Melubo Letema
JF-Expert Member
- Apr 1, 2020
- 370
- 355
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa naMichezo Dkt. Suleiman Selela atakabidhi bendera na kuiaga timu ya Taifa itakayoshirikikatika Michezo ya Olimpiki ya Majira ya joto inayoanzasiku ya Ijumaa Julai 26 hadi Jumapili Agosti 11, 2024 jijiniParis na miji mingine 16 nchini Ufaransa.
Makamu wa rais wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) Henry Tandau amesema hafla hiyo ya kukabidhi bendera nakuwaaga jumla ya wanamichezo 15 wataoiwakilishaTanzania katika michuano hiyo ya Olympiki mwaka huu, itafanyika kuanzia saa tatu asubuhi katika Uwanja waBenjamin William Mkapa jijini Dar es salaam.
Tandau amesema katika toleo hili la 33 la Michezo hiyoya Olimpiki, kikosi cha Tanzania kitakuwa na nahodhamkimbiaji Alphonce Felix Simbu ambaye pamoja namkimbiaji mwenzie Gabriel Geay watashiriki katika mbioza Marathon kwa wanaume.
Ametaja wengine kuwa ni wanariadha Jackline JumaSakilu na Magdalena Crispin Shauri, ambao watashirikimichuano ya Marathon kwa wanawake.
Pia amewataja waogeleaji wawili, Sophia Anisa Latiffatakayechuana mita 50 freestyle, kategoria ya wanawake naCollins Phillip Saliboko atakayecheza mita 100 freestyle kwa wanaume.
Mwanamichezo wa saba ni Andrew Thomas Mlugu, atayeshiriki katika mashindano ya mchezo wa Judo,
Tandau amesema timu hiyo itaambatana na makocha 3 wafani hizo tatu za michezo, daktari wa timu, Mwambata waMawasiliano na Habari pamoja na maafisa wawili kutokaTOC.
Zaidi ya wanamichezo 10,500 kutoka mataifa 206 wanatarajiwa kushiriki katika matukio 329, na fani 45 tofauti za michezo. Kwa mara ya kwanza kila jinsia itawakilishwa na wanamichezo 5,250.
Katika michezo hiyo kutakuwepo na Breaking (aina yabreakdancing) ambayo itakuwa ikichezwa kwa mara yakwanza kwenye Olimpiki, pamoja na kuteleza kwa ubao(Skateboarding) kupanda ukuta na kuelea kwenye mawimbi(surfing) makubwa ya bahari.
Tanzania ilishiriki kwa mara ya kwanza katika Michezo yaOlimpiki mwaka 1964 huko Tokyo, Japan, na toka wakatihuo imepeleka wanariadha kushiriki katika kila Michezo yaOlimpiki ya Majira ya joto isipokuwa ile iliyosusiwamwaka 1976, ila haijawahi kushiriki Michezo ya Olimpikiya Majira ya baridi.
Mwaka huo wa 1976, nchi 29, nyingi zikiwa za Kiafrika, zilisusia Michezo ya Olympic iliyofanyika Montreal, Canada, baada ya Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC) kukataa kuipiga marufuku New Zealand, baada ya timuyake ya kitaifa ya raga (rugby) kuzuru Afrika Kusinimapema mwaka 1976 kinyume na wito wa Umoja waMataifa wa michezo ulioiwekea Afrika Kusini vikwazokutokana na msimamo wao wa ubaguzi wa rangi.
Kamati ya Taifa ya Olimpiki ya Tanzania iliundwa mwaka1962, ili kushiriki michezo ya Jumuiya ya Madola mjiniGlasgow, Scotland. Mwaka 1968 TOC ilitambuliwa rasmina Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC).