Time Traveling: Je, linaweza kuwa suluhisho la kifo?

Da'Vinci

Da'Vinci

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2016
Messages
21,074
Points
2,000
Da'Vinci

Da'Vinci

JF-Expert Member
Joined Dec 1, 2016
21,074 2,000
hqdefault-1-jpg.1102207

SALUTE
Mara nyingi hua nasema vitu tunavyoona ni vyakijinga havi-make sense machoni na masikioni mwetu ndio hua na maana na vimeleta mabadiriko makubwa duniani kwetu. Mfano swali la kijinga zaidi alilowahi kujiuliza mwanasayans Issac Newton leo hii limetulitea mabadiriko na maendeleo kwenye maisha , hebu fikiria kama leo hii isac newton angekuuliza kwanini apple limemuangukia kichwani halikwenda juu ungemuona vipi? Hilo swali unaloliona la kijinga limeleta maendeleo makubwa sana. Pia ndoto moja aliyoota albert Einstein waweza kuona ni ya kawaida sana au haina maana lakini ni moja kati ya ndoto iliyoleta mafanikio makubwa duniani, kupitia ndoto tu ya kawaida sana aliyoota tulipata kitu kinachoitwa Theory of Ralativity mambo ya Emc2 yote yote unaweza ona ni kitu cha kawaida ila kina impact kubwa kwenye tasnia ya sayansi

Tarehe 11/5/2019 nilibahatika kuangalia muvi hii inayoitwa Avangers: Endgame, content iliyomo kwenye muvi hii ni Time Traveling, baada ya kuangalia muvi I really admitted that Death might no longer a threat to Mankind!.. Baada ya thanos ku-wipe nusu binaadamu wote ulimwenguni (Universe) , njia pekee iliyobakia kutimka ili kuwarudisha wale waliopotea. Probably Human can stop his Destiny which is Death, Nawaza tu labda Binaadamu twaweza kukiepuka na kukizuia kifo kwa kutumia Theory ya Time Traveling.

Time Travel ni nini..?

Ni kitendo cha kusafiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine ndani ya muda, namaanisha kua mtu anaweza kusafiri leo hii kwenda miaka 5,10,20,25 nk ijayo (Future) au kusafiri kurudi miaka 10,20,30,40,nk iliyopita (Past). Hadithi nyingi za zamani zimekua zikielezea swala hili la kusafiri katika muda.

Huko India kuna hadithi inamzungumzia mfale Raivata Kakudumi ambae alisafiri kwenda mbinguni kukutana na mung wake Brahma, aliporudi alishangaa kua ni miaka mingi imepita. Japan pia kuna hadithi inaitwa Nihongi, inamwelezea kijana mmoja mvuvi anayeitwa Urashima taro ambae alitembelea sehemu iliyochini ya maji, baada ya siku tatu alirudi kijijini kwake akakuta ni miaka 300 imepita, alikuta familia yake imefariki yote. Pia kwa wayahudi mnamo karne ya 1BC mwanafunzi aitwae Honi ha-M'agel inasemekana ailisinzia kwa muda wa miaka 27 alipoamka alikuta hakuna mtu aliyemjua sehemu aliyokua anaishi. Na simulizi nyingii sana kuhusu hii nadharia zimetolewa waweza tafuta ukasoma zaidi.

Wakati watu wengi wakidhani kua muda hautofautiani lakini Mwanasayansi Albert Einstein anaelezea kua muda (Time) haupo hivyo wanavyodhani, unaweza kutofautiana kwa mazingira tofauti, kutegemeana na kasi unayotembea nayo angani (in space)…Theory of special relative ya Enstein inasema kua muda kwenda haraka au kwenda taratibu inategemea na kasii unavyo safiri, mtu akisafiri kwa kasi ya mwanga kwa chombo cha anga angani umri wake utakua mdogo kulinganisha na ndugu au wazazi wake aliowaacha angani..kama akirudi yeye atakua kijana lakini nduguze watakua wamezeeka au wakawa wameshafariki.

Pia kwenye theory ya Albert Einstein ya Theory of General relativity anaelezea kua Garvity (kani ya uvutano) inaweza kupeleka muda mbele au kurudisha nyuma. Anaeleza kua chombo cha anaga kikiwa huko anagani kikakutana na kani ya uvutano basi hua kani hiyo husababisha muda kua slow, hivyo basi hata wanasayansi wa anaga wanakubali kua wasafiri wa anga wanaporudi duniani hua wapo nyuma kimuda yaani saa ya duniani inakua mbele kwa muda microsecond 38 kwa siku. Wanahitimisha kwa kusema mfano msafiri mmoja wa anaga ana pacha wake duniani ammbae hafu akikaa huko angani labda siku 14, Yule pacha aliyebaki duniani atamshinda kwa muda wa microsecond 532 (chukua Microsecond 38 zidisha siku 14)TIME MACHINE

Ili kufanikisha kusafiri katika muda inabidi kuwe na kifaa kinachoiitwa Time machine ambacho hichi kifaa kinauwezo wa kupeleka muda mbele au kurudisha muda nyuma. Bado wanasayansi wanalifanyia kazi suala hili, muda sio mrefu inaweza kuthibishwa kua Time machine inaweza kuanza kufanya kazi. Jinsi Nadharia ya Time Machine inavyofanya kazi kiukweli inanishinda kuielezea kwa Kiswahili kutokana na Ambiguity ya lugha yetu hii. Humo ni masuala ya physics tu so nashindwa niwekeje kwa lugha yetu labda aliyesoma hii kitu akaelewa inavyofanya kazi atatuelezea lifecoded.

Kwenye hili suala la tme Travel kuna kitu kinaitwa Grandfather Paradox ambapo hiki ni kitendo ambacho Time Traveller anarudi kwenye wakati uliopita kisha anaua wazazi wake au babu zake ili yeye awe hakuzaliwa.Kwa mujibu wa wanasayansi na wanafalasafa kama Plato kwenye theory yake ya Platonism anasema kua kubadili maisha yako ya nyuma hakuwezi kuathiri maisha yako ya sasa, lakini mambo yote hayo mawili yanakuja kupingwa na nadharia ya Butterfly Effectt ambapo inasema kua mabadiriko kidogo kwenye sehemu moja yanaweza kuleta mabadiriko makubwa au utofauti mkubwa baadae katika sehemu nyingine

Hii inamaanisha kwamba kama time traveler akirudi katika maisha yaliyopita akamuua baba aua babu yake anaweza sababisha mabadiriko katika maisha yake aliyotoka au future yake.

Kwa muhtsari huu kuhusu theory ya Time Traveling iko hivo japo watafiti wengi wanasema Time Travel hauwezekani iko too theoretically ila mimi naona hiki kitu ni real kabisa kipo, kwanini? Unajua binaadamu hawezi kufikiri nje ya vitu ambavyo vipo duniani nikimaanisha kua hata mimi au wewe hatuwezi kuwaza au kufikiri nje ya vile vitu tulivyoviona,kuambiwa au viliwahi kuwepo. Utawaza Mungu kwakua ulisikia kua kuna Mungu, utawaza nyumba kwakua ushaiona nyumba nk nk. Mantiki yangu ni kwamba hata hao watu wanaosema time travel is real hawakukaa tu wakafikiri kitu amabacho hakipo, mtazamo wangu naamini hiki kitu kipo na kinafanya kazi labda kwa siri kumbuka hata Internet tunaambiwa imeletwa mwaka 1991 na Tim Berners lee lakini ni kitu kipo toka miaka ya 1950s sema Tim aliifanya kua Popular baada ya kutengeneza World Wide Web…

Lakini haya ni mawazo yangu tu kwamba labada kama Time Machine ikifanikiwa kutengenezwa watu wanaweza kuitumia kukwepa kifo labda kwa kurudisha muda nyuma na kukwepa kile kitu kilichopelekea kufariki..kwa mafano kwenye muvi inaitwa Time Trveler’s wife wameelezea tukio hili linavyoweza kufanyika.
~Da'vinci..
 
Waterbender

Waterbender

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2018
Messages
287
Points
225
Waterbender

Waterbender

JF-Expert Member
Joined Oct 2, 2018
287 225
Kama black hole inakaataa hata mwanga kupitaa iwe mtu
 
Secret Star

Secret Star

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2011
Messages
1,518
Points
2,000
Secret Star

Secret Star

JF-Expert Member
Joined Jul 1, 2011
1,518 2,000
Kuna mambo mengi yanafikirisha sana kwa mfano:
Ukisafiri kwa kasi ya mara nne ya kasi ya mwanga kwa sekunde moja
Kasi ya mwanga 300,000km × 4 = 1,200,000 kwa sekund moja

Sekunde 125 × 1,200,000 = 150,000,000 kilometa utaondoka inje ya mifumo wa jua na kuanzia hapo ukitafta muda wa kusafiri kwa sekunde moja inje ya mfumo wa ni miaka ya nuru 1,200,000 kama utaongeza muda wa sekunde 125 × 1,200,000 kwenda na kurudi katika mfumo wa nyota ya jua ni sawa na miaka 150,000,000 ya nuru.
Na utaanza sekunde 125 za kuitafta dunia ambapo hesabu kamili ya muda wako halisi itakuwa mbele kwa miaka 150,000,000 na sekunde mia mbili na hamsin (250) kama umeondoka duniani na umri wa miaka 30 utarudi duniani na miaka 30 na sekunde 375 ila muda wa Duniani utakuwa mbele yako kwa miaka 150,000,000 na sekunde 250 kila ulicho kiacha hautakikuta utaikuta dunia mpya kama utaishi kwa kufanya hivyo huenda ikakuchukua mabilioni ya miaka kufika muda wa kuhisi njaa.
kwani njaa si unatembea nayo lazima uihisi
 
JIDONDOFILA

JIDONDOFILA

Senior Member
Joined
Jan 8, 2013
Messages
176
Points
225
JIDONDOFILA

JIDONDOFILA

Senior Member
Joined Jan 8, 2013
176 225
Si kweli kua utaenda past. Kwenda past haiwezekani, ni impossible, hata theoretically ni impossible siongelei physically tu. Kwenda future inawezekana ndiyo na proof zipo, ila kwenda nyuma ni impossible, what has happened has already happened, time ni abstraction tumetengeneza wenyewe kuexplain phenomena flani in nature ila doesn't mean kua kuna kitu physically kinaitwa time ambacho unaweza manipulate.

Ukitravel kwa speed ya mwanga (which is impossible coz you have mass) ni kama una-exist in all places at the same time, hii haimaanishi umeenda to the past hapana, bali upo in all places at once, the moment unapostop kuobserve there's no way utakua in the past, either the present somewhere else au in the future.

Unavyozunguka close to the speed of light basi time goes slower for u kuliko observer, haimaanishi unaenda past hapana, ila kwako sekunde tano yaweza kua mwaka kwa mwingine. Hii ni possible na proof zipo.

Tusiongelee kuhusu faster than light kwa kua ni impossible, huwezi kua na infinite mass, hii ingewezekana basi ingekua the end of the universe as we know it. Njia pekee ya kucover distance kubwa ni kwa kudistort spacetime, hii nayo ni theoretical japo scientist wanatafuta njia.

Swala la kwenda to the past futa kabisa akilini, ni impossible, stop wasting time with it in your mind, ni possible kwenye movies tu ila science inagoma. Kwenda past ni sawa na kuviolate conservation of energy.
Graph usiwe na maneno ya kusema impossible kwa mambo usio na ujuzi nayo.Dunia hii kila linalofanyika Tangu mwanzo limehifadhiwa.na ndio sababu tunaziita "Nyakati" na sio "Muda".Bro amini nakuambia "Future Past".namna ya kuifikia ndio bado haijavumbuliwa.
 
Graph

Graph

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2016
Messages
2,065
Points
2,000
Graph

Graph

JF-Expert Member
Joined Jul 20, 2016
2,065 2,000

Kuna vitu ni impossible na proof kua ni impossible ipo. Mfano binadamu huna mabawa huwezi kupaa bila kutumia chombo.

Kwenda past ni kitu kimekua proved again and again, ambao hamjasoma university physics mnaweza msielewe ila yeyote aliyesoma anajua haiwezekani, huwezi kwenda at light speed sababu inahitaji infinite energy, uwezekano wa kusafiri distance kubwa upo theoretically ila sio kwa kwenda speed kali hapana ni kwa kubend space time. Sasa kama hakuna kitu kama infinite energy unategemea past utaenda vipi? Vitu impossible vipo utake usitake in a million years I don’t care, impossible ni impossible.

Huo msemo never say never utumieni kwenye mambo mengine sio haya. Msikariri science sio siasa
 
safuher

safuher

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2019
Messages
3,989
Points
2,000
safuher

safuher

JF-Expert Member
Joined Feb 11, 2019
3,989 2,000
Kuna vitu ni impossible na proof kua ni impossible ipo. Mfano binadamu huna mabawa huwezi kupaa bila kutumia chombo.

Kwenda past ni kitu kimekua proved again and again, ambao hamjasoma university physics mnaweza msielewe ila yeyote aliyesoma anajua haiwezekani, huwezi kwenda at light speed sababu inahitaji infinite energy, uwezekano wa kusafiri distance kubwa upo theoretically ila sio kwa kwenda speed kali hapana ni kwa kubend space time. Sasa kama hakuna kitu kama infinite energy unategemea past utaenda vipi? Vitu impossible vipo utake usitake in a million years I don’t care, impossible ni impossible.

Huo msemo never say never utumieni kwenye mambo mengine sio haya. Msikariri science sio siasa
nakufatili mkuu.

nasubiri maelezo yako kuhusu concept ya Bwan Einsten kuhusu theory of relativity
 
JIDONDOFILA

JIDONDOFILA

Senior Member
Joined
Jan 8, 2013
Messages
176
Points
225
JIDONDOFILA

JIDONDOFILA

Senior Member
Joined Jan 8, 2013
176 225
Kuna vitu ni impossible na proof kua ni impossible ipo. Mfano binadamu huna mabawa huwezi kupaa bila kutumia chombo.

Kwenda past ni kitu kimekua proved again and again, ambao hamjasoma university physics mnaweza msielewe ila yeyote aliyesoma anajua haiwezekani, huwezi kwenda at light speed sababu inahitaji infinite energy, uwezekano wa kusafiri distance kubwa upo theoretically ila sio kwa kwenda speed kali hapana ni kwa kubend space time. Sasa kama hakuna kitu kama infinite energy unategemea past utaenda vipi? Vitu impossible vipo utake usitake in a million years I don’t care, impossible ni impossible.

