Timu ya taifa ya Chad yajitoa michuano ya kufuzu kombe la mataifa ya Afrika (AFCON 2017)

Amavubi

JF-Expert Member
Dec 9, 2010
30,156
13,249
Timu ya Taifa ya Chad imejitoa kwenye mashindano yanayoendelea ya kufuzu michuano ya kombe la mataifa ya Afrika, 'Afcon 2017' wakitoa sababu ya ukata wa fedha kuelekea mechi yao ya pili dhidi ya Tanzania ambayo ilipangwa kufanyika Machi 28 uwanja wa taifa, Dar es Salaam.

Timu hiyo ya Afrika ya kati ilipoteza dhidi ya Taifa Stars Jumatano ambapo Tanzania iliandika ushindi wa kwanza kwenye michuano hio mikubwa zaidi barani Afrika.

Barua iliyoandikwa na mamlaka ya michezo Chad imesomeka "Kama sehemu ya ushiriki wetu kwenye michuano ya kufuzu kombe la mataifa ya Afrika nchini Gabon 2017 na hasa mechi yetu ya marudiano na Tanzania, tunatoa angalizo kwamba timu yetu ya taifa imeshindwa kufika kwenye mechi ya marudiano Dar es Salaam Machi 28"

"Tunawatakia kila lakheri na tunaomba radhi kwa hali hii" Ilisomeka sehemu ya barua hio. Chad wanashikilia mkia kwenye kundi G bila alama yoyote baada ya kufungwa mechi tatu.

Kulingana na kanuni za shirikisho la michezo Afrika(CAF) matokeo yataondolewa hivyo mechi za Chad kwenye kundi G hazitahesabika, hio inamuacha Misri kubaki kinara wa kundi na alama nne, akifatiwa na Nijeria mwenye alama 2 na Tanzania kubaki na alama moja, Misri na Nijeria mechi yao itajechezwa Machi 29 mjini Alexandria. Pia kundi kundi G halitaweza tena kutoa mshindwa bora 'Best looser' kwani makundi yenye timu tatu huwa hayatoi mshindwa bora hivyo timu pekee itakayoenda Afcon nchini Gabon ni ile itayokuwa kinara wa kundi pekee.

12801533_573567216153002_2476720358037686431_n.jpg
 
Mhh! Hii ishakuwa taabu, watu tushaanza kupanga jinsi ya kupiga pesa siku ya mechi leo mnaleta balaa gani tena.
 
wanatufanyia maksudi kwa vile wanajua wao hawawezi kushiriki hawataki tuchukue point zetu ili sasa tuwe sawa na Nigeria hawa lazima wanatufanyia hujuma!

je juzi wangetufunga si wangekuja kwa mbembwe na vipi kuhusu mapato waliyopata kwenye mechi ya juzi si inawatosha kabisa kuwaleta hapa Tz alafu tuwachape tuchukue point zetu alafu wakajitoe huko mbele....
 
Ukiangalia kuanzia article 61 hadi 69 ya African Cup of Nations inaonesha cosquences
 

Attachments

  • 1459089912135.jpg
    1459089912135.jpg
    63.9 KB · Views: 40
  • 1459089934726.jpg
    1459089934726.jpg
    68.9 KB · Views: 48
  • 1459089948266.jpg
    1459089948266.jpg
    62.6 KB · Views: 48
Swali kubwa hapa ni Tanzania tunanufaikaje na kujitoa huku??

Jibu ni hakuna unufaikaji wowote, maana hao jamaa Misri na Nigeria kuashinda ni ndoto za mchana saa tisa baada ya kulewa shibe ya pilau la pasaka
 
Tuache ujinga ujinga sasa hii ni fursa ya kufanya 'biashara' kwani sisi ndo wenye ticket ya mshindi wa kwanza wa hili kundi. .... Eeheeee na hilo ndo football la africa. Unafikiri chad wamejitoa bure bure bila mkono wa ma-falao? Anyway haya mambo huwa hayaongelewi hadharan
 
Shirikisho la Soka Africa (Caf), limetangaza kuiondoa Chad katika michuano ijayo kuwania kufuzu kucheza Afcon na mingine yote iliyo chini yake.
Kama hiyo haitoshi, Caf imetangaza kuitwanga Chad faini ya dolla 20,000 (zaidi ya Sh milioni 44) kutokana na kitendo chake cha kujiondoa katika michuano ya ya kuwania kucheza Afcon.

Chad ilitarajiwa kucheza kesho dhidi ya Taifa Stars kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam baada ya kuwa imetwangwa bao 1-0 kwao ND’jamena.
 
Shirikisho la Soka Africa (Caf), limetangaza kuiondoa Chad katika michuano ijayo kuwania kufuzu kucheza Afcon na mingine yote iliyo chini yake.
Kama hiyo haitoshi, Caf imetangaza kuitwanga Chad faini ya dolla 20,000 (zaidi ya Sh milioni 44) kutokana na kitendo chake cha kujiondoa katika michuano ya ya kuwania kucheza Afcon.

Chad ilitarajiwa kucheza kesho dhidi ya Taifa Stars kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam baada ya kuwa imetwangwa bao 1-0 kwao ND’jamena.
Milioni 44 ni ndogo sanaaaaaa,
 
Back
Top Bottom