Timoth Apiyo Alazwa Afrika Kusini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Timoth Apiyo Alazwa Afrika Kusini

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pascal Mayalla, Apr 4, 2009.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Apr 4, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,576
  Likes Received: 18,507
  Trophy Points: 280
  Salaam,
  Habari toka nchini Afrika Kusini, zinasema,
  Katibu Mkuu wa Ikulu Mstaafu, Mzee Timothy Apiyo, amelazwa kwenye hospitali ya Milpark nchini Afrika Kusini.

  Mzee wetu huyu ambaye ni mjamaa wa kweli kama Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, alikuwa ni Katibu Mkuu wa Ikulu kwa Kipindi kirefu mpaka alipostaafu na kuhamia Kinyerezi hapa jijini Dar es Salaam ambapo ameendelea kuishi maisha ya kawaida ya kijamaa kwa kufuata falsafa ya Baba wa Taifa Mwl. Nyerere.

  Mzee Apiyo ambaye kiumri ni mtu mzima, alifiwa na mke na mtoto siku za nyuma, na hivi karibuni, alifiwa tena na mtoto wakati tayari akiwa nchini Afrika Kusini.

  Tunaomba Mungu aifariji familia ya Mzee Apiyo, awape nguvu, baraka na uwezo ili wayaweze yote katika Yeye awatiaye nguvu na kuwapa baraka za uponyaji wa haraka...Amen.
   
 2. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #2
  Apr 4, 2009
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Pasco,

  Huyo mzee wetu amelazwa huko kwa muda sasa. Hiyo habari ni sahihi ingawaje sijui kalazwa hospitali gani.

  Ni kumwombea heri mungu amsaidie ili apate nafuu haraka.
   
 3. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #3
  Apr 4, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0

  - Mzee ni jirani yangu kule Kinyerezi, wiki iliyopita alifiwa na mtoto wake wa mwisho wa kike Toto RIP, kwa sasa amepoteza mke, mtoto mmoja wa kiume aliyekuwa akimuaminia sana John RIP, na mtoto mwingine tena wa kiume Odinga RIP, that is a little bit too much to take at his age.

  - Kwa sasa karibu upande mmoja wa mwili wake umepooza, serikali imekuwa akimhudumia sana, tena sana na ilikuwa baada ya Chadema under Mtei/Ngwilulupi kuipigia kelele sana serikali on afya ya huyu mzee na huko SA amekuwa akienda mara nyingi sana na India, majuzi baada ya huyu mtoto wake kufariki alizidiwa ghafla na akapelekwa mara moja na sasa yupo huko SA hospitali, hali yake sio mbaya ni kawaida.

  - Kwa wakuu wowote humu JF mlioko Poland, sio vibaya mkamkumbusha mtoto wake mkubwa aliyeko huko kwa muda mrefu sana sasa, kwamba awe anajaribu kumcheki cheki mzee, maana wazee wanazeeeka sasa.

  Respect!

  FMES!
   
 4. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #4
  Apr 4, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,576
  Likes Received: 18,507
  Trophy Points: 280
  Pole FMES kwa kuuguza jirani. At his Age na RIP nne na hali hii ya ugonjwa!.
  Mungu amfariji, ampe uponyaji wa haraka, amtie nguvu na kusimama na familia yake.
   
 5. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #5
  Apr 4, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,313
  Likes Received: 5,605
  Trophy Points: 280
  Pole sana mzee wetu mjamaa alisia,sasa huyomtoto wake amejilipua huko poland??mbona ajabusana??yaani anamuachamzee wake ateseke yeye anakula maishatu huko poland?sio vizuri kabisa...msaurini arudi akamsalimie mzee wake...
   
 6. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #6
  Apr 4, 2009
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Tunampa pole sana Mzee Apiyo, Mwenyezi Mungu atamjaalia apate nafuu.

  Katika umri huu mkubwa ambapo watoto huwa wametawanyika kutafuta maisha, wazee wakiugua wanakosa jamaa wa kuwa nao karibu. Kule kwa watani zetu Musoma, wazee wa umri huo huuguzwa na mke mdogo ambaye mara nyingi anakuwa binti mwenye nguvu zake sijui Mzee Apiyo anatokea wapi?
   
 7. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #7
  Apr 4, 2009
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Mkuu FMES,

  Na wewe kwa kupakana na vigunge mbalimbali, kweli umetuzidi kwi kwi kwi!!

  Ni kweli mzee alipoteza huyo mtoto wake wa kike yeye akiwa yuko hospitalini huko SA.

  Unajua ukiwa mbali na matatizo yanakukumba inakuwa balaa tupu. Mungu amsaidie apate nafuu haraka.

  Huyo mtoto wake uliyemsema naamini anasoma JF. Hii JF ni jungu kuu, huwezi kuamini watu wanaoingia humu.
   
 8. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #8
  Apr 4, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Mkuu fafanua....
   
 9. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #9
  Apr 4, 2009
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Pasco,

  Huyo mtu mnayemwongelea yuko karibu sana na babake. Hata kama yuko nje lakini ana mawasiliano ya karibu sana na mzee wake. Naamini hata sasa muda wote anaongea na kumfariji babake. Yeye mwenyewe ni daktari, hivyo anajua vizuri mzee anasumbuliwa na nini.

  Labda FMES hakuelezea vizuri tu lakini mimi namfahamu vizuri na ni muungwana kweli kweli na ana uhusiano wa karibu sana na mzee wake, anaenda TZ muda wote kuwasalimia wazee wake na toka afariki mama yake amekuwa karibu sana na mzee wake.

  Aidha naamini huyo jamaa ni mwana JF mzuri tu, hivyo atasoma mawazo yenu.
   
 10. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #10
  Apr 4, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Mungu amjalie huyo mzee apone na kurejea katika afya yake
   
 11. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #11
  Apr 4, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,576
  Likes Received: 18,507
  Trophy Points: 280
  Asante sana nimefarijika sana na taarifa hii. Tena ndio ilitakiwa itolewe na jirani. Usije kuta ni ujirani wa kizungu wa kuona mapaa tuu, hapa kwa fulani na hapa kwa fulani.

  Mungu awaongoze.
   
 12. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #12
  Apr 4, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,576
  Likes Received: 18,507
  Trophy Points: 280
  Naanzia kwangu mwenyewe, sio nimepiga box, bali nimebeba zege London na baadaye nikahamia US. Baadhi ya niliowaacha London wapo bado huko huko. Na baadhi ya niliowakuta US nimewaacha na hata wakifiwa na wazazi, hawawezi rudi bongo.

  Taarifa yangu inasisitiza ni baadhi. Utakubaliana na mimi, wengi hata wakianzia box baadaye wanabadilisha job to the better. Waangalie wale ambao box ndio wamefika all their life, wakibeba mpaka they can carry no more, wataweza rudi bongo hawa?.
  Baadhi ya rafiki waliorudi, baadhi maisha ya bongo yamewashinda. Nakiri hao ni baadhi tuu na good success stories pia ni nyingi. Nimetembelea baadhi walioko Boston, nilitamani nisirudi ili kupata maisha kama yao, home ni investments kwa kwenda mbele. Ila kufanya kazi ile ile kwa miaka mingi kama haitumii brain, bongo inalala.

  Natanguliza na samahani, I didn't mean to ofend anybody, I'm just putting forward my observation.
   
 13. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #13
  Apr 4, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  Mkuu Mtanzania,

  - Mkuu wangu tena Mwakipesile ndio kabisa yuko karibu zaidi, toka akiwa Manager wa Dawa za mbu, anyways jamaa Dakatari nilichosema ni kwamba wazee wanazeeka asiwasahau sana, sikusema anything zaidi au less, jaamaa ni too decent na a good man, lakini wazee wanazeeka that is all nisingependa kusema zaidi.

  Respect

  FMES!
   
 14. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #14
  Apr 4, 2009
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Mkuu Pasco,

  Tuache na box zetu, mbona tunabeba na nyumbani tunarudi? Hivi kuna kazi haitumii brain? Kutumia brain maana yake nini? Ni kuwa kama Rostam kuchora mipango ya kila aina ya uchafu?

  Wacheni vijana wanaotaka kubeba box wabeba, wanaotaka kurudi TZ warudi ili mradi mtu achague anataka kufanya nini.

  Kitu ambacho nitaogopa ni kuacha kupiga box zangu na kisha kwenda Tanzania kuwaibia maskini. Hicho ni hatari zaidi ya kuendelea kupiga box.

  Jamani msiwe mnazikashifu kazi zetu, hizo zinatufanya tushibe, tusomeshe wadogo zetu, tujengee vibanda vya baba na mama zetu na sisi wenyewe kutufanya tulewe Umkomboti weekend kupumzisha akili.
   
 15. Steven Sambali

  Steven Sambali Verified User

  #15
  Apr 5, 2009
  Joined: Jul 31, 2008
  Messages: 314
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Skills, polepole ndugu yangu. Huna uhakika na maneno na tayari unaanza kuandika habari usizo na uhakika? Jamaa anaishi kihalali na wapi mtu anaishi ni maamuzi yake. Hata Mzee Timoth alihamia Dar na hajarudi kwao Mara.

  FMes,
  Juzijuzi tulikuwa tumefiwa na mwenzetu hapa Poland jamaa mwenyeji wa Kigoma aitwaye Kiboyi Kituli. Tulikuwa kwenye mazishi pamoja na Dr. Apiyo. Ila mwenzetu kumbe pia alikuwa katika kuuguza baba na dada yake. Apiyo yuko well informed na zaidi ya hivyo ni kuwa ndiye anaamua nini kifanyike na wapi hasa inapokuja kwenye ushauri wa kimatibabu. Ugonjwa wa mzee wake anaufahamu sana kwani na yeye ni dr wa mioyo.
  Huenda nyumbani mara kwa mara na hata mwezi wa 12 watoto wake walienda peke yao kutembea Tanzania. Hivyo jamaa hajaoza wala kusahau Tanzania. Nimeongea naye jioni hii na hata siku amepata msiba niliongea naye. Ndiye alikuwa akiagiza mzee aambiwe nini kwa muda ule. Hata wakati wanamwambia kuwa mwanaye kafariki, aliagiza lazima Dr. awepo karibu na alimpima hapohapo na kumpa dawa. Anasema alilia kama robo saa hivi na akatulia ila alimkatalia kurudi nyumbani kwenye mazishi.

  Juu ya ugonjwa wa dada yake, aliagiza rafiki yake wa karibu sana ambaye alienda kuwaona Dr.s wa Muhimbili na baadhi ni wale waliomaliza shule Poland na au wanafahamiana na Apiyo mwenyewe. Ila anasema alivyopata habari hali ilivyo, yeye kama Mganga alikata tamaa ukichukulia hali ya hospital zetu. Akabaki tu kuomba Mungu.

  Pasco,
  Jana ndiyo Mzee Timothy Apiyo kalazwa hospital hiyo ya Milpark. Wizara ya afya walichela kutuma pesa na akawa amefikia kwa rafiki yake. Hata taarifa za msiba alipewa akiwa nje ya hospital. Dr. Apiyo amewasiliana na kuongea hadi na dr. wake mwenye asili ya Kireno na amesema mzee anaendelea vyema. Akishamaliza hayo matibabu ndiyo atahamia kwenye hospital ya Medcare Rehab. Hivyo kidogo informer wako kaongeza chumvi kwa kuweka mambo ambayo yatatokea baadaye.

  Pasco, kama wee ni mwandishi basi Dr. huwa anasoma sana artical zako. Yuko zaidi kwenye mambo ya Blog na akina Mjengwa. Pia ni mwenyekiti wa Rotary club ya hapo kwenye mji anaoshi. Na ukiongeza na majukumu ya nyumbani, nafikiri anakuwa na shughuli nyingi sana. Hata msiba umefika yeye alishinda kazini siku nzima. Amepanga kuwa nyumbani mwezi wa tano. Hivyo kwa hilo nafikiri usiwe na wasiwasi kwani jamaa anaishi vizuri tu na anasaidia sana mzee wake kwa kadri anavyoweza. Hajaoza na wala si mbeba mabox. Haogopi kwenda nyumbani kwani huko huenda mara kwa mara.

  Samahani nimeandika mengi ila tu nilitaka kunyoosha habari ili isije kuwa akikukutwa na watu na kujitambulisha, watu wanasema "huyu alimuachaniza baba yake..." Katika maisha ya kila siku pale Dar, dr ndiye mwenye kuhakikisha kuwa mzee anaishi na kufuata masharti ya Dr's. Huamua nini na lini aambiwe. Wapi aende na lini nk nk. Akisema, NO, basi hakifanyiki kitu.

  Vinginevyo anashukuru kwa watu kuuheshimu mchango wa baba yake na kuwa naye karibu katika kipindi hiki kigumu. Yangu ni hayo....
   
 16. Steven Sambali

  Steven Sambali Verified User

  #16
  Apr 5, 2009
  Joined: Jul 31, 2008
  Messages: 314
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  FMes,
  Unakumbuka timu ya mpira ya Wazee? Nasikia Mwakipesile alikuwa back namba mbili na anakumbakumba kila anayemsogelea. Hadi watu wanakuwa wanakimbia upande wake.
  Ila nasikia alimsulubu yule Mwizi na mwanga kwa kitako cha Bunduki. Duu, hiyo imenimaliza sana sana. Sijawahi kumuona huyu Mwakipesile ila naanza kupata picha ya mtu mmoja Mbabe sanasana na mzinga wa mtu......

  NB: Mtanzania, Dr Apiyo siyo member wa hii forum. Yeye yuko zaidi kwenye blogs na Michuzi.
  Sanasana yupo pia kwenye forum ya Pol.conections na au kuteta na rafiki yake Benny.
   
 17. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #17
  Apr 5, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0

  - Sawa sawa mkuu tupo pamoja ila tu usisahau kumpa mkulu ujumbe wangu, kwamba wazee wamezeeka na wanahitaji msaada wa karibu sana, sina zaidi kwa leo.

  Respect!

  Wazee wa sauti ya umeme FMES!
   
 18. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #18
  Apr 5, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,576
  Likes Received: 18,507
  Trophy Points: 280
  Asante sana S.Sambali, taarifa hii yako ndiyo imejibu swali la hii thread na sasa modereta anaweza kuibadilisha na kuwa sio tetesi tena. Thanks.

  Kuhusu kuhamishiwa Medcare Rehab, siyo Mzee Apiyo, ni mpigapicha wa Daily News, Athumani Hamisi, aliyekuwa amelazwa Milpark sasa amehamishiwa Medcare.

  Taarifa za Dr. Apiyo ni faraja kubwa kwetu sote
  Naomba sasa tuelekeze nguvu zetu kwenye sala na maombi ya uponyaji wa haraka, huku tukizidi kuomba Mungu, asimame na familia nzima ya Apiyo, wabarikiwe sana na kuwapa nguvu na uwezo wa kusimama imara katika kipindi hiki kigumu cha kumuuguza Mzee wetu.

  N.B. Mwandishi ni Pascal, Mimi ni Pasco.
   
 19. F

  Future-Tanzania JF-Expert Member

  #19
  Apr 5, 2009
  Joined: Dec 14, 2008
  Messages: 334
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwanini watanzania wasiache watu na familia zao waishi kama watakavyo na sehemu yoyote watakayo?

  Field Marshall ES, mbona anamngangania huyu jamaa awe karibu na baba yake? how do you know he is not? nyie ndio watu mnaochonganisha miji/familia za watu.. sorry if i have touch inner part of some people here.. its just i couldn't stand watu mnavyoongelea familia za watu. nafikiri watu muunze kujua how far to go with respect to other people families
   
 20. Mwawado

  Mwawado JF-Expert Member

  #20
  Apr 5, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 998
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 35
  Mkuu FMES Heshima mbele Mkuu,Nafikiri maneno yako mazito Dr.Apiyo atakuwa ameyasikia,na itakuwa vyema uyaachie hapo,hakuna sababu yoyote ya maendelezo ya kumuomba Dr.Akumbuke nyumbani ,eti kwa sababu Wazazi wamekuwa Wazee ,nina uhakika Dr analijua hilo vizuri kuliko wewe.kumbuka kwamba Mr Apiyo ni baba yake mzazi.

  Mzee Apiyo ni mgonjwa kwa muda mrefu sasa,ni hivi karibuni tu hali yake ya Afya ilizidi kunyongea,labda kwa sababu ya kukumbwa na matatizo ya misiba ya mfululizo na ukizingatia afya na umri wake ni vitu vinavyopelekea magonjwa mengi...

  Mimi kama wewe (FMES) Namfahamu Mzee Apiyo kwa ukaribu...na bila uoga naweza kusema kuwa Serikali imechangia sana matatizo ya maisha ya Mzee Apiyo...Mzee huyu kama walivyo wengine kwenye Utawala wa Mwalimu hawakuwa watu wa kujilimbikizia mali,mara baada ya kustaafu amekuwa mtu wa kuhangaika mpaka hivi karibuni ambapo baadhi ya viongozi wakiongozwa na Waziri Wassira walipomuomba Mzee Kikwete awape msaada viongozi hawa,ikiwa ni pamoja na matibabu na angalau usafiri...sio Apiyo tu wapo wastaafu wengine wawili wanaangaliwa kwa kiwango hicho.

  Tukimtupia lawama Dr.Apiyo tutakuwa tunamuonea,Dr kama vijana wengine waliosomea western Europe hawakuwa na uwezo wa kupata pesa za kuweza ku-support familia nyumbani,hivi sasa baada ya masomo ndio angalau ana uwezo wa kusaidia kwa pesa na ushauri,na anafanya hivyo.Ndugu zetu mnaosoma/fanyakazi huko America na Europe mna uwezo wa kumudu maisha na kutoa msaada nyumbani,hali hiyo si kwa wote.....

  Kamanda FMES. Dr ameupata ujumbe vilivyo, na ni imani yangu atawasiliana nawe...Hivi sasa sote kwa pamoja tukusanye nguvu zetu na kumuombea Mzee apate nafuu ya haraka na arudi nyumbani..
   
Loading...