BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,832
- 287,782
Tishio jipya CCM
na Martin Malera, Dodoma
Tanzania Daima~Sauti ya Watu
KIKAO cha Bunge la Bajeti kiliendelea mjini Dodoma jana huku upepo wa kisiasa ukionekana dhahiri kuendelea kukigawa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika makundi ambayo sasa yanatoa mwelekeo wa kihasama kuliko wa kishindani.
Uchunguzi uliofanywa na Tanzania Daima kwa siku nzima jana na kufuatilia kauli zilizotolewa na baadhi ya wabunge, zinaonyesha kwamba semina ya mwishoni mwa wiki iliyojumuisha wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM na wabunge wanaotokana na chama hicho tawala, imethibitika kuzaliwa na kushamiri upya kwa makundi.
Aidha, semina hiyo kwa upande mwingine, imethibitisha kwamba vidonda vilivyotokana na Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005 ndani ya chama hicho havijapona na bado vinakitafuna chama hicho.
Mmoja wa watu waliohudhuria kikao hicho ameieleza Tanzania Daima kwamba kauli aliyoitoa ndani ya semina hiyo Mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete, akisema kuna watu bado wana ndoto za urais unaweza ukawa ushahidi kwamba makundi yamegeuka kuwa ugonjwa sugu.
Dalili za kuendelea kushamiri kwa makundi hayo zimethibitishwa na kile kinachodaiwa kutokea ndani ya Bunge jana kati ya Mbunge wa Kigoma Mjini, Peter Surukamba (CCM) na Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango.
Taarifa ambazo Tanzania Daima ilizipata kutoka bungeni jana na zikathibitishwa na Serukamba mwenyewe, zinaeleza kuwa Kilango alimfuata Serukamba katika kiti alichokaa na akamuonya kuhusu matamshi aliyoyatoa wakati wa semina ya mwishoni mwa wiki kabla ya kumtaka ajiandae kwa kisasi.
Ni kweli leo asubuhi Mama Kilango kanifuata katika kiti changu na kunitisha kutokana na kile nilichosema ndani ya semina jana na akasema eti alikuwa akikusudia kulipiza kisasi, sijui ni kisasi cha namna gani amepanga kulipiza, alisema Serukamba.
Kwa mujibu wa Serukamba, mbunge huyo mwenzake wa CCM alitoa matamshi hayo wakati wabunge wengine wawili, Ritha Mlaki (CCM-Kawe) na Nazir Karamagi (CCM-Karagwe) wakisikia.
Alipoulizwa ni kitu gani hasa alikuwa amekisema wakati wa semina hiyo ya CCM, Serukamba alisema anaamini pengine ni kauli aliyoitoa kwa makada wenzake wa chama hicho kuacha kuwatuhumu watu katika kashfa pasipo kuwa na uhakika wa kutosha kuhusu kile wanachotuhumu.
Serukamba alikiri kutoa mfano wa matamshi yaliyopata kusemwa ndani ya Bunge na Kilango wakati wa mjadala wa ufisadi kuwa mfano wa tuhuma ambazo zilitolewa pasipo kuwapo kwa ushahidi.
Alipoulizwa ni hatua gani alikuwa akikusudia kuchukua kutokana na kauli hizo, Serukamba alisema alikuwa ameshaamua kumtaarifu Spika wa Bunge, Samuel Sitta, kuhusu suala hilo, pia alikuwa akitarajia kulifikisha mbele ya vikao vya CCM.
Hata hivyo, mwandishi wa Tanzania Daima aliyepo bungeni Dodoma alipomtafuta Kilango bungeni jana mchana na kumkosa, na baadaye kuwasiliana naye kwa simu, mbunge huyo aliahidi kulizungumzia suala hili jioni ya jana, atakapokuwa amerejea bungeni. Hata hivyo hakuweza kuonana naye jana.
Kwa upande wake, Mlaki ambaye ilielezwa na Serukamba kuwa alikuwa karibu kabisa wakati Kilango akitoa matamshi hayo, hakuwa tayari kusema lolote alipofuatwa na mwandishi na kuulizwa iwapo alikuwa amesikia lolote.
Suala hili linatokea wakati huu, wakati ikieleweka bayana kwamba, Kilango amekuwa mstari wa mbele na waziwazi akipambana na ufisadi ndani ya CCM na serikali, wakati Serukamba amekuwa mmoja wa watu ambao siku zote wamekuwa wakipinga kuhusu ufisadi kugeuzwa ajenda ya kisiasa.
Ndani na nje ya vikao rasmi, Serukamba amekaririwa mara kadhaa akieleza kukerwa na namna wabunge wenzake wa chama hicho tawala, akiwamo Kilango, wanavyoufanya ufisadi kuwa ni ajenda ya kumalizana wenyewe kwa wenyewe CCM.
Mbali ya hilo, katika hatua nyingine, taarifa za kuwapo kwa mbunge mmoja wa CCM aliyedaiwa kutupa vitu vya kishirikina ndani ya Bunge mwishoni mwa wiki iliyopita, ziliendelea kuzua mjadala hata baada ya chama hicho tawala kutoa taarifa ya ufafanuzi juzi.
Habari za uhakika kutoka miongoni mwa makada wa chama hicho tawala zinaeleza kuwa, suala hili nalo sasa linaonekana kuchukua mkondo ule ule wa ugomvi wa kimakundi, ambao unakitafuna chama hicho tawala.
Katika hatua ya kushangaza, ofisa mmoja wa juu wa Ikulu jana aliwasiliana na Tanzania Daima na akaitaka kulichukulia kwa uangalifu mkubwa suala hilo ambalo alidai limekuzwa kwa sababu na malengo ya kisiasa.
Mbali ya hilo, ofisa huyo wa Ikulu ambaye hakutaka kuandikwa gazetini, alisema mtuhumiwa mkuu katika sakata hilo ambaye bado jina lake halijatajwa rasmi, alikuwa ameshajiandaa kueleza ukweli kuhusu tuhuma hizo nzito zinazoelekezwa kwake, ambazo iwapo zitathibitika, basi anaweza kutiwa hatiani kwa kosa la jinai chini ya Sheria dhidi ya uchawi ya mwaka 1971, iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Wakati hilo likitokea, jana hiyo hiyo Spika wa Bunge, Samuel Sitta, alilazimika kutoa ufafanuzi zaidi kuhusu taarifa hizo za watu wanaodaiwa kuingia ndani ya ukumbi wa Bunge na kufanya mambo yanayodhaniwa kuwa ni ya kishirikina.
Akizungumza bungeni jana, Sitta alisema kuwa mbunge mmoja na ofisa mmoja wa Bunge wanaohisiwa kuweka vitu vya ushirikina ndani ya ukumbi wa Bunge, walifanya tukio hilo majira ya saa 2:10 usiku, wakati wabunge wengine wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) walipokuwa kwenye kikao chao.
Alisema ingawa ofisi yake kwa bahati mbaya ilikuwa ikitoa majibu tofauti, asingeweza kupuuzia taarifa ya kuwapo ushirikina ndani ya Bunge, kwani alihisi wahusika waliweka aina ya sumu ya kisasa.
Sitta alisema mara ya kwanza alizipata taarifa hizo Juni 12, siku ya Alhamisi iliyosomwa hotuba ya bajeti kutoka kwa Kaimu Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashilila.
Naunganisha na tukio hilo, baadaye siku hiyo hiyo, Mbunge wa Lupa, Mheshimiwa Victor Mwambalaswa, aliniandikia kikaratasi kunijulisha kuwa ameondoka kumsaidia Mheshimiwa Dk. Harrison Mwakyembe kumpeleka hospitali baada ya kuugua ghafla bungeni.
Nilihisi inawezekana wahusika walitupa kitu aina ya sumu ya kisasa, nikaona nisipuuzie. Bahati mbaya sana katika majibu, ofisi yangu ilitoa majibu tofauti, alisema Sitta.
Alisema siku ya Jumamosi, maofisa usalama walifanya ukaguzi wa kitaalamu na kubaini kuwa ukumbi wa Bunge uko salama na kuwataka wabunge kuondoa wasiwasi uliokuwapo awali wa kuwapo aina ya vitu vya kishirikina.
Alisema kwa sasa, maofisa wa usalama wamechukua picha za kamera hiyo zilizopigwa kwa saa 72, sawa na siku tatu kabla ya siku ya tukio, na kuziweka kwenye CD, ili kuangalia kwa makini tukio hilo, ambalo juzi liliwafanya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, mbele ya Mwenyekiti wao, Rais Jakaya Kikwete, kutofautiana kimawazo.
Kwa sasa tuchukulie taarifa hiyo kama ni uvumi tu, hadi hapo uchunguzi utakapokamilika, alisema Sitta.