Timu ya Everton inayoshiriki ligi kuu ya Uingereza kutua nchini

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,890
17457728_901734583302533_651348095612929093_n.jpg

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga amekutana na muwakilishi wa Sports Pesa Tanzania,Luca Neghesti kumpa taarifa Waziri huyo kuhusu maandalizi ya kuileta timu ya Everton inayoshiriki ligi kuu ya Uingereza kwa ajili ya kucheza mechi za kirafiki hapa nchini.

Waziri huyo pia amekutana na wawakilishi wa timu hiyo ofisi kwake jijini Dar es salaam kwaajili ya ziara hiyo hapa nchini.

Aidha Waziri Mahiga amesema ziara hiyo itasaidia kuitangaza Tanzania duniani pamoja na kuhamasisha mchezo wa mpira wa miguu kwa vijana wa Kitanzania.
 
kuhamasisha kivipi maana timu ya taifa wanateuliwa simba na yanga matokeo anapanga dj malinzi viwanja vingi ni vipara yaani makorongo tu hata kama wangekuja wachezaji wa ligi ya EPL hamna kitu
 
kuhamasisha kivipi maana timu ya taifa wanateuliwa simba na yanga matokeo anapanga dj malinzi viwanja vingi ni vipara yaani makorongo tu hata kama wangekuja wachezaji wa ligi ya EPL hamna kitu
Umeishia kuorodhesha matatizo tu ila huna solution
 
Waambie waje waje

Oh oh Waje ......Waje

Waje na mashabiki wao waje! ooh waje waje​
 
Back
Top Bottom