi kwenye kupoteza kabisa matumizi ya benki sababu benki zinatunza fedha halisi hivyo badala ya kutumia benki fedha zitakuwa zinabadilishwa kuwa za digitali na mauzo yake yatakuwa yanakubalika kwenye huduma zote,tukiwa tunaendelea sasa hivi kila kitu kinaunganishwa na alama za vidole hii ikiwa ni kwamba mbeleni huko hata benki,mobile money zote zitakuwa linked na wewe kupitia alama yako ya kidole hapo hutahitaji tena kadi ya benki ila alama yako ya kidole kufanya manunuzi kila sehemu mwisho tutapewa namba yako kama mwananchi itatunza kila kitu chako humo so hutahitaji tena kuwaza kukumbuka au kubeba id kila kitu kitakuwa kwenye namba yako na password yako ni alama ya kidole.

baada ya pesa halisi kupotea kabisa hapo ndio mmiliki wa hizi system atakapo amrisha dunia kwa nguvu 1 na dunia itatii sababu nchi itakuwa haina fedha halisi ila thamani tu,hivyo akifunga thamani yako unapata balaa....

So huu ni mchakato tunaouita kukua kwa teknolojia unaotupeleka kwenye mtego taratibu hauna haraka na unaenda hatua kwa hatua benki zitapata shida sababu fedha itakuwa ikienda hairudi inakuwa imebadilishwa kuwa ya digitali hivyo zinafeli sababu hakuna tena fedha halisi tofauti na hapo na zenyewe zijiunge na fedha za kidigitali.

Hivyo hii alert ya benki kuu ni kujaribu kuziokoa fedha halisi zisipotee ila ni ngumu kwa jinsi mtandao na teknolojia vinavyotupeleka kasi hasa huku tunapopokea zaidi bila kutengeneza.
 
Umeanza mambo ya kisabato..kila kitu kizuri Ni Freemason
 
Mi kila nikitafakari hii biticoin naishia kuumia kichwa kwa maswali yafuatayo:

1. Wanasema inakuja kuua sekta za mabenki wakati huo huo ili uweze kuuza na kununua Bitcoin lazima uwekeze pesa ambayo ni hizi hizi hela za kawaida na lazima utumia account ya benki! Sasa hapo benki zinakufaje?

2. Pili ili utumie pesa uliyoivuna kwa kuuza biticoin lazima uilete kwenye pesa ya kawaida kupitia benki! Au unataka kusema kwamba itafikia mahali tutafanya malipo kwa biticoin badala ya malipo ya hizi hela za kawaida!

3. Halafu naomba kueleweshwa, hivi unaweza kumiliki biticoin kama hauna account ya benk? Unaweza kumiliki biticoin kama hauna hela benk?

Naomba ufafanuzi wa hayo
Hiyo noamba 3 nadhani ndo tunakoelekea maana hiyo ni online money na kuna makampuni yatakuja malipo unafanyia online !! Watachofanya ni kuimarisha mifumo yao tuu
 
Back
Top Bottom