Timu ya Taifa ya "TAEKWONDO" kushiriki mashindano ya Afrika Maputo. Serikali yaitelekeza.

Saharavoice

JF-Expert Member
Aug 30, 2007
3,882
2,374
Timu ya Taifa ya Taekwondo inatarajiwa kuondoka siku ya Ijumaa tarehe 9 Sept 2011 kuelekea maputo Msumbiji kushiriki kwenye michezo ya Afrika. habari kutoka ndani ya kambi hiyo zinadokeza kwamba licha ya juhudi kubwa zinazofanywa na wakufunzi na wachezaji kuhakikisha wanaiwakilisha vyema nchi yetu huko, serikali imeshindwa kutoa msaada wowote kwa timu hiyo.
Habari za kiuchunguzi zinaonyesha kwamba Timu hiyo imewezeshwa usafiri na baadhi ya wapenda michezo, ingawa mpaka sasa bado wanahangaika kutafuta pesa za kujikimu watakapokuwa Mjini Maputo.

My take
Ni lini Serikali itaanza kuwekeza kwenye michezo mingine kama hii ya Taekwondo? au michezo ni football tu? ikumbukwe kwamba Twiga Stars pia iko Maputo kwa mashainadano haya haya. Je Twiga Stars nao wametelekezwa kama hawa wa Taekwondo?
 
Mkuu,
Hivi watabeba Bendera ya Taifa gani?...Kama ni hilihili la kwetu bora wa-canseli safari hiyo!
Nani atakayewakabidhi hiyo bendera?...Dr Nchimbi?
Anyway, siwezi shangaa, maana kama baba mwenye nyumba ana mambo mbofumbofu, lazima na watoto wanaigiza!
 
Serikali yetu bwana......
Siasa gani inafanya bila ya kuthamini michezo?
Tujifunze kutoka Ethiopia na majirani zetu Kenya.
Hakika tutapata medali nyingi hadi tushindwe pa kuziweka
 
Mkuu,
Hivi watabeba Bendera ya Taifa gani?...Kama ni hilihili la kwetu bora wa-canseli safari hiyo!
Nani atakayewakabidhi hiyo bendera?...Dr Nchimbi?
Anyway, siwezi shangaa, maana kama baba mwenye nyumba ana mambo mbofumbofu, lazima na watoto wanaigiza!

Si unajua serikali inavizia? wakifanikiwa kubeba mamedali ndo utawasikia, mpaka Bungeni wataitwa. shame.
 
Back
Top Bottom