Tishio dhidi ya TLS: Wanasheria Afrika Mashariki wamlima barua Waziri Mwakyembe

Mambo ya kujitakia hayo....

Kwa nini mhimili mmoja wa serikali unataka kumeza mihimili mingine?

Kiujumla bado tunasafari ndefu ....
Katiba imekaa vibaya. Ni lazima hiyo mihimili mingine imezwe tu .

Kwanza yote miwili iko chini ya wizara zilizoko serikalini na hivo ziko chini ya mawaziri husika kwa hali hiyo lazima ziingiliwe ukizingatia ni serikali hizi za ki Africa.

Watu wapate akili wote wapiganie katiba yenye separation of power (ya wananchi na si watawala)
 
Hii law society iliyotoa hilo tamko ni aibu kwa tasnia ya sheria africa masharriki yaani bila aibu wana quote magazeti na vyombo vya habari kuwa ndio source ya wao kufikia kutoa tamko lao!!! SHAME on you.

Mbowe tu aligoma kuitika wito wa Makonda kuwa hawezi kuitika kupitia wito wa kupitia vyombo vya habari.Tundu lisu na wanasheria wa Tanzania wakajifanya kusema sio sahihi kuitika wito kupitia vyombo vya habari sio official!!

Leo hii kichombo kinajiita EAST african law society kinajibu na kuchukulia kilichoandikwa magazetini kama official information na kukitolea tamko. Shame on you.What kind of lawyers are you?

Halafu ni lini wanachama wa EAST AFRICAN LAW SOCIETY WALIKAA na kumtuma huyo Richard Mugisha kutoa hilo tamko? Mtu hawezi ibuka tu nyumbani kwake na kujitolea tamko.East African Law SOCIETY MWONDOENI HUYO MTU anadhalilisha hiyo society
hivi we we unajua unacho ongea mnajitoa ufahamu kutetea usicho kijua kweli vijana Wa ccm
mnakazi kweli kweli
 
Safi sana. Haya majitu ccm ni kuyajibu kwa kutumia sheria tu.....tuna viongozi wasionaakili kabisa wamesoma lkn hawajaelimika
 
0cbfd53299c234a47e06966983c0c65a.jpg

209ab52edc878cd1cf08e21556b72fa0.jpg

d777b2251eed2fb2469289e5a85f7f94.jpg
Inawezekana TLS haijaweza vigezo vinavyokidhi haja ktk kuwapata Viongozi wake.
Kwamba TLS kinapaswa ku-perform its functions without external forces, ni sahihi kabisa.
Lakini itawezekana vipi pasiwepo external forces ilihali kiongozi wake mkuu anaweza kuwa forced eternally...!!??
Kivip....!??
Chukua mfano wa Zitto kabwe na sakata la kumuomba CAG akague matumizi ya Ruzuku Vyamani, hapo Zitto alionyesha Professionalism akaacha ukada. Nini kilitokea
Viongozi wenzie waliona msaliti na wakasema alitakiwa kama anaajenda hiyo awataarifu chama waweke mambo sawa kwanza kama wataweza kisha ndio akatoe hoja yake Bungeni ili kwamba wao waonekane wako safi (na kama angewataarifu bila shaka wangemzuia). Lengo likiwa mapungufu yale yawaangukie vyama vingine. Utakumbuka hiyo ilikuwa ni moja ya hoja iliyotumika kumpikia jungu Zitto mpaka hatimae akatoka CDM
Swali; Tundu Lissu, hawezi kubanwa kama Zitto pale ambapo atasimamia mambo yatakayoiumiza taswira ya Chadema kama alivofanywa Zitto
Au; Ilikuepuka kuwekwa kitimoto na viongozi wenzie huoni kama TL ataepuka na kuzuia maamuzi yoyote yakaoiathiri CDM, yasimkute yalomkuta Zitto..?
Huo ndio mgongano wa kimaslahi utakaozuia TLS kuperform it's functions without external interference. Au wanataka kutuambia kwamba kwa vile Waziri wa sheria ni mwanasheri au mwanasheria Mkuu wa serikali (AG) au Jaji Mkuu au itokee Rais au Waziri Mkuu ni mwanasheria kwa taaluma na ni mwanachama wa TLS basi wanaweza kuwa viongozi wa TLS na bado TLS ikawa huru na ikaweza kuperform it's functions without external interference (external interests) !?
Kama suluhisho basi TLS walipaswa kuweka Vigezo na Msharti kama sifa ya kuwata viongozi wake.
Kwa kuwa inaonekana kwambTLS wameshindwa kujijengea mazingira ya neutrality hata Mimi siamini kwamba watafanya kazi zao bila shinikizo, Raisi yuko sahihi kusema hatopokea mapendekezo majina ya wanasheria wanaostahili kuwa Majaji kwani kuna uwezekano wakapendekezwa watu wenye mlengo wa Viongozi wao kwa maslahi ya chama chao.
Nina wasiwasi na tafsiri ya wanasheria kuhusu Uhuru wanaopigania, je ni Uhuru usio na mipaka wala masharti!?
Nawasilisha
 
hapo wamemkumbusha mwakyembe juu ya kauli yake ya kuifuta TLS. hana mamlaka ya kuifuta TLS kutokana na mikataba tuliyosign wenyewe. akae sasa atulie afanye mambo mengine.

Tusubiri uchaguzi uishe, atakayechaguliwa ndo huyo huyo maisha yaendelee.
 
Pona yao wamejificha kwenye kichaka cha lugha,vinginevyo wangepigwa kigongo hicho,wasingekaa wamsahau baba jesca lakini kwa hiyo lugha waliyotumia,they are safe!
 
Kwani mwisho wa hiyo barua ni nini? wataenda Mahakamani kumshtaki Mwakyembe?
Hii barua ni baadhi ya nyaraka za ushahidi zitakazotumika kuwapeleka jela nyie mnaovunja sheria za nchi hapo badae.sasa hivi si mna kinga ya madaraka.ila ipo siku mtasimama kizimbani kujibu mashtaka.
 
Back
Top Bottom