Tip: Ujumbe muhimu kutoka kwenye UWABATA (Umoja wa wanaume bahili Tanzania)

Mech engineer

JF-Expert Member
Aug 25, 2017
318
399
Habari za mchana ndugu zangu.

Baada ya chama kukubaliana kuhusu kukaza masharti ya kuhonga, sasa wanawake wamekuja na mbinu moja matata sana. Tafadhari sana usije ukauza mechi kwa hawa wasichana wa siku hizi. Ukikubali tu, basi hiyo ni one mistake. Ukishafanya nae, the next week anaanza story za kwamba hajaziona siku zake. Kwahiyo atakuomba pesa kwa ajili ya termination. Hii nimeishuhudia kwa watu wengi sana. Nitatoa mifano michache.

Kuna Jamaa alimuita msichana gheto akakaa nae kwa siku moja na alimpa pesa kwa ajili ya kununua P2. Msala ulianza baada ya wiki moja binti akadai haoni siku zake, Jamaa akawa anamuuliza imewezekana vipi na wakati alimpa pesa ya kununua p2??

Msichana akadai kwamba alisahau 😀. Jamaa ikabidi aingie mfukoni kutoa pesa ya termination. Cha ajabu ni kwamba baada ya miezi miwili yule msichana akarudi tena kwa jamaa akidai kwamba mimba ilikataa kutoka hivyo anahitaji pesa nyingine ili ajaribu njia tofauti na ya Mwanzo.

(Niliposimuliwa hapa nikajua kuna mtu kapigwa) 😀. Baada ya Jamaa kushauriwa na wakulungwa akaamua amwambie msichana kwamba ailee tu mimba then akijifungua jamaa atalea. Binti baada ya kuona mambo yamekua magumu akaamua alegeze masharti na kusema kwamba anaomba pesa ya kujaza gesi 😀😀😀😀.

Mfano wa pili hauna utofauti sana na huu wa kwanza, Kuna Jamaa nae aliokota manzi kwenye sehemu za starehe, kuingia chumbani jamaa alikaza atumie mpira japo binti alikua hataki. Baada ya mwezi binti anampigia simu jamaa kumuambia kwamba ana mimba yake 😀😀. Jamaa akahamaki kwamba inawezekana vipi mimba kuingia na ilhali walitumia mpira, binti akajibu kwamba mpira ulipasuka 😀😀😀. Jamaa kwasababu notes tayari alikua nazo, ikabidi akaze akamuambia Lea tu mimba nitalea.

Three months later msichana anampigia simu jamaa akimlaani kwamba amemuendea kwa mganga ili mimba yake iharibike 😀😀😀. USHAURI WANGU!! hii sasa inaonekana ni mbinu mpya inayotumiwa na wadada kujipatia pesa siku hizi, kuwa makini tumia ndom na kama ukijisahau hakikisha anameza p2 mbele yako ili kuepuka vizinga.

(Hii ni kwa wanawake tunaowapitia tu, kama una malengo nae huu ujumbe haukuhusu)

Wasalaam!!
 

Shadow7

JF-Expert Member
Sep 28, 2020
8,640
10,765
Sawa Ujumbe wako tumeupokea na tutausambaza kwa wana UWABATA TAIFA

1623069829163.png
 
2 Reactions
Reply
Top Bottom