Timu ya taifa ina sababu gani ya kutowaita wachezaji wetu wa kimataifa?

mundele

Member
Jun 5, 2009
45
1
Nimejaribu kuisoma na kuichanganua timu yetu ya taifa na kujiuliza je? nini chanzo cha kutofanya vizuri katika michezo ya kimataifa? je? inawezekana kwamba ni tatizo la kocha kama wengi wetu tunavyofikiria? au ni urasimu uliopo kwenye vyama vyetu vya michezo nchini??? lakini nimegundua kwamba Tanzania ina wachezaji zaidi ya 10 wanaocheza mpira wa kimataifa katika mataifa mbalimbali ulimwenguni na wengiwao kwenye Super league za mataifa hayo...Nafikiri labda tungewatumia hao wachezaji wetu wa nje labda wangekuja na technics mbalimbali za kimpira walizozipata kutoka huko kwenye vilabu vyao kuliko kungangania suala la kocha ambalo linaonekana ni ndiyo tatizo kwa sasa...Huo ni mtazamo wangu tu wadau, Kazi kwenu.....
 
Ebu wataje hao wachezaji basi!
 
Hakuna wachezaji wa Tanzania walio nje ambao ni bora kuliko walio ndani ya Tanzania.

Wachezaji wanapaswa kuteuliwa timu ya Taifa kama tu wanafikia viwango vinavyotakiwa, si tu kama wanacheza nje.

Kama alivyosema mchangiaji wa kwanza, wataje walio na kiwango. Kwanza tungeshawasikia kama tunavyowasikia wa nchi nyingine.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom