Timu kamambe ya CCM inayoungwa mkono sana na CHADEMA! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Timu kamambe ya CCM inayoungwa mkono sana na CHADEMA!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kibunago, Oct 9, 2012.

 1. Kibunago

  Kibunago JF-Expert Member

  #1
  Oct 9, 2012
  Joined: Jan 11, 2008
  Messages: 288
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Hapo chini, ndio timu ya CCM (Musoma) ambayo CHADEMA inapozisoma namba zake, kibwagizo cha CCM- PURESHA INAPANDA INASHUUUKA! (CCM Presha inapanda inashuka - YouTube) kinaanza kupigiwa jalamba. CHADEMA wana kila haki ya kusema "Asante Mungu, mapenzi yako ya M4C yaendelee kutimizwa hapa Musoma kama huko Arusha na hata utakapotimu mwaka wa mwisho wa kutawala kwake Kikwete, muendelezo mjini Musoma na Mara kwa ujumla utakuwa ‘CHADEMA mwendo mudundo!"

  TIMU KAMAMBE INAYOINGIA UWANJANI:

  Mwenyekiti wa CCM (W) – Daudi Misango, Ex- diwani, Ex- Makamu Meya aliyepigwa chini. Ana rekodi za kuwa wa kwanza kuingia bar na rekodi ya kuwa wa mwisho kuondoka bar kwa fedha yake au ya kupiga wateja wengine mabao!

  MNEC - Vedastus Mathayo – Ex- Mbuge aliyepigwa chini. Ana rekodi ya kulazimisha wajumbe wote wa Jumuiya za CCM, na wa Matawi na Watendaji Kata zote kuwa lazima wamuunge mkono na kumsujudu kwa kutembeza fedha. Yuko Out of touch na matatizo ya wananchi isipokuwa kuhakikisha kuwa biashara zake zinaendelea kwa kasi ya kuzipiku za wengine wote.

  Mwenezi wa Itikadi (W) Ramadhan aka Musoma Bus – Ni mwenye ustadi wa kuongea neno lolote popote mbele ya halaiki hata la kutapeli akisema ‘katumwa kumwakilisha mama Maria Nyerere au hata Rais Kikwete' kufikisha ujumbe wake. Ulipo mgao wa fedha haramu, hapo atakaa na kulala. Kwamba, uwezo wa kueneza itikadi za chama na kuhamasisha umma haupo na kwamba maadili yake na hata uwezo wa kufikiri ni hafifu, CHADEMA wamelamba madume tupe!

  Mwenyekiti UVCCM (M) aliyepatikana jana kwa kulazimisha ni- Kijana asiyekifahamu Chama wala hasiye na uwezo wa kuhamasisha vijana wa karne ya 21 yuko kwenye payroll ya Ex- Mwenyekiti UVCCM (M)- Marwa Mathayo na Vedastus Mathayo, viongozi waliopoteza heshima na kukosa mvuto popote Musoma isipokuwa kwenye pump zao za mafuta (yaliyochakachuliwa). Tena ni hatari kwa sababu pia ni watu wenye visasi sana; pata habari kamili toka familia ya Mhasibu wao aliyeuwawa kinyama na hata chuki zao kwa Ex- Mbunge, Mh. Mkuu wa Wilaya ya Nyang'hwale Ibrahim Marwa! Kisa ni kusema bungeni kuwa Mathayo & sons na kampuni ya Hass Petroleum (T) hawakuwa wanalipa kodi stahiki na ni bayana hata ukaguzi uliofanyika Musoma walikamatwa wakichakachua mafuta ambapo fedha zake zinatumika kuisambaratisha CCM Mara.

  Mimi mwanachama mkongwe wa CCM, sitabiri bali naeleza hali halisi itakavyokuwa kwamba ninyi Viongozi wa CCM (T), endeleeni kunyamaza tu kama vile hamyajui au kuyaona haya maana huu wimbo (CCM Presha inapanda inashuka - YouTube) hauchuji wala hauhitaji kumleta Msanii aliye juu -Bongo kuunzisha majukwaani.

  Mwenyekiti J. Kikwete, Katibu W. Mkama na kijana Nape, mnawezaje kukubali kuwa uchaguzi unaweza kuitwa huru na wa haki katika mazingira ya vita vya wazi ambapo watu wamechapana kwa viti, mawe na silaha hadi wajumbe wengine kujeruhiwa na kuonyeshwa kwenye TV? Mnasubiri, tume iundwe ndio iwambie kuwa kweli uchaguzi ulivurugwa na kuna watu wanastahili kuadabishwa kwa kutoa rushwa na pia kujenga hatari ya ukabila mkoani Mara?

  Ninyi mnalijua vyema hili lengo la CCM katika Ibara ya 16 ya Katiba ya CCM ya 1977 toleo la 2010,
  " Kuona kwamba katika nchi yetu hakuna aina yoyote ya dhuluma, vitisho,
  ubaguzi, rushwa, uonevu na/au upendeleo".


  Leo wale vijana wote wanaojituma wa UVCCM – Mara ambao hawakuwa na sponsors wenye fedha za kugawa na kugawiwa wanalia wakisema, hiyo ibara ya 16 haioni! Na siku si nyingi watatafuta Katiba ya chama ambapo mfanano wa ibara hiyo upo na unasimamiwa ipaswavyo bila kumwonea mkiukaji haya!
   
 2. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #2
  Oct 9, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu mhasibu gani huyo tena?
   
 3. t

  true JF-Expert Member

  #3
  Oct 9, 2012
  Joined: Nov 26, 2011
  Messages: 496
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 45
  Mkenya mkuu?!
   
 4. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #4
  Oct 9, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Izrael mtoa roho anaizungukia ccm kila upande!
   
 5. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #5
  Oct 9, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 12,000
  Likes Received: 2,655
  Trophy Points: 280
  Shetani atawavuruga sana magamba,kila kona ni vurumai tu soon wataanza kulipuana kwa mabom.
   
 6. Joseph

  Joseph JF-Expert Member

  #6
  Oct 9, 2012
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 3,527
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Afadhali ya wewe ambaye umeanza kusoma alama za nyakati,unasubiri nini kuhama?Hapo hata useme nini hautasikilizwa
   
 7. C

  Concrete JF-Expert Member

  #7
  Oct 9, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 3,607
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Hili kundi lililoshinda ni mtandao wa nani katika list ya wapigania urais ndani ya CCM?
   
 8. Mandingo

  Mandingo JF-Expert Member

  #8
  Oct 9, 2012
  Joined: Sep 22, 2011
  Messages: 3,380
  Likes Received: 316
  Trophy Points: 180
  Hilo linyimbo ni tamu na lina mzuka kuliko zile za kapiteni kitambi!.....chama chetu cha mwabwepande...chauwa nchiiii....
   
 9. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #9
  Oct 9, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  siku hizi nikiona mtu amevaa shati la kinani natapika hata kma sijala.
   
 10. B

  Baba Hellen JF-Expert Member

  #10
  Oct 9, 2012
  Joined: Jul 2, 2012
  Messages: 764
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  ooooooooh hawa nyinyiem ni marehemu sematu wapo motuary wakisubiri chadema watoe hati yakiwanja chamaazishi
   
 11. HUGO CHAVES

  HUGO CHAVES JF-Expert Member

  #11
  Oct 9, 2012
  Joined: Mar 25, 2011
  Messages: 1,852
  Likes Received: 235
  Trophy Points: 160
  fanya maamuzi sasa mkuu hujachelewa.jiunge na m4c
   
 12. Christine1

  Christine1 JF-Expert Member

  #12
  Oct 9, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 12,275
  Likes Received: 1,204
  Trophy Points: 280
  na endelee kuwazunguka tu,dadadeki
   
 13. W

  Wakwe2 Member

  #13
  Oct 9, 2012
  Joined: Sep 28, 2012
  Messages: 91
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  puresha inapanda inashukaaa mm naomba uandaliwe mkakati wa kuitwaa kilimanjaro hususani jimbo la mwanga na same kuna watani zangu hawaelewi wakipewa kofia na kanga wanajisahau hawajui thamani yao ni zaidi ya kofia na kanga
   
 14. E

  Elizabeth Dominic Platinum Member

  #14
  Oct 9, 2012
  Joined: Dec 7, 2007
  Messages: 4,547
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Kila jambo lina wakati wake, inapofikia wakati wako lazima tu uitike hata kama hutaki....
   
 15. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #15
  Oct 9, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,005
  Likes Received: 739
  Trophy Points: 280
  ngoja tuone.....
   
 16. babykailama

  babykailama JF-Expert Member

  #16
  Oct 9, 2012
  Joined: Mar 5, 2012
  Messages: 241
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Duu Kibs hakika umeandika kwa hisia sana na haya maneno yanatakiwa kufanyiwa kazi.

  Sidhani kwamba kiongozi yeyote mwenye akili timamu anaweza kukubali matokeo ya uchaguzi uliofanywa kwenye fujo za ngumi live ambazo unasema zilioneshwa hata kwenye TV??

  Kwa nini mtu akubalike kuwa kiongozi kama anawagawa watu na anatumia fedha hivi huko Musoma hakuna wazee na vijana wakaibuka na kuwakataa kama ukoma hao akina Mathayo kama kweli wanafanya mambo haya hadharani?

  Kibs nime click huo wimbo nikasisimkwa! mbona kweli tunajiandaa kama mazuzu kupigwa chini?
   
 17. H

  Hon.MP Senior Member

  #17
  Oct 9, 2012
  Joined: Jul 15, 2012
  Messages: 142
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  "Ex- Mwenyekiti UVCCM (M)- Marwa Mathayo na Vedastus Mathayo, viongozi waliopoteza heshima na kukosa mvuto popote Musoma isipokuwa kwenye pump zao za mafuta (yaliyochakachuliwa). Tena ni hatari kwa sababu pia ni watu wenye visasi sana; pata habari kamili toka familia ya Mhasibu wao aliyeuwawa kinyama na hata chuki zao kwa Ex- Mbunge, Mh. Mkuu wa Wilaya ya Nyang’hwale Ibrahim Marwa! Kisa ni kusema bungeni kuwa Mathayo & sons na kampuni ya Hass Petroleum (T) hawakuwa wanalipa kodi stahiki na ni bayana hata ukaguzi uliofanyika Musoma walikamatwa wakichakachua mafuta ambapo fedha zake zinatumika kuisambaratisha CCM Mara."


  Hivi POLISI NA TAKUKURU HAWANA OFISI MARA au nao wako kwenye payrol ya hiyo timu kamambe?

  Lakini hata hivyo kweli ni kichekesho kama watu waliangushwa chaguzi zilizopita sasa wanarudishwa kuongoza chama kweli mtakatiza 2015? Haya subirini tutaona!
   
 18. Kibunago

  Kibunago JF-Expert Member

  #18
  Oct 10, 2012
  Joined: Jan 11, 2008
  Messages: 288
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mkenya aliuwawa tena kwa mateso makali todate hakuna aliyetiwa hatiani! Probably rushwa ilituka hata kubadili vipimo vya madaktari na death certificate! Lakini intelligence ina kila nyendo za hiyo kijana Marwa Mathayo & the coy.
   
 19. Kibunago

  Kibunago JF-Expert Member

  #19
  Oct 10, 2012
  Joined: Jan 11, 2008
  Messages: 288
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0

  Hapo kwenye red, sasa utashangaa kuwa matokeo yanakubalika pengine ni kweli hii ni timu iliyojipanga kwa makusudi mengine makubwa tusiyoyajua. Ole wenu siku wana Musoma (original) wakiamka hao watu watajuta kuishi maisha ya rushwa rushwa na ujanja ujanja wa kitapeli.
   
 20. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #20
  Oct 10, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu nilikuwa nadhani ni yule mhasibu wao tumbo tumbo!
   
Loading...