Time Travel: Je, linaweza kuwa suluhisho la kifo?

"Makarim Shiraz..hasa kwenye Atafsiru Nemuneh Juzuu 6 ukurasa wa 202,,shekh kama hujapita hapo nakuomba kapite ili angalau Uzione nyakati 6 za uumbaji.
Wewe ni SHIA kiitikadi au umeamua tu kufatilia maandiko yake hjyo msomi wa Kishia ?

Nakuuliza swali hili sababu naijua itikadi ya SHIA katika mambo mengi.
 
Kuna haka kastory niliakandika kitambo kidogo ngoja nikaweke hapa ili tusijaze server za watu . haka kastori kanahusu viumbe wanaokuja duniani kutoka anga za mbali kuja kututembelea.. sometime waweza jiuliza tu kwanini Rc ilibadiri sala ya Mwanakondo uondoae dhambi za dunia kua mwanakondoo uondoae dhambi za ulimwengu! ni kwasababu Teknoljia inazidi kukua pia elimu yazidi kupanuka hivyo wakajua tu haiwezekani katika Ghalaxy yetu ya Milky way yenye solar system zaidi ya 1mil kuwe na binaadamu/viumbe duniani tu.
kastory kenyewe ni haka...
View attachment 1102218
Ilikua july 1954 ambapo maofisa wa wa uwanja wa Haneda Airport(kwasasa Tokyo airport) nchini Japan waliripoti tukio la kushangaza lilitokea uwanjani hapo… Msafiri kutoka Ulaya mwenye pasi ya kusafiria ya nchi iliyokua inaitwa Tuared.

Msafiri huyo alikua namwonekano mwenye ndevu kiasi na mwonekano wa Caucusian kama watu wanaotoka nchi za Ulaya, kwa mujibu wake alisema kua nchi hiyo ya Tuared iko ulaya pia alikua ana fedha za mataifa mbalimbali. Maofisa wa polisi walifikiraia kua watakua na maelezo kidogo tu kuhusu kwanini hawajui nchi hiyo ilipo hivyo wakaamua kumpelekea chemba kwa mahojiano zaidi… Walipoanza kumuuliza taarifa iliwapate kuifahamu hio nchi ilipo Yule msafiri alianza kua mkali na kusema kua hiyo ilikua safari yake ya tatu hapo nchini japan kwa safari za kampuni anayofanyia kazi, pia amekua akifanya safari nchini humu kwa muda wa miaka mitano iliyopita. Msafiri alishangaa kwanini maofisa wanachelewa ku-Approve safari yake, lakini maofisa walipoulizia kwenye hiyo kampuni aliyosema ndio anakwenda kikazi walikataa kua hawamfahamu mtu huyo pia hata hiyo kampuni aliyotoka pia maofisa waligundua kua haijawahi kuwepo pia hata hotel aliyosema kafanya Resevation/booking walikaa kua hawamfahamu mtu huyo na hajachukua chumba hapo.

Msafiri huyo alikua anaongea kifaransa, kijapan na lugha nyingine nyingii. Kuongea kwake kijapani kidogo ilikua ni ushahidi kua hua anakuja nchini Japani. Lakini walipomuonyesha ramani ya dunia aonyeshe wapi nchi yake hiyo ya Tuared ilipo alishangaa kua haioni kwenye ramani, akaonyesha sehemu inayoitwa Andorra kua ndiko nchi yake hiyo ilikuwepo. Akasema tured ipo miaka zaidi ya elfu hivyo ingekuwepo kwenye ramani, akahitaji maofisa wamalizane na hilo swala lake aondoke kachoka kukaa kwenye chumba cha mahojiano. Hivyo maofisa uhamiaji wale walimtafutia chumba kwenye hotel iliyopo jirani na uwanja wa ndege, maafisa uhamiaji wawili walipangwa kulinda chumba chake hicho usiku kucha ili kesho yake aendelee kufanyiwa uchunguzi. Asubuhi kulipokucha walikuta Yule msafiri katoweka. Haikujulikana alipitia wapi maana kama ni dirisha la chumba cha hoteli lilikua juu kabisa hotelini pia mtaa ule ulikua bize muda wote hivyo angeonekana dirisha pia lilikua limefungwa. Hadithi ya msafiri huyo inaishia hapo maana hakuonekana tena mpaka leo na hakuna mtu aliyewahi kujua nchi hiyo ya tuared iko wapi japo wanhistoria mbali mbali kutoka japani walijaribu kufuatiia nchi hiyo uwepo wake miaka iliyopita.

Story ya uongo hii, usiamini sana kila kinachoandikwa online utaishia kua ovyo sana kichwani. Hakuna sehemu inaongoza conspiracy theories kama kwenye internet, na sababu zimejaa ni kwa kua story zinapendwa sana so wengi mnafungua page zao zina ads wanaingiza pesa za bure. Story kama hii inaonekana fascinating, millions of view daily mtu anapiga $1,000 kilaini, unadhani ataacha kuendelea kutunga story za uongo?

Grow up, soma, alafu tumia akili, story kama hizi utakua ukisoma kidogo tu huitaji hata kumaliza unagundua kama ni nuksi au la, hakuna evidence yoyote iliyotolewa kwenye story yako, majina feki, identity fake, hakuna proof yoyote ile zaidi ya kuandika ugoro kibao.
 
all in all time travel ili iwezekane lazima uwe na speed kali kuliko ya mwanga,,
hivyo ni impossible kwa time travel kutokea,,hata ikotokea itakuwa umesafiri kwenda past na sio future...........
labda wanasayansi wa CERN wanaweza kuja na jibu kupitia particle accelerator yao............

Si kweli kua utaenda past. Kwenda past haiwezekani, ni impossible, hata theoretically ni impossible siongelei physically tu. Kwenda future inawezekana ndiyo na proof zipo, ila kwenda nyuma ni impossible, what has happened has already happened, time ni abstraction tumetengeneza wenyewe kuexplain phenomena flani in nature ila doesn't mean kua kuna kitu physically kinaitwa time ambacho unaweza manipulate.

Ukitravel kwa speed ya mwanga (which is impossible coz you have mass) ni kama una-exist in all places at the same time, hii haimaanishi umeenda to the past hapana, bali upo in all places at once, the moment unapostop kuobserve there's no way utakua in the past, either the present somewhere else au in the future.

Unavyozunguka close to the speed of light basi time goes slower for u kuliko observer, haimaanishi unaenda past hapana, ila kwako sekunde tano yaweza kua mwaka kwa mwingine. Hii ni possible na proof zipo.

Tusiongelee kuhusu faster than light kwa kua ni impossible, huwezi kua na infinite mass, hii ingewezekana basi ingekua the end of the universe as we know it. Njia pekee ya kucover distance kubwa ni kwa kudistort spacetime, hii nayo ni theoretical japo scientist wanatafuta njia.

Swala la kwenda to the past futa kabisa akilini, ni impossible, stop wasting time with it in your mind, ni possible kwenye movies tu ila science inagoma. Kwenda past ni sawa na kuviolate conservation of energy.
 
Mimi nipo upande wa mwanaadam na bila shaka akili yangu ya kufikiria imewekewa kikomo.na huo ndio udhaifu wangu na bila shaka lazima niyaone baadhi ya mambo yana utata...
Sio akili yako tu bali akili ya mwanadamu yeyote ina ukomo,ndio maana Allah akaleta mitume na ufunuo ili kutufunulia yale ambayo akili zetu haziwezi kuyadiriki.

Lakini kuna ule uchache wa elimu na aina fulani ya kufikiri kulingana na mazingira aliyokulia mtu.

Kwahiyo suala la kuona maandiko fulani yana utata yanabakia katika tatizo lako binafsi na si andiko kwa dhati yake.
Upande wa Allah sw..kwanin nasema hivyo..Wewe umeishahukumu na kufunga mjadala wa kutafakari..na sbb unahisi kua wenye mawazo tofauti na ulichohukumu wana Elimu ndogo...mf umehukumu nukta 2 tulizojadili bila uthibitisho wa aina yoyote.
Katika hili sio sawa,na Mashia wengi huwa nawaona wamejikita sana katika matumizi ya Falsafa na kuwa nukuu wanafalsafa wa kale katika Tafsir zao za Qur'aan na hili limewaathiri sana na kuwafanya wakosee sana katika kuitafsiri Qur'aan kwani huwa wanafata sana rai kuliko dalili. Rejea Tafsiri ya Jawad Mughniya iitwayo al Kashif kama sikosei. Wafatilie wanazuoni wao kaa vile kina Seestani,kina al Khui,kina Murtadha Mutahari,kina Musawi Lari,kina Sadri mwenye kitabu "Falsafatuna" wasome hao utaona namna gani walivyojikita katika Falsafa na kucha dalili za wazi.

Naendelea ......

Kufikiri pia kuna elimu yake,sio unafikiria hovyo hovyo bila mipaka,kwani kufikiri bila mipaka ni utumwa wa kifikra,binadamu mwenye akili lazima afikiria katika hali zote yaani na si kama wanavyofikiria Wanafalsafa na Wakana Mungu wao hufikiri kwa upande mmoja.
 
1,Umehukumu kua mbingu saba zimesimama bila nguzo hali ya kua huna ushahidi wa aina yoyote
Ushahidi uko wazi,tatizo je utaukubali ?

Rejea sura ar Raad aya ya pili.
Na Mtume alipoulizwa kua Umemuona Allah sw jibu lake lilikua ni Nuru.Nuru.Nuru..swali langu ni Wewe umejuaje kua hakumuona kama wewe haupo upande wa mungu..?niwie radhi kwa mara nyingine kama nitakua nimekukwaza ..sikua na nia hio lengo langu ni mjadala uwe na afya na kuongeza maarifa.

Swali rahisi,je alimuona ?

Hiyo sio dalili kuonyesha ya kuwa mtume alimuona Allah sababu "Nuru" ni miongoni mwa majina ya Allah. Rejea aya ya 35 katika surat an Nuur.

Hivi mathalani ukaulizwa umemuona Zurri,ukajibiwa "Zurii Zurri" hapa unapata maana gani ?

Na Allah anajua zaidi.
 
Ya tafiti zote naona wanafanya kusafiri kwenda past but trust me kama ikifanikiwa kwenda past basi itakua so simple kwenda future. Ya inabidi uwe unamwendo mkali kuliko mwanga ili kutengeneza Curveture kwenye Gravity ili kurudisha muda nyuma au kuupeleka mbele
Katika vitu ambavyo vimethibitisha Mimi ni kilaza ni hii time traveling.Mbali na kwamba je inawezekana kutokea hata kuielewa tu nimeshindwa.

Nimesoma Sana kuhusiana na hii kitu plus kuangalia movie Lakini wapi huwa siielewi kabisa.
Mi' mwenyewe mweupeee .....kwa ninachokisoma labda nirudie rudie ndo n'tapata concept....
 
Ushahidi uko wazi,tatizo je utaukubali ?

Rejea sura ar Raad aya ya pili.

Swali rahisi,je alimuona ?

Hiyo sio dalili kuonyesha ya kuwa mtume alimuona Allah sababu "Nuru" ni miongoni mwa majina ya Allah. Rejea aya ya 35 katika surat an Nuur.

Hivi mathalani ukaulizwa umemuona Zurri,ukajibiwa "Zurii Zurri" hapa unapata maana gani ?

Na Allah anajua zaidi.

Shekh Zurr hili nililitarajia na ndio shida kubwa tulip nayo waislam wa zama hizi za Usultan na Ufalme.
1.Wajuaji wasiopenda kujulishwa.
2.Hawajui na hajui kua Hawajui.
3.Kubaguana kati Yao na Sisi.
Ngoja nikupe mawaidha kidogo kuhusu watoto wawili wa baba yetu Adam ..yaani Habil na Kabili.hawa vijana walipewa neema 1 ya mazao na 2 Mifugo..Allah sw akawataka watoe ktk alivyowaneemesha..ukweli wa kimaumbile upo hivi vitu 2 haviwezi kuchukua nafasi 1 kwa pamoja .nilazima kiwepo kinachoanza na kinachofuata.sio lengo langu kuhadithia kisa chote ila nilitaka kukuweka kwenye mstari juu ya maudhui ninayotaka kushae na wewe...Allah sw ampetupanga wanaadam katika makundi matatu
1.Walioruzukiwa Elimu kutoka kwake..(2)
2.Wajinga(2)
3.Wapumbavu...
Labda nikufafanulie Kundi la kwanza lina watu wa aina 2,
1,mitume na manabii
2,watu wema mf.Lukman na Khidhr ambae alikuja kumfundisha Mtume musa subra.sbb kubwa ya nabii mussa kufundishwa na mtu wa kawaida ni jibu lake la kujiaminisha hakuna mtu mwenye elimu kubwa kumzidi yeye katika kipindi chake cha utume..Allah sw ili kumuweka sawa nabii wake akamletea mtu ili amthibitishie yeye si chochote ktk..ujuzi usiomithilika wa enzi yake.
Moja ya kazi ya mitume ni kuwajuza na kuwafundisha umma wao juu ya Subra..mussa alipewa mtihani mdogo wa subra na alishindwa..funzo tunalolipata hapa ni kuwa hata kama umemaliza na umebobea katika fan zote za Elimu bado utakua hujui...
Kundi la pili ni wajinga..nalo limegawanyika Mara 2,
1.wenyekujifunza kwa njia mbalimbali kwa mukhtarha wa kuyafaham mambo na kuyaelewa mambo kinaga ubaga..kundi hili ndio la wafuasi wa mitume na Manabii...
2.wasiotaka kujifunza .kundi hili lipo kama bendera upepo unapoelekea na lenyewe ndiko linakoelekea..wapowapo tu na hawajui kama hawajui.
Kundi la tatu hili ni lawapumbavu...wao wapo tofauti kidogo na kundi la pili na sifa zao kubwa ni hizi.
1,Hujiaminisha kua wanajua kila jambo na ujuzi wao ni gift.kutoka kwa muumba...ila Uhalisia nikwamba hawajui chochote na mtaji wao mkubwa ni Matusi na uzushi wenye maudhi kwa kundi la kwanza na lapili.
Wanajua kua hawajui lakin wanajifanya wanajua hali ya kua wanajijua kua Hawajui.
Kaka yangu zurr nimeamua kushea na wewe maneno haya huenda ukaifungua akili yako na kuiacha huru kutoka kifungoni ulikofungwa..Kitendo chako cha kuniliza natumia tafsiri za wanazuoni wa madhaby gani na kunibainishia Uhaifu na kuzibagaza madhaby nyingine imekuonyesha wazi ulivyo mweupe kama debe tupu katika Bahari ya Maarifa..Utafiti unafunjwa kwa utafiti na huwezi kuwa mpingajipingaji tu bila kua dalili za mashiko na fact zisizo na Shaka..mfano mzuri ni katika nukta ya Uumbaji wa mbingu saba...nimekujuza jambo hili linatatanisha katika mantiki yake ila wewe hulioni unapinga tu bila fact zozote..Tafsiri ya Yusufu ally aya inayozungumzia uumbaji wa mbingu inasema "Ni yeye alieziumba mbingu saba bila kua na nguzo zinazoonekana" mwisho wa kunukuu..maelezo ya aya yameishia hapo yenyewe wala hayatatanishi...kwa wasomi hatuishii hapo ni lazima tufanye utafiti...na utafiti unafanyika ktk Maneno haya"Pasi na nguzo Zisizoonekana" Na happa ndio dhana tatanishi inapojitokeza...
1,Pasi na nguzo...tafsiri ni bila nguzo.
2.Nguzo zisizoonekana.....Nguzo zipo lakini hazionekani.
Hapa utata utaisha pale tu Allah sw atakapomteua mja wake ili aubainishie umma juu ya utata huu...kama alivyoubainisha utata wa Viza vitatu ndani ya tumbo la mjamzito kupitia mashine za Utra Sound...Tuombeane kheri tupo katika kutafuta maarifa na hakuna ajuae yote isipokua Allah sw mjuzi wa kila jambo.
 
thats truee
 
Shekh Zurr hili nililitarajia na ndio shida kubwa tulip nayo waislam wa zama hizi za Usultan na Ufalme
Kwanza kabisa mimi si sheikh na nipo katika kujifunza,maelezo yako nimeyasoma na nimeyaelewa vyema na nina uhakika kila unachokisema unamaanisha.

Na hapa hakuna kufichana lazima tuwekane wazi ili tufahamiane vizuri.

Mwanzo unakumbuka ulimgusia "Makarim Shirazi" ? Nikakuuliza swali wewe ni SHIA au umeamua kumfatilia huyo sheikh wa Kishia bila kujua ?

Muda huu umetaja suala la Ufalme na Usultani,hapa najua kabisa umemaanisha japokuwa hapakuwa na haja ya wewe kuweka kauli hiyo.

Sababu najua umemaanisha na mimi nakuuliza swali je Usultani na Ufalme ni jambo baya ? Je Uislamu unakataza Ufalme ? Kwanini umeiweka kauli hiyo hapa ? Je kulikuwa na haja ?
1.Wajuaji wasiopenda kujulishwa.
2.Hawajui na hajui kua Hawajui.
3.Kubaguana kati Yao na Sisi.

Haya unayoyasema yako sahihi na yapo na tunayaona.
Ngoja nikupe mawaidha kidogo kuhusu watoto wawili wa baba yetu Adam ..yaani Habil na Kabili.hawa vijana walipewa neema 1 ya mazao na 2 Mifugo..Allah sw akawataka watoe ktk alivyowaneemesha..ukweli wa kimaumbile upo hivi vitu 2 haviwezi kuchukua nafasi 1 kwa pamoja .nilazima kiwepo kinachoanza na kinachofuata.sio lengo langu kuhadithia kisa chote ila nilitaka kukuweka kwenye mstari juu ya maudhui ninayotaka kushae na wewe...
Nakupata vizuri. Hivi visa navyovitoa ingekuwa vizuri kama ukiwa unaweka na marejeo,kama unavyonituhumu mimi ya kuwa siweki ushahidi.
Allah sw ampetupanga wanaadam katika makundi matatu
1.Walioruzukiwa Elimu kutoka kwake..(2)
2.Wajinga(2)
3.Wapumbavu...
Labda nikufafanulie Kundi la kwanza lina watu wa aina 2,
1,mitume na manabii
2,watu wema mf.Lukman na Khidhr ambae alikuja kumfundisha Mtume musa subra.sbb kubwa ya nabii mussa kufundishwa na mtu wa kawaida ni jibu lake la kujiaminisha hakuna mtu mwenye elimu kubwa kumzidi yeye katika kipindi chake cha utume..Allah sw ili kumuweka sawa nabii wake akamletea mtu ili amthibitishie yeye si chochote ktk..ujuzi usiomithilika wa enzi yake.
Nakupata vizuri.
Moja ya kazi ya mitume ni kuwajuza na kuwafundisha umma wao juu ya Subra..mussa alipewa mtihani mdogo wa subra na alishindwa..funzo tunalolipata hapa ni kuwa hata kama umemaliza na umebobea katika fan zote za Elimu bado utakua hujui...
Kundi la pili ni wajinga..nalo limegawanyika Mara 2,
1.wenyekujifunza kwa njia mbalimbali kwa mukhtarha wa kuyafaham mambo na kuyaelewa mambo kinaga ubaga..kundi hili ndio la wafuasi wa mitume na Manabii...
2.wasiotaka kujifunza .kundi hili lipo kama bendera upepo unapoelekea na lenyewe ndiko linakoelekea..wapowapo tu na hawajui kama hawajui.
Kundi la tatu hili ni lawapumbavu...wao wapo tofauti kidogo na kundi la pili na sifa zao kubwa ni hizi.
1,Hujiaminisha kua wanajua kila jambo na ujuzi wao ni gift.kutoka kwa muumba...ila Uhalisia nikwamba hawajui chochote na mtaji wao mkubwa ni Matusi na uzushi wenye maudhi kwa
Uko sahihi kabisa.
Wanajua kua hawajui lakin wanajifanya wanajua hali ya kua wanajijua kua Hawajui.
Kaka yangu zurr nimeamua kushea na wewe maneno haya huenda ukaifungua akili yako na kuiacha huru kutoka kifungoni ulikofungwa..Kitendo chako cha kuniliza natumia tafsiri za wanazuoni wa madhaby gani na kunibainishia Uhaifu na kuzibagaza madhaby nyingine imekuonyesha wazi ulivyo mweupe kama debe tupu katika Bahari ya Maarifa..

Kaka elimu haitaki mja uwe kama sponchi lazima uchuje kipi cha kuchukua na kipi cha kuacha. Kama mwanachuoni mkubwa alipata kuathiriwa na mtu muovu vipi mimi ambae sina elimu,unamjua Imaamu Safarini ? Mwenye kitabu kiitwacho "Aqidat as Safariniyyah" ?

Sasa kama leo hii kuna watu wanaitakidi Jibril alifanya hiyana juu ya kupeleka ujumbe kwa mtume na alipaswa apelekewe Ali,huku ni kuitukana dini ya Uislamu,mtu ambae anasema mama Aisha ni mzinifu wakati Qur'aan imewatakasa wakeze mtume,na mtu ambae anaitakidi ya kuwa Qur'aan haijakamilikana iliyokamilika iko pangoni ? Hivi mtu huyu atakueleza nini katila Dini akawa mkweli ?

Kaka ukisoma katika kitabu cha Mukadima wa Sahihi Muslimu cha Imam Muslim ameelzea maneno ya Imamu Muhammad bin Sirrin akionyesha umuhimu wa kuwajua rijali katika mapokezi ya habari anazo nasibishwa nazo mtume,na hii ni baada ya kudhihiri fitna na akasema ya kuwa kuuliza juu sanadi ndio dini basi tuangalie wapi unachukua dini yako.

Mtume ameondoka ameacha Uislamu ukiwa safi na usiku wake ni sawa na mchana wake. Kaka siwezi kuchukua dini lwa mtu mzushi na muongo kama Jahmiyyah,Ashaira,Mu'tazila ambao wapo karibu sana kiitikadi na MASHIA,Maturudiya na wengineo katika makundi potofu.

Kaka bora wewe unione mimi sina maarifa ila sitaki kuichanganya Itikadi yangu na uchafu.
Utafiti unafunjwa kwa utafiti na huwezi kuwa mpingajipingaji tu bila kua dalili za mashiko na fact zisizo na Shaka..mfano mzuri ni katika nukta ya Uumbaji wa mbingu saba...nimekujuza jambo hili linatatanisha katika mantiki yake ila wewe hulioni unapinga tu bila fact zozote..

Kuna muda nilikugusia athari walizokuwa nazo wanazuoni wa dini ya USHIA kutokana na wao kujikita na Falsafa ikawapelekea kukana baadhi ya sifa za Allah.

Nakuuliza swali,hivi Qur'aan ni maneno ya Allah au ni kiumbe ?

Pili,utata uko wapi wakati jambo hili limeshawekwa wazi karne na karne na wanazuoi wa Tafsiri ? Ndio maana nilikuuliza unatumia tafsiri gani ? Sababu nilijua tu kama wewe sio SHIA basi umeathirika na USHIA. Sasa wewe si unasema au unahimiza juu ya utafiti,je ushawahi kusoma Tafsiri za Qur'aan nje ya Tafsiri za Kishia ? Na kama umesoma ni tafsiri zipi umesoma ? na kama hujasoma kwanini mimi unataka niwe huru wakati wewe hauko huru ?

Sasa,nenda kasome Tafsiri ya Imaam Ibn Kathiir iitwayo "Al Qur'aan Adhwiim" katika kuilezea aya hiyo ya pili ya surt ar Raadi,uone je hiyoaya ina utata au utata mnauweka nyinyi ?

Kaka kwanza ulitakiwa ujue ni kwa namna gani wanazuoni walivyopambana kwa idhni ya Allah juu ya kuihudumia Qur'aan na kuweka wazi aya zote zinazohisiwa na watu kwamba zina utata,rejea pia kitabu cha Imaamu Muhammad al Amiin ash Shanwitwiy kiitwacho"Dafu'u Ihami adh Twirab 'an Ayaat al Kitaab" pia rejea kitabu cha Mwanachuoni mkubwa wa Hadithi aitwae Abdul Muhsin al Abaad al Badr kiiteacho "Ayaat mutashabihaat al Alfadh fi Qur'aan al Kariim" na namna ya kuzitofautisha. Ili uone ya kuwa kila kitu kilishawekwa wazi muda mrefu na mnayoyaleta nyinyi ni Talbisat za kuwayumbisja watu kwa makusudi wakati mambo yako wazi na dalili ziko wazi ila hamzifati kwa makusudi.
Tafsiri ya Yusufu ally aya inayozungumzia uumbaji wa mbingu inasema "Ni yeye alieziumba mbingu saba bila kua na nguzo zinazoonekana" mwisho wa kunukuu..
Ile ya Ysuf Ali sio Tafsir,bali ni tarjama kwa lugha ya kiingereza,tafuta Tafsir za wanazuoni wakubwa ambao wamejea maana ya aya kwa mtume na maswahaba zake. Aya hizo zimewekwa wazi. Na hapo Yusif Ali hajatafsiri bali matini ya aya ndio yanasema hivyo.
kwa wasomi hatuishii hapo ni lazima tufanye utafiti...na utafiti unafanyika ktk Maneno haya"Pasi na nguzo Zisizoonekana" Na happa ndio dhana tatanishi inapojitokeza...
1,Pasi na nguzo...tafsiri ni bila nguzo.
2.Nguzo zisizoonekana.....Nguzo zipo lakini

Nakuuliza swali rahisi,sasa wewe baada ya kuona aya na ukadai kwamba ina utata,je ni wewe umeliona hilo au wanazuoni wako wameliona hilo ndio wewe ukakariri ?

Je baada ya kuhisi utata huo je ulisoma vitabu vya madhehebu ngapi za Uislamu juu ya aya hiyo na madhehebu hizo zimesema kwamba aya hiyo ina utata au ?

Je kabla ya wanazuoni wako je maimamu gani wa Kishia kati ya wale 12 walisema kwamba aya hiyo ina utata ? Je kama hakuna,wewe na maimamu wa Kishia nani mwenye elimu kubwa ?

Unajua kuna ujinga mwingine huwa mnajitakia tu,muonekane mnajua kuhoji wakati mnapotea,rudini katika asili kila kitu kipo.
Hapa utata utaisha pale tu Allah sw atakapomteua mja wake ili aubainishie umma juu ya utata huu...
Sababu nimeshakujua wewe ni nani kiitikadi,nakuuliza maswali kulingana na maelezo yako,je ina maana mpaka muda huu Allah hajamteua huyo mja wa kutoa huo utata ? Na kama bado wewe umejuaje hilo na unahisi huyo mja ni nani ? Al Mahdi au ? Jamaa acheni kudanganya watu,mtakuja kuulizwa kwa huu ujinga mnaoufanya mwa kuitukanisha dini ya Allah.
kama alivyoubainisha utata wa Viza vitatu ndani ya tumbo la mjamzito kupitia mashine za Utra Sound...Tuombeane kheri tupo katika kutafuta maarifa na hakuna ajuae yote isipokua Allah sw mjuzi wa kila jambo.

Hivi hata unachokiandika huwa unakihakiki ?

Kaka katika maelezo yangu humu nimekuuliza maswali kadhaa,naomba unijibu maswali yangu yote niliyokuuliza.

Pili,marejeo yote niliyokupa naomba ukayafatilie na uyasime kikamilifu.

Ninacho kukumbusha ni kuwa dini ya UISLAMU imekamilika na USHIA sio Uislamu bali ni dini pweke inayojitegemea na hakuna hata ibada moja ya kishia inayo fanana na ya Uislamu.

Kama kuna lolote nililokosea ni kwa udhaifu wangu na Allah aliye juu ametakasika na ukamilifu ni wake yeye.
 
Story ya uongo hii, usiamini sana kila kinachoandikwa online utaishia kua ovyo sana kichwani. Hakuna sehemu inaongoza conspiracy theories kama kwenye internet, na sababu zimejaa ni kwa kua story zinapendwa sana so wengi mnafungua page zao zina ads wanaingiza pesa za bure. Story kama hii inaonekana fascinating, millions of view daily mtu anapiga $1,000 kilaini, unadhani ataacha kuendelea kutunga story za uongo?

Grow up, soma, alafu tumia akili, story kama hizi utakua ukisoma kidogo tu huitaji hata kumaliza unagundua kama ni nuksi au la, hakuna evidence yoyote iliyotolewa kwenye story yako, majina feki, identity fake, hakuna proof yoyote ile zaidi ya kuandika ugoro kibao.
Nitaaminije kua ni ya uongo kisa wewe umeniambia?
 
Kwanza kabisa mimi si sheikh na nipo katika kujifunza,maelezo yako nimeyasoma na nimeyaelewa vyema na nina uhakika kila unachokisema unamaanisha.

Na hapa hakuna kufichana lazima tuwekane wazi ili tufahamiane vizuri.

Mwanzo unakumbuka ulimgusia "Makarim Shirazi" ? Nikakuuliza swali wewe ni SHIA au umeamua kumfatilia huyo sheikh wa Kishia bila kujua ?

Muda huu umetaja suala la Ufalme na Usultani,hapa najua kabisa umemaanisha japokuwa hapakuwa na haja ya wewe kuweka kauli hiyo.

Sababu najua umemaanisha na mimi nakuuliza swali je Usultani na Ufalme ni jambo baya ? Je Uislamu unakataza Ufalme ? Kwanini umeiweka kauli hiyo hapa ? Je kulikuwa na haja ?

Haya unayoyasema yako sahihi na yapo na tunayaona.

Nakupata vizuri. Hivi visa navyovitoa ingekuwa vizuri kama ukiwa unaweka na marejeo,kama unavyonituhumu mimi ya kuwa siweki ushahidi.

Nakupata vizuri.

Uko sahihi kabisa.

Kaka elimu haitaki mja uwe kama sponchi lazima uchuje kipi cha kuchukua na kipi cha kuacha. Kama mwanachuoni mkubwa alipata kuathiriwa na mtu muovu vipi mimi ambae sina elimu,unamjua Imaamu Safarini ? Mwenye kitabu kiitwacho "Aqidat as Safariniyyah" ?

Sasa kama leo hii kuna watu wanaitakidi Jibril alifanya hiyana juu ya kupeleka ujumbe kwa mtume na alipaswa apelekewe Ali,huku ni kuitukana dini ya Uislamu,mtu ambae anasema mama Aisha ni mzinifu wakati Qur'aan imewatakasa wakeze mtume,na mtu ambae anaitakidi ya kuwa Qur'aan haijakamilikana iliyokamilika iko pangoni ? Hivi mtu huyu atakueleza nini katila Dini akawa mkweli ?

Kaka ukisoma katika kitabu cha Mukadima wa Sahihi Muslimu cha Imam Muslim ameelzea maneno ya Imamu Muhammad bin Sirrin akionyesha umuhimu wa kuwajua rijali katika mapokezi ya habari anazo nasibishwa nazo mtume,na hii ni baada ya kudhihiri fitna na akasema ya kuwa kuuliza juu sanadi ndio dini basi tuangalie wapi unachukua dini yako.

Mtume ameondoka ameacha Uislamu ukiwa safi na usiku wake ni sawa na mchana wake. Kaka siwezi kuchukua dini lwa mtu mzushi na muongo kama Jahmiyyah,Ashaira,Mu'tazila ambao wapo karibu sana kiitikadi na MASHIA,Maturudiya na wengineo katika makundi potofu.

Kaka bora wewe unione mimi sina maarifa ila sitaki kuichanganya Itikadi yangu na uchafu.

Kuna muda nilikugusia athari walizokuwa nazo wanazuoni wa dini ya USHIA kutokana na wao kujikita na Falsafa ikawapelekea kukana baadhi ya sifa za Allah.

Nakuuliza swali,hivi Qur'aan ni maneno ya Allah au ni kiumbe ?

Pili,utata uko wapi wakati jambo hili limeshawekwa wazi karne na karne na wanazuoi wa Tafsiri ? Ndio maana nilikuuliza unatumia tafsiri gani ? Sababu nilijua tu kama wewe sio SHIA basi umeathirika na USHIA. Sasa wewe si unasema au unahimiza juu ya utafiti,je ushawahi kusoma Tafsiri za Qur'aan nje ya Tafsiri za Kishia ? Na kama umesoma ni tafsiri zipi umesoma ? na kama hujasoma kwanini mimi unataka niwe huru wakati wewe hauko huru ?

Sasa,nenda kasome Tafsiri ya Imaam Ibn Kathiir iitwayo "Al Qur'aan Adhwiim" katika kuilezea aya hiyo ya pili ya surt ar Raadi,uone je hiyoaya ina utata au utata mnauweka nyinyi ?

Kaka kwanza ulitakiwa ujue ni kwa namna gani wanazuoni walivyopambana kwa idhni ya Allah juu ya kuihudumia Qur'aan na kuweka wazi aya zote zinazohisiwa na watu kwamba zina utata,rejea pia kitabu cha Imaamu Muhammad al Amiin ash Shanwitwiy kiitwacho"Dafu'u Ihami adh Twirab 'an Ayaat al Kitaab" pia rejea kitabu cha Mwanachuoni mkubwa wa Hadithi aitwae Abdul Muhsin al Abaad al Badr kiiteacho "Ayaat mutashabihaat al Alfadh fi Qur'aan al Kariim" na namna ya kuzitofautisha. Ili uone ya kuwa kila kitu kilishawekwa wazi muda mrefu na mnayoyaleta nyinyi ni Talbisat za kuwayumbisja watu kwa makusudi wakati mambo yako wazi na dalili ziko wazi ila hamzifati kwa makusudi.

Ile ya Ysuf Ali sio Tafsir,bali ni tarjama kwa lugha ya kiingereza,tafuta Tafsir za wanazuoni wakubwa ambao wamejea maana ya aya kwa mtume na maswahaba zake. Aya hizo zimewekwa wazi. Na hapo Yusif Ali hajatafsiri bali matini ya aya ndio yanasema hivyo.

Nakuuliza swali rahisi,sasa wewe baada ya kuona aya na ukadai kwamba ina utata,je ni wewe umeliona hilo au wanazuoni wako wameliona hilo ndio wewe ukakariri ?

Je baada ya kuhisi utata huo je ulisoma vitabu vya madhehebu ngapi za Uislamu juu ya aya hiyo na madhehebu hizo zimesema kwamba aya hiyo ina utata au ?

Je kabla ya wanazuoni wako je maimamu gani wa Kishia kati ya wale 12 walisema kwamba aya hiyo ina utata ? Je kama hakuna,wewe na maimamu wa Kishia nani mwenye elimu kubwa ?

Unajua kuna ujinga mwingine huwa mnajitakia tu,muonekane mnajua kuhoji wakati mnapotea,rudini katika asili kila kitu kipo.

Sababu nimeshakujua wewe ni nani kiitikadi,nakuuliza maswali kulingana na maelezo yako,je ina maana mpaka muda huu Allah hajamteua huyo mja wa kutoa huo utata ? Na kama bado wewe umejuaje hilo na unahisi huyo mja ni nani ? Al Mahdi au ? Jamaa acheni kudanganya watu,mtakuja kuulizwa kwa huu ujinga mnaoufanya mwa kuitukanisha dini ya Allah.

