Tetesi: Timu ya Gor Mahia Fc inayoshiriki Ligi Kuu nchini kenya imeanza mipango ya kutafuta Saini ya kocha Msaidizi wa Simba Matola

AbbasTwalb

Member
Oct 15, 2020
11
75
Timu ya Gor Mahia Fc inayoshiriki Ligi Kuu nchini kenya imeanza mipango ya kutafuta Saini ya kocha Msaidizi wa sasa wa Simba Selemani Matola.

Hii inakuja Baada ya Mabingwa hao Wa Kenya kukaa kwa muda mrefu bila kuwa na Kocha wa kiwango kizuri cha kuifundisha timu hiyo ambayo hapo awali ilikuwa chini ya Kocha Roberto Oliviera ambaye aliondoka Klabuni hapo Wiki chache zilizopita.

Tetesi zinasema Gor Mahia wanamuangalia Matola kama chaguo lao lakwanza kwani Wamekuwa na Matokeo yasiyo yakufurahisha katika kipindi cha mienzi ya Hivi karibuni na wanatazamia Kuingia nae mkataba mapema iwezekanavyo huku wachambuzi wengi wa Soka wakisema kwamba Zoezi hilo huenda likapata upinzani mkubwa kutoka kwa waajiri wake wa Sasa Simba ambao bado wanahitaji huduma ya kocha huyo Mtanzania.

Hii ni taarifa njema kwa makocha wa Tanzania baada ya kuwa na kipindi kirefu cha kutokuaminika kiasi cha kukosa ajira za ukocha nje ya Nchi kutokana na wengi wao kuonekana hawana Makali katika kazi zao huku wenzao wa Burundi wakionekana kula Shavu kila uchwao.

NB. PICHA KWA HISANI YA MUUNGWANA
selemani-matola_1mpcc1qm0d1jh1iv32d2i10p4v.jpg
 

Magema Jr

JF-Expert Member
Apr 22, 2020
1,100
2,000
Matola huyu huyu MATOLE wa pale mikiani??😁😁
Hata hivyo hamalizi game 6 kibarua kiote ukoka😂😂

#nikiongea ndo nimemaliza
#jr
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom