Timu nane tu zimetwaa Kombe la Dunia Tangu lianzishwe miaka 83 iliyopita

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,883
6,883
Pele-and-Brazil.png

Kikosi cha Brazil kilichoongozwa na mchawi wa soccer Pele
Italy-soccer-team.jpg Italy download (1).jpg German download (2).jpg Argentina download.jpg Uruguay download.jpg France download (5).jpg Hispania 2012-634746297073729390-372.jpg England

Kwa kipindin cha miaka 83, fainali za Kombe la Dunia zimefanyika mara 19, lakini hadi sasa ni timu nane tu ambazo zimeshatwaa ubingwa wa michuano hiyo mikubwa ya soka duniani.
Fainali hizo zilifanyika kwa mara ya kwanza mwaka 1930 nchini Uruguay na zimekuwa zikifanyika kila baada ya miaka minne, isipokuwa mwaka 1942 na 1946 kutokana na Vita Kuu ya dunia .


  1. Brazil inaongoza kwa kutwaa Kombe la Dunia baada ya kutwaa taji hilo mara tano. Brazil ilitwaa taji hilo nchini Sweden mwaka 1958, nchini Chile (1962), Mexico (1970), Marekani (1994) na Korea/Japan (2002). Brazil pia ndiyo nchi pekee iliyoshiriki fainali zote za Kombe la Dunia tangu zilipoanzishwa mwaka 1930 na imefunga jumla ya 210 katika fainali 19.
  2. Italia imetwaa ubingwa huo mara nne. Ilitwaa taji hilo kwa mara ya kwanza ilipoandaa mwaka 1934, baadaye nchini Ufaransa (1938), Hispania (1982) na Ujerumani (2006). Italia imeshiriki fainali hizo mara 17 na kufunga mabao 126.
  3. Ujerumani Magharibi (sasa Ujerumani) Kati ya 1950 na 1990, ilitwaa ubingwa mara tatu. Ilitwaa ubingwa nchini Uswisi 1954, na baadaye ilipoandaa fainali hizo mwaka 1974 na nchini Italia (1990). Kati ya 1930 mpaka 2010 Ujerumani imeshiriki fainali hizo mara 17 na imefunga mabao 206.
  4. Argentina Mwaka 1978 ilikuwa ni taifa la tano kutwaa ubingwa wa dunia. Ilitwaa tena ubingwa wa dunia mwaka 1986. Tangu 1930 mpaka 2010, Argentina imeshiriki fainali hizo mara 15 na kufunga mabao 123.
  5. Uruguay ilikuwa nchi ya kwanza kutwaa kombe hilo wakati ilipoandaa fainali hizo 1930. ilitwaa kombe hilo kwa mara ya pilimwaka 1950 nchini Brazil. Uruguay imeshiriki Fainali za Kombe la Dunia mara 13 na kufunga mabao 76.
  6. Ufaransa imetwaa ubingwa wa dunia mara moja mwaka 1998 walipokuwa wenyeji. Ufaransa imeshiriki fainali hizo mara 13 na kufunga mabao 13.
  7. Hispania ilisubiri hadi mwaka 2010 kutwaa kombe hilo kwa mara ya kwanza na ndio mabingwa watetezi. Hispania imeshiriki fainali hizo mara 13 na kufunga mabao 88.
  8. England iliandaa na kutwaa ubingwa mwaka 1966. Imeshiriki mara 13 na kufunga mabao 77.
 

Attachments

  • download (6).jpg
    download (6).jpg
    14.7 KB · Views: 378
Yaani wengine wote dunia nzima wanasindikiza tu.

Siku Tanzania ikifuzu kuingia kombe la dunia ndio siku ambayo Africa itatwaa kombe hilo.
 
Timu saba tu ndo zimebeba, Waingereza (England) kama kawaida ya kupora na kuiba vya watu waliliiba kombe la dunia 1966.
 
wachezaji wanaolipwa hela za kununua karanga mnataka muwalindanishe na wanaoendesha million dollar cars, hapo hata kipaji lazima kitofautiane... waombeni msamaha kwa kuwacompare
 
Timu nane au nchi nane...?

Hata ikiwa nchi mwenyeji huwa na timu moja tu inayowakilisha nchi, kwa maana hiyo kila timu iliyochukua ubingwa inawakilisha nchi. Nchi haichezi mpira wa miguu kombe la dunia, ila nchi inakuwa na timu ya mpira wa miguu inayowakilisha nchi katika ushindani kombe la dunia.
 
duh!hapo kwa ufaransa panantia shaka yan ndiyo timu iliyofunga magoli machache kupitiliza ukilinganisha na ushiriki wao
 
duh!hapo kwa ufaransa panantia shaka yan ndiyo timu iliyofunga magoli machache kupitiliza ukilinganisha na ushiriki wao

Inawezekana baadhi ya miaka ya ushiriki wao kombe la dunia walikuwa wasindikizaji ni kupigwa tu.
 
Hili la Ufaransa kushiriki mara 13 na kufunga mabao 13 likoje.

kwanza 98 tu nafikiri hayo magoli 13 walifikisha,walichukuaje ubingwa?ikiwa final tu walishnda 3-0?nusu?robo?makundi?duh,weka takwimu zako sawa mkuu
 
Hili la Ufaransa kushiriki mara 13 na kufunga mabao 13 likoje.

Hapa naona kutakuwa na typing error. Mchezaji mwenye rekodi ya kufunga magoli mengi zaidi kwenye fainali moja za kombe la dunia alikuwa mfaransa Justine Fontaine, na alifunga magoli 13 fainali za 1958!
 
dah hii cjapata kujua aisee, halafu hwa brazil hata friendly match cwaoni kwenye ratiba ndo wanajiamini sana au?
 
Back
Top Bottom