Hivi hata unachokiandika huwa unakihakiki ?

Kaka katika maelezo yangu humu nimekuuliza maswali kadhaa,naomba unijibu maswali yangu yote niliyokuuliza.

Pili,marejeo yote niliyokupa naomba ukayafatilie na uyasime kikamilifu.

Ninacho kukumbusha ni kuwa dini ya UISLAMU imekamilika na USHIA sio Uislamu bali ni dini pweke inayojitegemea na hakuna hata ibada moja ya kishia inayo fanana na ya Uislamu.

Kama kuna lolote nililokosea ni kwa udhaifu wangu na Allah aliye juu ametakasika na ukamilifu ni wake yeye.

Nemekuelewa wala sintoongeza chochote.mjadala wetu nimeufunga..na sababu .
1,Sijadili haki kwa Ujinga.
2.Uislam ni haki.Kila MTU atalipwa kwa nia yake
3.Kuijadili haki kwa fitna.Abadan aslan sintokuja kulifanya jambo hilo.
4,Nalijua lengo la mimi kuwepo ktk uso wa ardhi.Sijaja Kumtukana au kumkufurisha mtu kwa sbb ya Anachokiamin
5.Walla tazzru wazratu wizra Ughra"...Wama kunna Muadhibina hataa Nabaatha Rassullah"..Ni juu yako kuamua kama unadhani "Mashekh wako watabeba madhambi yako kwa Kusambaza Fitna zao".Ewallah endelea.
Ushauri wangu ..Makosa ya Mababu zako haifai kuwarithisha Wanao Kama wewe Sio "Mpumbavu"
 
Story ya uongo hii, usiamini sana kila kinachoandikwa online utaishia kua ovyo sana kichwani. Hakuna sehemu inaongoza conspiracy theories kama kwenye internet, na sababu zimejaa ni kwa kua story zinapendwa sana so wengi mnafungua page zao zina ads wanaingiza pesa za bure. Story kama hii inaonekana fascinating, millions of view daily mtu anapiga $1,000 kilaini, unadhani ataacha kuendelea kutunga story za uongo?

Grow up, soma, alafu tumia akili, story kama hizi utakua ukisoma kidogo tu huitaji hata kumaliza unagundua kama ni nuksi au la, hakuna evidence yoyote iliyotolewa kwenye story yako, majina feki, identity fake, hakuna proof yoyote ile zaidi ya kuandika ugoro kibao.
View attachment 1102207
SALUTE
Mara nyingi hua nasema vitu tunavyoona ni vyakijinga havi-make sense machoni na masikioni mwetu ndio hua na maana na vimeleta mabadiriko makubwa duniani kwetu. Mfano swali la kijinga zaidi alilowahi kujiuliza mwanasayans Issac Newton leo hii limetulitea mabadiriko na maendeleo kwenye maisha , hebu fikiria kama leo hii isac newton angekuuliza kwanini apple limemuangukia kichwani halikwenda juu ungemuona vipi? Hilo swali unaloliona la kijinga limeleta maendeleo makubwa sana. Pia ndoto moja aliyoota albert Einstein waweza kuona ni ya kawaida sana au haina maana lakini ni moja kati ya ndoto iliyoleta mafanikio makubwa duniani, kupitia ndoto tu ya kawaida sana aliyoota tulipata kitu kinachoitwa Theory of Ralativity mambo ya Emc2 yote yote unaweza ona ni kitu cha kawaida ila kina impact kubwa kwenye tasnia ya sayansi

Tarehe 11/5/2019 nilibahatika kuangalia muvi hii inayoitwa Avangers: Endgame, content iliyomo kwenye muvi hii ni Time Traveling, baada ya kuangalia muvi I really admitted that Death might no longer a threat to Mankind!.. Baada ya thanos ku-wipe nusu binaadamu wote ulimwenguni (Universe) , njia pekee iliyobakia kutimka ili kuwarudisha wale waliopotea. Probably Human can stop his Destiny which is Death, Nawaza tu labda Binaadamu twaweza kukiepuka na kukizuia kifo kwa kutumia Theory ya Time Traveling.

Time Travel ni nini..?

Ni kitendo cha kusafiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine ndani ya muda, namaanisha kua mtu anaweza kusafiri leo hii kwenda miaka 5,10,20,25 nk ijayo (Future) au kusafiri kurudi miaka 10,20,30,40,nk iliyopita (Past). Hadithi nyingi za zamani zimekua zikielezea swala hili la kusafiri katika muda.

Huko India kuna hadithi inamzungumzia mfale Raivata Kakudumi ambae alisafiri kwenda mbinguni kukutana na mung wake Brahma, aliporudi alishangaa kua ni miaka mingi imepita. Japan pia kuna hadithi inaitwa Nihongi, inamwelezea kijana mmoja mvuvi anayeitwa Urashima taro ambae alitembelea sehemu iliyochini ya maji, baada ya siku tatu alirudi kijijini kwake akakuta ni miaka 300 imepita, alikuta familia yake imefariki yote. Pia kwa wayahudi mnamo karne ya 1BC mwanafunzi aitwae Honi ha-M'agel inasemekana ailisinzia kwa muda wa miaka 27 alipoamka alikuta hakuna mtu aliyemjua sehemu aliyokua anaishi. Na simulizi nyingii sana kuhusu hii nadharia zimetolewa waweza tafuta ukasoma zaidi.

Wakati watu wengi wakidhani kua muda hautofautiani lakini Mwanasayansi Albert Einstein anaelezea kua muda (Time) haupo hivyo wanavyodhani, unaweza kutofautiana kwa mazingira tofauti, kutegemeana na kasi unayotembea nayo angani (in space)…Theory of special relative ya Enstein inasema kua muda kwenda haraka au kwenda taratibu inategemea na kasii unavyo safiri, mtu akisafiri kwa kasi ya mwanga kwa chombo cha anga angani umri wake utakua mdogo kulinganisha na ndugu au wazazi wake aliowaacha angani..kama akirudi yeye atakua kijana lakini nduguze watakua wamezeeka au wakawa wameshafariki.

