Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 269,632
- 697,794
Japo kazeeka lakini kila nimwonapo nakumbuka alivyotikisa enzi hizo pale kijijini mpaka kupelekea mimi kupata mkasa huu nyumba yao ilikuwa inapakana na shamba la migomba hivyo kila jioni nilifika migombani na kurusha jiwe kwenye paa la nyumba yao naye hutoka na kuja, tulichokosea ni kwamba hatukubadili mbinu, kumbe mamaake akawa kashtukia kale kamchezo bwana, siku hiyo nimetinga viwalo vipya nikatia timu kwenye venue yetu, nikarusha jiwe, dakika chache baadae nikaona mtu anatoka na sufuria kabla sijatafakari vema nikajikuta nimemwagiwa ukoko wa ugali na mamaake huku akinisindiza na matusi ya kipwani, break ya kwanza ilikuwa home, nanuka ukoko mwili mzima huku natetema kwa baridi.
kwakweli kila nikikutana na Tina huwa nakumbuka mkasa huu.
kwakweli kila nikikutana na Tina huwa nakumbuka mkasa huu.