Timu ya Rais yatakiwa kuwataja mafisadi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Timu ya Rais yatakiwa kuwataja mafisadi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BAK, Mar 15, 2008.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Mar 15, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,601
  Likes Received: 82,167
  Trophy Points: 280
  Posted Date::3/14/2008
  Timu ya Rais yatakiwa kuwataja mafisadi

  Na Ramadhan Semtawa
  Mwananchi

  MJADALA wa kutaka kutajwa majina ya watuhumiwa wa ufisadi katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ya Benki Kuu (BoT), umezidi kushika kasi ambapo Timu ya Rais ya kusimamia mchakato huo imetakiwa kuwataja ili kuwapa wananchi haki ya kuwafahamu.

  Kutotajwa majina ya watuhumiwa hao ni moja ya mjadala mzito unaoitikisa nchi kwa sasa, kutokana na mtazamo wa wengi kwamba, waliochota mabilioni hayo ya umma, ni vigogo ndani na nje ya serikali.

  Akizungumza na gazeti hili jana, Makamu wa Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Eric Ng'mario, alisema wananchi wengi wanataka kujua majina ya watuhumiwa hao na pia ni haki yao kuwajua.

  Hata hivyo, Ng'mario aliweka bayana kwamba ni jukumu la timu hiyo kuangalia umuhimu wa kutaja watu hao na upande mwingine athari zake kiupelelezi.

  "Wananchi wana haki ya kujua majina ya watuhumiwa, ni suala la tume kuangalia na kuweka katika mizania, kuona umuhimu na athari za kuwataja watu hao ," alifafanua.

  Alisema hakuna njia ya mkato ya kutowataja watu hao, kwani hata kama si sasa, lakini ni lazima watajwe mwisho wa siku tume ikimaliza kazi.

  Mwanasheria huyo aliongeza pia kwamba, hakuna njia ya mkato lazima watu hao mwisho wa siku wafikishwe mahakamani.

  Kwa msisitizo, Ng'mario alisema suala la kurejesha fedha ni hatua moja muhimu na ya kushitakiwa ni nyingine hivyo Watanzania watataka kuona watuhumiwa hao wanashitakiwa.

  Alisema sheria za Tanzania si kama Marakeni ambako mtu anaweza kukubaliana kurejesha fedha, lakini asishtakiwe, hivyo ni matumani ya Watanzania kuona watuhumiwa wakirudisha fedha na kushitakiwa.

  "Marekani sawa, mtu anaweza kurudisha fedha halafu akafanya mazungumzo asishitakiwe, sisi hapana lazima tuone watuhumiwa wote wanashitakiwa," alisisitiza Ng'mario.

  Kuhusu mchakato, alisema ni vema watu wakawa na subira kwani miezi sita si mingi ambayo mwisho wa kazi ya timu hiyo itapaswa kuwa imechukua hatua zote.

  "Nafikiri ni suala la wakati tu, tunaweza kuichia timu ifanye kazi yake katika kipindi chote cha miezi sita, mwisho wa siku itatoa majibu,"alisisitiza.

  Katika hatua nyingine, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Profesa Benno Ndulu, leo anatarajiwa kufanya mkutano na wandishi wa habari.

  Hata hivyo, hadi jana jioni ajenda za mkutano huo hazikuwa zimefahamika vema.

  Kwa sasa BoT inaangaliwa kama taasisi ambayo inahitaji kusafishwa, kutokana na sakata la tuhuma za ufisadi wa zaidi ya Sh133 bilioni katika EPA.

  Tofauti na hoja iliyotolewa na wadau mbalimbali wakiwamo wanaharakati, kamati hiyo inayoongozwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) Johnson Mwanyika, imetoa taarifa yake ya tatu ambayo imeshindwa kujibu hoja ya vipi watuhumiwa hawakamatwi.

  Hata hivyo, kinyume na agizo hilo na sheria za nchi, watuhumiwa hao katika makampuni 22 yaliyochota fedha hizo, wamekuwa wakirejesha fedha bila kukamatwa huku kukiwa na usiri wa kutaja majina ya makampuni yaliyorejesha fedha na watuhumiwa.

  Juzi timu hiyo chini ya Mwanyika ilivyozungumza na wahariri, pia ilisita kutaja majina ya watuhumiwa na makampuni kwa madai ya kuogopa kuvuruga upelelezi.

  Ufisadi katika EPA ulibainika baada ya ukaguzi wa kimataifa wa Kampuni ya Ernst&Young, ambao awali uliibuliwa na Deloitte&Touche, ulimfanya Rais Jakaya Kikwete, kutengua uteuzi wa gavana Daud Ballali na kuunda timu hiyo chini ya Mwanyika.
   
 2. N

  Ngurudoto JF-Expert Member

  #2
  Mar 15, 2008
  Joined: Mar 13, 2008
  Messages: 208
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  NEW TANZANIA NDIO HII
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  Mar 15, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,601
  Likes Received: 82,167
  Trophy Points: 280
  Wewe uliye katika old Tanzania huitakii mema nchi yetu maana old Tanzania tulikuwa hatuna mafisadi kama tulionao hivi sasa. Acha kulala usingizi mzito! fungua macho uone udhalimu wa mafisadi!
   
 4. a.9784

  a.9784 Senior Member

  #4
  Mar 18, 2008
  Joined: Feb 19, 2008
  Messages: 146
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwizi hawezi kujitaja.
   
Loading...