Pia kwenye theory ya Albert Einstein ya Theory of General relativity anaelezea kua Garvity (kani ya uvutano) inaweza kupeleka muda mbele au kurudisha nyuma. Anaeleza kua chombo cha anaga kikiwa huko anagani kikakutana na kani ya uvutano basi hua kani hiyo husababisha muda kua slow, hivyo basi hata wanasayansi wa anaga wanakubali kua wasafiri wa anga wanaporudi duniani hua wapo nyuma kimuda yaani saa ya duniani inakua mbele kwa muda microsecond 38 kwa siku. Wanahitimisha kwa kusema mfano msafiri mmoja wa anaga ana pacha wake duniani ammbae hafu akikaa huko angani labda siku 14, Yule pacha aliyebaki duniani atamshinda kwa muda wa microsecond 532 (chukua Microsecond 38 zidisha siku 14)

TIME MACHINE

Ili kufanikisha kusafiri katika muda inabidi kuwe na kifaa kinachoiitwa Time machine ambacho hichi kifaa kinauwezo wa kupeleka muda mbele au kurudisha muda nyuma. Bado wanasayansi wanalifanyia kazi suala hili, muda sio mrefu inaweza kuthibishwa kua Time machine inaweza kuanza kufanya kazi. Jinsi Nadharia ya Time Machine inavyofanya kazi kiukweli inanishinda kuielezea kwa Kiswahili kutokana na Ambiguity ya lugha yetu hii. Humo ni masuala ya physics tu so nashindwa niwekeje kwa lugha yetu labda aliyesoma hii kitu akaelewa inavyofanya kazi atatuelezea lifecoded.

Kwenye hili suala la tme Travel kuna kitu kinaitwa Grandfather Paradox ambapo hiki ni kitendo ambacho Time Traveller anarudi kwenye wakati uliopita kisha anaua wazazi wake au babu zake ili yeye awe hakuzaliwa.Kwa mujibu wa wanasayansi na wanafalasafa kama Plato kwenye theory yake ya Platonism anasema kua kubadili maisha yako ya nyuma hakuwezi kuathiri maisha yako ya sasa, lakini mambo yote hayo mawili yanakuja kupingwa na nadharia ya Butterfly Effectt ambapo inasema kua mabadiriko kidogo kwenye sehemu moja yanaweza kuleta mabadiriko makubwa au utofauti mkubwa baadae katika sehemu nyingine

Hii inamaanisha kwamba kama time traveler akirudi katika maisha yaliyopita akamuua baba aua babu yake anaweza sababisha mabadiriko katika maisha yake aliyotoka au future yake.

Kwa muhtsari huu kuhusu theory ya Time Traveling iko hivo japo watafiti wengi wanasema Time Travel hauwezekani iko too theoretically ila mimi naona hiki kitu ni real kabisa kipo, kwanini? Unajua binaadamu hawezi kufikiri nje ya vitu ambavyo vipo duniani nikimaanisha kua hata mimi au wewe hatuwezi kuwaza au kufikiri nje ya vile vitu tulivyoviona,kuambiwa au viliwahi kuwepo. Utawaza Mungu kwakua ulisikia kua kuna Mungu, utawaza nyumba kwakua ushaiona nyumba nk nk. Mantiki yangu ni kwamba hata hao watu wanaosema time travel is real hawakukaa tu wakafikiri kitu amabacho hakipo, mtazamo wangu naamini hiki kitu kipo na kinafanya kazi labda kwa siri kumbuka hata Internet tunaambiwa imeletwa mwaka 1991 na Tim Berners lee lakini ni kitu kipo toka miaka ya 1950s sema Tim aliifanya kua Popular baada ya kutengeneza World Wide Web…

Lakini haya ni mawazo yangu tu kwamba labada kama Time Machine ikifanikiwa kutengenezwa watu wanaweza kuitumia kukwepa kifo labda kwa kurudisha muda nyuma na kukwepa kile kitu kilichopelekea kufariki..kwa mafano kwenye muvi inaitwa Time Trveler’s wife wameelezea tukio hili linavyoweza kufanyika.
~Da'vinci..
Hii Mada ni Kati ya Mada nzuri kuzisoma humu JF. Ina kufanya kufikiri kwa mapana, ina uvumbuzi mkubwa ndani yake. Kuna baadhi humu wanakosoa kuwa time travel no illusion bila scientific proof. Ni vyema tukajiongeza kuliko kupinga kila kitu.
Huwa ninaamini USICHOKIJUA NI MWISHO WAKO WA KUFIKIRI!
 
Nemekuelewa wala sintoongeza chochote.mjadala wetu nimeufunga..na sababu .
1,Sijadili haki kwa Ujinga.
2.Uislam ni haki.Kila MTU atalipwa kwa nia yake
3.Kuijadili haki kwa fitna.Abadan aslan sintokuja kulifanya jambo hilo.
4,Nalijua lengo la mimi kuwepo ktk uso wa ardhi.Sijaja Kumtukana au kumkufurisha mtu kwa sbb ya Anachokiamin
5.Walla tazzru wazratu wizra Ughra"...Wama kunna Muadhibina hataa Nabaatha Rassullah"..Ni juu yako kuamua kama unadhani "Mashekh wako watabeba madhambi yako kwa Kusambaza Fitna zao".Ewallah endelea.
Ushauri wangu ..Makosa ya Mababu zako haifai kuwarithisha Wanao Kama wewe Sio "Mpumbavu"
Una deni la maswali yangu,ila uache uzushi na talbisaat.

Jambo lingine ni makosa kuandika matini ya Qur'aan kwa lugha nyingine kwani unapoteza maana na kukengeusha matamshi,bora ungeweka tarjama ingekuwa bora zaidi.

Hii dini iko wazi na imekamilika,naona umeona nimegusa penyewe.

Nyinyi MASHIA ndio mnaufanya Uislamu utukanwe na uonakane wa ajabu,ila siku zote haki huwa iko juu na hakuna kilicho juu ya haki.

NIMEMALIZA.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom