Tina
JF-Expert Member
- Jul 9, 2007
- 572
- 579
Hali si shwari ndani ya Baraza Kuu la Waislamu (BAKWATA) na sasa kundi la viongozi ndani ya baraza hilo wanakula njama za kumuondoa kiongozi wao makini Mufti Zubeir.
Hali hiyo inakuja huku zaidi ya miezi miwili Bakwata haina ofisi na zaidi ya wafanyakazi 50 wa Bakwata Makao Makuu hawajalipwa mishahara yao kwa zaidi miezi kumi na moja(11).
Kadhalika zaidi ya walimu kumi na tano wa shule ya Bondeni Arusha hajalipwa mishahara yao, na huku Baraza lote la Masheikh la mkoa wa Katavi na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bakwata Mkoa wa Katavi kujiuzulu kutokana na kutokuwa na IMANI na mufti zuberi.
Tayari zipo taarifa sasa za kuandaliwa mpango wa kuondolewa madarakani mufti kutokana kile kinachodaiwa kwamba ni kushindwa kuongoza Bakwata na ubadhirifu mkubwa wa mali za Bakwata uliofanywa na mufti na ndugu zake wa karibu.
Wajumbe kadhaa wa Baraza la masheikh Taifa wanajiandaa kutumia katiba ya Bakwata kumuengua mufti katika nafasi yake ya umufti kabla ya mwisho wa mwaka huu.
Wakati wajumbe wengine kumi wa halmashauri kuu ya Bakwata Taifa wakijiandaa kuwasilisha hoja ya kutokuwa na Imani na mufti katika kikao kijacho ili kutoa nafasi ya mufti kujiuzulu kabla hawajatoa taarifa za siri za ubadhilifu mkuu wanaoujua wajumbe hao dhidi ya mufti.
Wakati huo huo viongozi wa Bakwata toka mikoa mitano, wanajiandalia kujiuzulu kutokana na kuchoshwa kwao na vitendo vya mufti Zuberi. Vitendo hivyo ikiwa ni pamoja na mufti Zuberi kuingiza Bakwata kwa miaka miwili sasa bila muelekeo wowote, huku vitendo vya ubadhirifu, ubinafsishaji wa mali za bakwata na ubabaishaji kushika kasi na ndugu wa mufti kupewa kipaumbele bila kuzingatia katiba ya Bakwata.
Updates:
Masheikh watatu ambao ni wajumbe wa baraza la ulamaa taifa Bakwata,wakishirikiana na sheikh mkuu wa dar es salaam,sheikh mkuu wa tabora,pamoja na kiongozi mwandamizi wa zamani wa Bakwata ndio wanasuka mpango wa kumuondoa mufti wa Tanzania Abubakar Zuberi.
Mpango huo ulioandali kwa umakini mkubwa,huenda ukamfanya mufti Zuberi kuwa ni mufti wa kwanza kuenguliwa katika historia ya bakwata na kupelekea mufti kwa mara ya kwanza kutoka Rufiji.
Mpango ambao ulikuwa utekelezwe wakati Mufti Zuberi akiwa yupo Morocco,ambao kwa sasa utatekelezwa wakati wowote.
Nitaendelea kuwapa update!!!