Huo msemo never say never utumieni kwenye mambo mengine sio haya. Msikariri science sio siasa
Kaka sikukatalii mtazamo wako.na Imani yako juu ya uelewa wa jambo hili.Sio habari za alinacha .soma kisa cha Malkia Sheba(Balkis) na Mfalme solomon(Suleiman)...
Kiufupi Kiti cha enzi cha malkia Balqis kilisafirishwa kutoka Ethiopia mpaka Palestina kwa speed kubwa zaid ya speed ya mwanga..na hii imetokea hapa hapa duniani tena wakati wa nyuma kabisa kabla ya yesu na Mtume Muhammad saw...
Kisa chenyewe kwa ufupi ni kua "Suleimani akiwa na jeshi lake alitoa agizo la kuletewa Kiti cha enzi cha Malkia Balqis.Mmoja kati ya askari wake akasema anaweza kukileta kabla ya kukauka kwa Mate atakayotema chini.Askari wa Kijini ambae pia alikua katika jeshi la Mfalme Suleiman akaona ni muda mrefu sana huo akamwambia mfalme suleiman atakileta kiti hicho kabla ya kusimama wima kutoka kwenye kiti chake alichokikalia.Akasimama mwanajeshi wa tatu ambae alikua Myahudi kama yeye Mfalme Suleiman na Kumwambia .Mfalme mimi nitakuletea kiti hicho cha Enzi cha malkia Balqis kabla ya kupepesa mboni ya jicho lako.na Kweli kabla ya kupepesa hizo kope zake Kiti kilikua mbele yake...
Nakuacha kwa kukuuliza swali hili...Kile kiti kilikua na Mass 0,?
 
JIDONDOFILA

JIDONDOFILA

Senior Member
Joined
Jan 8, 2013
Messages
176
Points
225
JIDONDOFILA

JIDONDOFILA

Senior Member
Joined Jan 8, 2013
176 225
Kuna vitu ni impossible na proof kua ni impossible ipo. Mfano binadamu huna mabawa huwezi kupaa bila kutumia chombo.

Kwenda past ni kitu kimekua proved again and again, ambao hamjasoma university physics mnaweza msielewe ila yeyote aliyesoma anajua haiwezekani, huwezi kwenda at light speed sababu inahitaji infinite energy, uwezekano wa kusafiri distance kubwa upo theoretically ila sio kwa kwenda speed kali hapana ni kwa kubend space time. Sasa kama hakuna kitu kama infinite energy unategemea past utaenda vipi? Vitu impossible vipo utake usitake in a million years I don’t care, impossible ni impossible.

Huo msemo never say never utumieni kwenye mambo mengine sio haya. Msikariri science sio siasa
Graph my brother vitu impossible ni viwili tu ambavyo M/Mungu ametuambia hatuwezi kuvibadili 1,Uzee 2,Kifo
Ni lazima tuzeeke na lazima tufe..Mamlaka ya kuitawala dunia na kuitumia tutakavyo ametupatia..Siri za ulimwengu huu tulizokwisha kuzigundua ni ndogo mnoo na mfano wake ni kama punje ya mchanga uitupe ndani ya Bahari ya Atlantic...
Mpaka sasa tunawasifia sana wakina Izack Newton.Eisten na wengineo kuwa walikua na akili nyingi na uwezo mkubwa wa kutumia Ubongo wao..Lakin yote waliofanya ni asilimia 3 tu ndio waliotumia 97% hawajaitumia kabisaa..
 
Graph

Graph

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2016
Messages
2,065
Points
2,000
Graph

Graph

JF-Expert Member
Joined Jul 20, 2016
2,065 2,000
Graph my brother vitu impossible ni viwili tu ambavyo M/Mungu ametuambia hatuwezi kuvibadili 1,Uzee 2,Kifo
Ni lazima tuzeeke na lazima tufe..Mamlaka ya kuitawala dunia na kuitumia tutakavyo ametupatia..Siri za ulimwengu huu tulizokwisha kuzigundua ni ndogo mnoo na mfano wake ni kama punje ya mchanga uitupe ndani ya Bahari ya Atlantic...
Mpaka sasa tunawasifia sana wakina Izack Newton.Eisten na wengineo kuwa walikua na akili nyingi na uwezo mkubwa wa kutumia Ubongo wao..Lakin yote waliofanya ni asilimia 3 tu ndio waliotumia 97% hawajaitumia kabisaa..
Umeanza kunichanganyia dini kwenye science mkuu? Sio kila mtu anaamini mambo ambayo hayana proof hayo. Sorry sana aisee dini peleka kwa wengine.
 
kali linux

kali linux

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2017
Messages
560
Points
1,000
kali linux

kali linux

JF-Expert Member
Joined May 21, 2017
560 1,000
Kuna vitu ni impossible na proof kua ni impossible ipo. Mfano binadamu huna mabawa huwezi kupaa bila kutumia chombo.

Kwenda past ni kitu kimekua proved again and again, ambao hamjasoma university physics mnaweza msielewe ila yeyote aliyesoma anajua haiwezekani, huwezi kwenda at light speed sababu inahitaji infinite energy, uwezekano wa kusafiri distance kubwa upo theoretically ila sio kwa kwenda speed kali hapana ni kwa kubend space time. Sasa kama hakuna kitu kama infinite energy unategemea past utaenda vipi? Vitu impossible vipo utake usitake in a million years I don’t care, impossible ni impossible.

Huo msemo never say never utumieni kwenye mambo mengine sio haya. Msikariri science sio siasa
mkuu kwenye kitabu cha stephen hawking (BRIEF ANSWERS TO BIG QUESTIONS) alipokua anaelezea kuhusu uwepo wa Mungu alisema kwamba "Some things just need to be given time in order to prove them totally right or wrong"(sijaquote exactly lkn hicho ndicho alichomaanisha) akimaanisha kwamba tutafikia muda na sisi tutajua origin yetu ni ipi LAKINI itatuchukua muda sana kujua. na alitoa mifano kama vle kuna watu waliamini sana katika laws of motion za newton lkn kwa sasa tunaona newton nae hayuko sahihi kivile.

Ungekuwepo mwaka 101 afu ukaambiwa kwamba miaka hii watu tungekua na smartphone basi ungekataa kwa asilimia 10000000% lkn nadhan unaona sasa zinatumika

SO MY POINT NI KWAMBA HIVI VITU TUVIPE MUDA TU. I BELIEVE IN THEORETICAL PHYSICS COZ INATOA MAJIBU KUHUSU MASWALI MENGI SANA.
 
JIDONDOFILA

JIDONDOFILA

Senior Member
Joined
Jan 8, 2013
Messages
176
Points
225
JIDONDOFILA

JIDONDOFILA

Senior Member
Joined Jan 8, 2013
176 225
Umeanza kunichanganyia dini kwenye science mkuu? Sio kila mtu anaamini mambo ambayo hayana proof hayo. Sorry sana aisee dini peleka kwa wengine.
Proof IPI unayoitaka..kwa hio in science ipi unayoijua..Only mathematics ndio inayoweza kuwa proverble kwa namba..think twice bro! Kuna vitu viwili watu kama wewe wa kukopi na kupest mnapungukiwa.
1.Mnadhani ufaham wa mtu upo kweye sense organ pekee.huko ni kukosa msarifa na kufeli katika kupambanua mambo.
2.Unaweza kuwa umekusanya phd hata 3.lakin ukawa bado mjinga tu kama hutokua na "Viini vya Akili",na kua na viini vya akili ni kujitambua wewe ni nani na nini kusudio la wewe kuwepo ktk uso wa dunia.Pia kuufuta ujinga ulio ndani ya Ubongo wako kua Ulimwengu huu ulitokea kwa bahati mbaya na utaodoka kwa bahati mbaya pia.Kaa ukijua Ulimwengu huu yupo alieye uumba na ni yeye pekee anaeuendesha na hajamshirikisha yoyote katika Kuumba mambo haya.Na pia Yu vilevile alivyokua kabla hajaumba mambo haya.Anajua yaliokua na anajua yanayokua na anajua yatakayokua...Na anajua yasiokua laiti hayo yasiokua yangekua Anajua yeye vip na namna gani hayo yasiokua Yangekua..
 
Forum statistics

Threads 1,336,206
Members 512,562
Posts 32,530,544
Top