TinduLissu aibuka kidedea | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TinduLissu aibuka kidedea

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by PrN-kazi, Mar 9, 2011.

 1. PrN-kazi

  PrN-kazi JF-Expert Member

  #1
  Mar 9, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 2,890
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Tindu Lissu aibuka kidedea katika kesi iliyokua inamkabiri juu ya kuwekewa pingamizi ya uhalali wake kuwepo mjengoni kama Mbunge kutokana na ushindi alioupata kwenye uchaguzi wa Oktoba 31, 2010.

  Mwenye habari kamili juu ya hilo atujuze kwa mapana zaidi..
   
 2. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #2
  Mar 9, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  wengine ndio kwanza tunasikia toka kwako, mengi tunangoja kutoka huko huko kwako
   
 3. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #3
  Mar 9, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  acha kukurupuka, fanya utafiti kabla ya kupost chochote humu badala ya kuomba "habari zaidi!" Hakuna uchaguzi uliofanyika Novemba "31," 2010 kwa kuwa tarehe hiyo haipo!
   
 4. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #4
  Mar 9, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  thanx!
   
 5. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #5
  Mar 9, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dodoma, jana ilifutilia mbali kesi iliyokuwa ikimkabili Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu (Chadema) na kusema kuwa kesi hiyo ilifunguliwa kimakosa hivyo haiwezi kuendelea kusikilizwa.

  Jaji Sivangilwa Mwangesi,alisema kuwa kesi hiyo ilikuwa na kasoro nyingi kutokana na vifungu vya kisheria na akasema haiwezi kuendelea kusikilizwa mahakamani hapo.Kesi hiyo ilifunguliwa na wanachama wawili wa CCM, Shaban Itambu na Pascal Hallu ambao wamewafungulia kesi ya kupinga matokeo Mbunge wa Singida Mashariki, Tindu Lissu, msimamizi wa uchaguzi na mwanasheria wa serikali.

  Hata hivyo wakati kesi hiyo ikifutwa jana, Lissu mwenyewe hakuwepo mahakamani baada ya kuelezwa kuwa aliharibikiwa na gari akiwa njiani kuja Dodoma ambapo aliwakilishwa na ndugu yake Samson Mkotya ambaye alisema kuwa mbunge huyo alikuwa Morogoro baada ya juzi kuharibikiwa na gari lake.

  Kufutwa kwa kesi hiyo ni ushindi kwa Tundu Lissu ambaye tangu mwanzo wa kesi hiyo alionekana kujiamini zaidi na kusema kuwa kesi hiyo ingeishia katika hatua za mwanzo bila ya kufika mbali.

  "Mimi nasema kuwa,kesi hii naisimamia mwenyewe na ninatambua kuwa haiwezi kufika mahali popote kwa kuwa imejaa makosa mengi ya kisheria ambayo kimsingi kama Jaji ataamua kufuata haki hakuna kesi hapa," alisema Lissu siku alipowasilisha ombi la kufutwa kwa kesi hiyo.

  Mbunge huyo ambaye kitaaluma ni mwanasheria aliwasilisha kumbukumbu za hukumu za kesi nyingi ambazo zilifunguliwa kwa mtindo huo ambazo alisema kuwa yeye (Lissu) alizisimamia lakini alishindwa.

  Baadhi ya kesi alizonukuu Lissu ni pamoja na kesi ya John Mnyika na Charles Keenja, Joyce Chitende na Zainabu Gama, John Jomba na Christopher Ole-Sendeka ambazo alisema kuwa zote zilifunguliwa kwa mtindo huo lakini zilishindwa kuendelea.

  Jana Jaji Silivangira alisema licha ya Kifungu cha 111 (b) ambacho Lissu alisema kuwa kimekosewa kutokuwa na mapungufu ya moja kwa moja, lakini kwa kutumia sheria hiyo katika kifungu 112 (a),(b) bado ufunguaji wa kesi hiyo ulionekana kuwa na makosa.

  Moja ya vitu ambayo Lissu alitaka viwekwe ni pamoja na wadai hao kulipa gharama za kesi ya uchaguzi ambazo walishindwa kuzilipa,kingine ni pamoja na kufutilia mbali ombi la wadai walilotaka kusamehewa kulipa gharama hizo akidai kuwa kama hawana fedha wasingeweza kuweka mawakili.

  Kwa upande wao Mawakili waliokuwa wakisimamia kesi hiyo kwa upande wa wadai kampuni ya Uwakili la Wasonga walishindwa kuzungumza chochote kwani mara baada ya kumalizika kwa kesi hiyo waliondoka mahakamani hapo.


  Source: Mwananchi
   
 6. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #6
  Mar 9, 2011
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,944
  Likes Received: 2,091
  Trophy Points: 280
  Tetesi na kukurupuka tofauti yake ni nini?
   
 7. m

  mwabaluhi JF-Expert Member

  #7
  Mar 9, 2011
  Joined: Oct 16, 2010
  Messages: 561
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Congrats lissu endeleza kasi yako bungeni sasa
   
 8. W

  We can JF-Expert Member

  #8
  Mar 9, 2011
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 681
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Inamaana hawakuilipa mahakama ada ya kufungulia kesi? Sasa msajiri aliisajiri vipi? Mambo haya.
   
 9. M

  Mabulangati JF-Expert Member

  #9
  Mar 9, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 779
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Ingekuwa ni CCM wameshinda hapo duh kila tusi lingeelekezwa kwao, siasa jamani si mchezo.
   
 10. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #10
  Mar 9, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  tukana na wewe kama imekuuma uone rungu litakavyo kuangukia...
   
 11. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #11
  Mar 9, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  hahaaaaa .....Makamba Yusufu shkamoo babu
   
 12. L

  LAT JF-Expert Member

  #12
  Mar 9, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  kipenda roho hula nyama mbichi...!
   
 13. M

  Mabulangati JF-Expert Member

  #13
  Mar 9, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 779
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Crashwise mimi si wa hivyo ndugu, kimeshapitishwa na mahakama hakina siasa. Hakijaniuma kwa kuwa ndiyo justice na justice haina siasa.
   
 14. G

  Giddy Mangi JF-Expert Member

  #14
  Mar 9, 2011
  Joined: Feb 14, 2011
  Messages: 833
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  2po pamoja Mh Lissu
   
 15. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #15
  Mar 9, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  unaiaibisha ID yako. We ndo unakurupuka haswa. Ebu soma tena ndo umuelewe mwenzio.
   
 16. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #16
  Mar 9, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Hongera Lissu, Hongera Singida Mashariki, Hongera CDM.
   
 17. c

  carefree JF-Expert Member

  #17
  Mar 9, 2011
  Joined: Dec 19, 2010
  Messages: 265
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Duh mawakili wetu hovyo sana kama walijua wateja wao hawana vijisenti vya kugharamia kesi kwa nini walienda kuisumbua mahakama wkt kuna watu wamejaa magerezani wakisubiri majaji hao wawasikilizie kesi zao
   
 18. MartinDavid

  MartinDavid JF-Expert Member

  #18
  Mar 9, 2011
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 876
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  hongera sana TUNDU LISSU!!
   
 19. samirnasri

  samirnasri JF-Expert Member

  #19
  Mar 9, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Aliyeweka thread hajakurupuka ni ulimi kuteleza tu akasema novemba badala ya octoba. Pili unaposema afanye chunguzi kabla kuandika unakosea, yeye alikua hana uhakika ndio maana akaandika tetesi. Tusiwe tuna challenge kila kitu ili tuonekane sisi tunajua sana. Tetesi haiitaji kufanyiwa uchunguzi kiasi unachotaka wewe vinginevyo neno tetesi halina maana. Hongera lissu.
   
 20. jeviounipers

  jeviounipers Member

  #20
  Mar 9, 2011
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 68
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 15
  CAMARADARIE says thanks for every POST,constructive and destructive, so strange!
   
Loading...