Time Traveling: Je, linaweza kuwa suluhisho la kifo?

Da'Vinci

Da'Vinci

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2016
Messages
21,076
Points
2,000
Da'Vinci

Da'Vinci

JF-Expert Member
Joined Dec 1, 2016
21,076 2,000
hqdefault-1-jpg.1102207

SALUTE
Mara nyingi hua nasema vitu tunavyoona ni vyakijinga havi-make sense machoni na masikioni mwetu ndio hua na maana na vimeleta mabadiriko makubwa duniani kwetu. Mfano swali la kijinga zaidi alilowahi kujiuliza mwanasayans Issac Newton leo hii limetulitea mabadiriko na maendeleo kwenye maisha , hebu fikiria kama leo hii isac newton angekuuliza kwanini apple limemuangukia kichwani halikwenda juu ungemuona vipi? Hilo swali unaloliona la kijinga limeleta maendeleo makubwa sana. Pia ndoto moja aliyoota albert Einstein waweza kuona ni ya kawaida sana au haina maana lakini ni moja kati ya ndoto iliyoleta mafanikio makubwa duniani, kupitia ndoto tu ya kawaida sana aliyoota tulipata kitu kinachoitwa Theory of Ralativity mambo ya Emc2 yote yote unaweza ona ni kitu cha kawaida ila kina impact kubwa kwenye tasnia ya sayansi

Tarehe 11/5/2019 nilibahatika kuangalia muvi hii inayoitwa Avangers: Endgame, content iliyomo kwenye muvi hii ni Time Traveling, baada ya kuangalia muvi I really admitted that Death might no longer a threat to Mankind!.. Baada ya thanos ku-wipe nusu binaadamu wote ulimwenguni (Universe) , njia pekee iliyobakia kutimka ili kuwarudisha wale waliopotea. Probably Human can stop his Destiny which is Death, Nawaza tu labda Binaadamu twaweza kukiepuka na kukizuia kifo kwa kutumia Theory ya Time Traveling.

Time Travel ni nini..?

Ni kitendo cha kusafiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine ndani ya muda, namaanisha kua mtu anaweza kusafiri leo hii kwenda miaka 5,10,20,25 nk ijayo (Future) au kusafiri kurudi miaka 10,20,30,40,nk iliyopita (Past). Hadithi nyingi za zamani zimekua zikielezea swala hili la kusafiri katika muda.

Huko India kuna hadithi inamzungumzia mfale Raivata Kakudumi ambae alisafiri kwenda mbinguni kukutana na mung wake Brahma, aliporudi alishangaa kua ni miaka mingi imepita. Japan pia kuna hadithi inaitwa Nihongi, inamwelezea kijana mmoja mvuvi anayeitwa Urashima taro ambae alitembelea sehemu iliyochini ya maji, baada ya siku tatu alirudi kijijini kwake akakuta ni miaka 300 imepita, alikuta familia yake imefariki yote. Pia kwa wayahudi mnamo karne ya 1BC mwanafunzi aitwae Honi ha-M'agel inasemekana ailisinzia kwa muda wa miaka 27 alipoamka alikuta hakuna mtu aliyemjua sehemu aliyokua anaishi. Na simulizi nyingii sana kuhusu hii nadharia zimetolewa waweza tafuta ukasoma zaidi.

Wakati watu wengi wakidhani kua muda hautofautiani lakini Mwanasayansi Albert Einstein anaelezea kua muda (Time) haupo hivyo wanavyodhani, unaweza kutofautiana kwa mazingira tofauti, kutegemeana na kasi unayotembea nayo angani (in space)…Theory of special relative ya Enstein inasema kua muda kwenda haraka au kwenda taratibu inategemea na kasii unavyo safiri, mtu akisafiri kwa kasi ya mwanga kwa chombo cha anga angani umri wake utakua mdogo kulinganisha na ndugu au wazazi wake aliowaacha angani..kama akirudi yeye atakua kijana lakini nduguze watakua wamezeeka au wakawa wameshafariki.

Pia kwenye theory ya Albert Einstein ya Theory of General relativity anaelezea kua Garvity (kani ya uvutano) inaweza kupeleka muda mbele au kurudisha nyuma. Anaeleza kua chombo cha anaga kikiwa huko anagani kikakutana na kani ya uvutano basi hua kani hiyo husababisha muda kua slow, hivyo basi hata wanasayansi wa anaga wanakubali kua wasafiri wa anga wanaporudi duniani hua wapo nyuma kimuda yaani saa ya duniani inakua mbele kwa muda microsecond 38 kwa siku. Wanahitimisha kwa kusema mfano msafiri mmoja wa anaga ana pacha wake duniani ammbae hafu akikaa huko angani labda siku 14, Yule pacha aliyebaki duniani atamshinda kwa muda wa microsecond 532 (chukua Microsecond 38 zidisha siku 14)TIME MACHINE

Ili kufanikisha kusafiri katika muda inabidi kuwe na kifaa kinachoiitwa Time machine ambacho hichi kifaa kinauwezo wa kupeleka muda mbele au kurudisha muda nyuma. Bado wanasayansi wanalifanyia kazi suala hili, muda sio mrefu inaweza kuthibishwa kua Time machine inaweza kuanza kufanya kazi. Jinsi Nadharia ya Time Machine inavyofanya kazi kiukweli inanishinda kuielezea kwa Kiswahili kutokana na Ambiguity ya lugha yetu hii. Humo ni masuala ya physics tu so nashindwa niwekeje kwa lugha yetu labda aliyesoma hii kitu akaelewa inavyofanya kazi atatuelezea lifecoded.

Kwenye hili suala la tme Travel kuna kitu kinaitwa Grandfather Paradox ambapo hiki ni kitendo ambacho Time Traveller anarudi kwenye wakati uliopita kisha anaua wazazi wake au babu zake ili yeye awe hakuzaliwa.Kwa mujibu wa wanasayansi na wanafalasafa kama Plato kwenye theory yake ya Platonism anasema kua kubadili maisha yako ya nyuma hakuwezi kuathiri maisha yako ya sasa, lakini mambo yote hayo mawili yanakuja kupingwa na nadharia ya Butterfly Effectt ambapo inasema kua mabadiriko kidogo kwenye sehemu moja yanaweza kuleta mabadiriko makubwa au utofauti mkubwa baadae katika sehemu nyingine

Hii inamaanisha kwamba kama time traveler akirudi katika maisha yaliyopita akamuua baba aua babu yake anaweza sababisha mabadiriko katika maisha yake aliyotoka au future yake.

Kwa muhtsari huu kuhusu theory ya Time Traveling iko hivo japo watafiti wengi wanasema Time Travel hauwezekani iko too theoretically ila mimi naona hiki kitu ni real kabisa kipo, kwanini? Unajua binaadamu hawezi kufikiri nje ya vitu ambavyo vipo duniani nikimaanisha kua hata mimi au wewe hatuwezi kuwaza au kufikiri nje ya vile vitu tulivyoviona,kuambiwa au viliwahi kuwepo. Utawaza Mungu kwakua ulisikia kua kuna Mungu, utawaza nyumba kwakua ushaiona nyumba nk nk. Mantiki yangu ni kwamba hata hao watu wanaosema time travel is real hawakukaa tu wakafikiri kitu amabacho hakipo, mtazamo wangu naamini hiki kitu kipo na kinafanya kazi labda kwa siri kumbuka hata Internet tunaambiwa imeletwa mwaka 1991 na Tim Berners lee lakini ni kitu kipo toka miaka ya 1950s sema Tim aliifanya kua Popular baada ya kutengeneza World Wide Web…

Lakini haya ni mawazo yangu tu kwamba labada kama Time Machine ikifanikiwa kutengenezwa watu wanaweza kuitumia kukwepa kifo labda kwa kurudisha muda nyuma na kukwepa kile kitu kilichopelekea kufariki..kwa mafano kwenye muvi inaitwa Time Trveler’s wife wameelezea tukio hili linavyoweza kufanyika.
~Da'vinci..
 
Baba Swalehe

Baba Swalehe

JF-Expert Member
Joined
Jun 6, 2017
Messages
14,266
Points
2,000
Baba Swalehe

Baba Swalehe

JF-Expert Member
Joined Jun 6, 2017
14,266 2,000
kusema tu kwamba hakukuwa na simu alafu ukataka nielewe sio vizuri hivyo mkuu.
kuna baadhi ya mambo mtu anahoji kwa uelewa wake apate jawabu stahiki kabisa.

yani camera wakati huo zilikuwepo, pengine na redio za kudaka mawasiliano. na picha zikarekodiwa kupitia camera hiyo.

sasa kama hivyo viliwezekana kwa nini iwe ajabu kwa wakati huo kuweko Kwa simu zenye camera za kurekodia..?

ninachotaka kusema ni kwamba hiyo hoja haipaswi kuweka kTika hoja ambazo zinatetea time travelling. ni hoja dhaifu kabisa.

ni Sawa na mtu kuoneahwa picha ya camera ya kwanza kutengenezwa pasi na kujiuliza kama hiyo ni ya kwanza vipi ipigwe picha.

muhimu tusitukanane na kuvunjianaadabu, lakini kutaka kila kinachosemwa na watu fulani kikubalike moja kwa moja kama unavyokubali wewe hilo sioni kama tutakuwa na maelewano mazuri baina yetu.
Nisikilize vifaa

Vya kurekodia vya zamani vilikua on analogie form

Mfano mrahisi hakukua na ku editi ngoma ukirekodi umesharekodi

System ya simu za sasa na vifaa vya zamani vya kurekodia ni vitu viwili tofauti

Tafadhali sana
 
Baba Swalehe

Baba Swalehe

JF-Expert Member
Joined
Jun 6, 2017
Messages
14,266
Points
2,000
Baba Swalehe

Baba Swalehe

JF-Expert Member
Joined Jun 6, 2017
14,266 2,000
Hahahaaa unalo.. naona kaamua kukukaba na maswali
Mkuu amenishangaza sana

Sababu mfumo wa simu kuwekwa kamera ni wa hivi karibuni haswa

Na mfumo wa camera za zamani uko tofauti sana

Sasa nakuogopa kumweleza huyu bwana deep zaidi tutaanza kuonekana wajuaji
 
JIDONDOFILA

JIDONDOFILA

Senior Member
Joined
Jan 8, 2013
Messages
176
Points
225
JIDONDOFILA

JIDONDOFILA

Senior Member
Joined Jan 8, 2013
176 225
Mkuu unanishawishi niongelee kitu kinachoitwa Multi Universe.. sema nikiongea hapa tutazidi kuachana gizani. Matukio ya hvyo kuhusu picha zinapigwa afu intakea jambo lisilo la kawaida kwenye picha nadhani yako mengi.. baadhi yameelezwa kwenye nyuzi humu. Naomba tu siku Time Travelling ikiwa possible watu wote waliosoma uzi huu wawe hai
Da Vinci nafaham Uzi huu sio wakidin.ila ninachotaka kuwaeleza hio Time travell ni Real ila haiwezi kuzuia Kifo...
Fact:Hio kitu imeelezwa waziwazi na Abal Qassim kwenye safari yake ya miraji..
1,Aliwaona wanawake wengi wamejaa motoni. .jambo ambalo hata hukumu haijapita
2,Speed ya buraq na ngazi ya miraji kama iliwezekana kwake basi ni ishara tosha ipo cku kitaundwa chombo chenye 0mass na kitakua na speed kuliko mwanga..
3,Jawabu alilotoa swahaba wake alimuuliza Kati ya Mwanamume na Mwanamke nani anaenjoy zaidi kwenye tendo la jimai...Swahabu huyu alijibu ni Mwanamke..kisa chenyewe kipo hivi..
Swahaba huyu alikua kwenye darsa la Abal Qassim jioni ya siku ya Akhamis Akamuuliza Abal Qassim hivi..Ewe Mjumbe wa Allah naomba uujulishe Umma na Wanadam kwa ujumla Kati ya M/mke na M/mme ni nani Anafaidi zaidi kuliko mwenzie katika Tendo la jimai..Kabla hajatoa jawabu muda wa swala ukawa umeingia akamwambia atamjibu kesho baada ya swala ya yaumul jumaa..
Siku ya ijumaa ikaingia na Huyu swahaba aliposikia ile adhana ya mapemama akawahi mtoni ili akaoge na kuchukua udhu kwa ajili ya swala ya jumaa na shauku ya kupata jibu la swali lake.
Akafika mtoni akavua nguo zake na kujrusha mtoni...wakati anajiandaa kupiga mbizi mtoni alimsikia muadhiini ndio anasema Maneno ya Mwanzo kabisa yaani "Allahu akbar Allahu akbar..
Swahaba huyu alipoibuka hakuona nguo zake na wala sehemu alioibukia hakuwahi fika wala kuijua kabisa na cha kushangaza aliibuka akiwa bint kigori kabisaa..na alipotoka mtoni akakuta nguo za kike akajistiri..
Alipoanza kuelekea sehem za makazi akakutana na m/mme mmoja akamueleza yeye ni mgeni na hana makazi..
Kwa Urembo na uzuri aliokua nao yule mwanaume alimpenda na kuamua kumuoa..Swahabu huyu aliebadilika na kuwa binti Alishiriki tendo la ndoa na mumewe na katika vipindi tofauti na kumzalia watoto wawili...
Siku moja akapata hamu yakwenda mtoni kuoga na kuchota maji.akaenda mtoni akavua nguo zake na kujitumbukiza mtoni..
Alipoibuka akaibukia palepale alipoziacha nguo zake za kiume na akiwa mwanamume na cha kushangaza zaidi alimsikia muadhini yuleyule akimalizia Adhana kwa maneno ya Mwisho "Laila hailallah" .
Alivaa nguo zake na kuelekea msikitini..
Baada ya swala maswahaba walimkumbusha mtume juu swali aliloulizwa jana..na kabla hajajibu alimsimamisha Swahaba yuleyule aliemuuliza swali ili atoe jibu.
Alijibu ni Mwanamke na kisha Abal Qassim alikielezea kisa kizima kilichomkuta swahaba yule kama nilivyokihadithia.
4 Kwa suleiman bin Daudi hali hii ilitokea ya Time travell.Sulemain alikua na mwanafunzi wake ambae hakupenda kufa akiwa kijana..na kifo ni siri ya Allah Sw.basi yule kijana akamuomba suleiman amuombee afe akiwa mzee..suleiman akamuombea..kijana akafurah na kua na yakini za Dua za mtume ni Makubuul.
Siku ilifuata suleimani akiwa katka misafara yake na kijana wake Malaika mtoa roho akamfikia yule kijana.kijana aliogopa sana na akaamua kumfuata Suleiman na kumueleza kuna mtu amemjia anatisha sana.akamuelekeza mahala alipo.
Suleimani alupomuona akamwambia yule ni malaika mtoa roho.na amekuja kuichukua Roho yako.kijana akapagawa na kumuuliza kama dua yake haikukubaliwa.Suleimani akamwambia Asihofu dua yake ilkubaliwa.
Alichofanya suleimani ni kuuamrisha upepo umpeleke mashariki linapochomoza jua..sehemu hio kwa mwendo wa farasi mwenye kasi sana wakati huo angetumia miaka 50 kufika..na kuuamrisha upepo popote anapotaka apelekwe huyo kijana basi upepo umtii..
Upepo ule ulimsafirisha mpaka mashariki linapochomoza jua.kwa muda mfupi sana.alipofika hakukaa hata muda mrefu akamuona tena yule malaika mtoa roho..alipoona hivyo akauamrisha upepo umpeleke magharibi jua linapozama..ukafanya hivyo.ila alupofika msgharibi jua linapozama akamkuta pia malaika mtoa roho anamgojea..baada ya kuana hakuna pa kumkwepea mtoa roho akaamua kuuamrisha upepo umrudishe palepale alipoanzia safari yake akiwa na suleimani.alipofika kwanza alishangaa mno na alipowauliza wenyeji juu ya mfalme suleimani walimjibu kwa kumwambia mfalme huyo alikuwepo miaka 200 iliopita hali ya kua yeye bado kijana .
Muda mchache baadae malaika mtoa roho alimfikia na kuichukua roho yake..
Kisa hiki kina mafunzo mawili
1Time travel ipo na inatendeka ndani ya ulimwengu huu.
2.Pamoja na kuwepo kwake haitazuia kifo na hata utaratibu wa Qadari ya Allah sw.inawezekana kabisa watu kuishi kwenye past zao na Hata future zao..
Kinachofanyika ktk uweza wa Allah sw ni kun faya kun(kuwa na inakua),
Wanachofanya wanajitihada ( wanasayansi wa mambo haya) ni kupata kifaa maalumu kitakachothibitisha juu ya Nadharia hii ambayo imekuwepo enzi na enzi.
 
JIDONDOFILA

JIDONDOFILA

Senior Member
Joined
Jan 8, 2013
Messages
176
Points
225
JIDONDOFILA

JIDONDOFILA

Senior Member
Joined Jan 8, 2013
176 225
Kifo ni hatua ya kuelekea maisha ya kaburini kisha ufufuo kisha malipo na mwisho kabisa maisha ya milele.

Kama ilivyo hatua ya kutambaa mtoto kisha atembee.

Inabidi pia uchunguze je ni kweli hao Wanasayansi wanashughulika na kutafuta tiba ya kifo ? Isiwe wanafurahisha tu sababu wameshawajua mnapenda story za kisayansi huku Ukweli wakiujua ya kuwa haiwezekani kwa jambo hilo,kama vile wanavyowafurahisha katika "Time Travel" au kama walivyowafurahisha katika "Safari ya mtu kwenda Mwezini". Muwe mnawahoji hao Wanasayansi msifanywe kama jalala lisilochagua taka.

Mimi nipo,ila mnatakiwa mjue ya kuwa kifo si tatizo wala kifo si Ugonjwa sasa vipi utafute tiba ? Wanasayansi huwa wanafikiri kitoto sana na ujuaji ukiwa mwingi kuna maarifa wananyimwa.
Bro Zuri mie nakukubali katika uchambuzi wa baadhi ya nadharia za kisayansi na ufafanuzi ktk uelewa wanasayansi wa kikufari.ila bado napata tabu juu ya neno la Qur an Mutashabiha.kama haya mambo mutashabiha yapo vip unakua unayafutu maswala ambayo ni mutashabia ambayo huna yakini nayo
 
safuher

safuher

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2019
Messages
3,989
Points
2,000
safuher

safuher

JF-Expert Member
Joined Feb 11, 2019
3,989 2,000
Nisikilize vifaa

Vya kurekodia vya zamani vilikua on analogie form

Mfano mrahisi hakukua na ku editi ngoma ukirekodi umesharekodi

System ya simu za sasa na vifaa vya zamani vya kurekodia ni vitu viwili tofauti

Tafadhali sana
kuna kujibu na kujitetea wewe mkuu unajitetea.

enewei mkuu naomba tufikie hapo kuepusha kutoelewana.
 
safuher

safuher

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2019
Messages
3,989
Points
2,000
safuher

safuher

JF-Expert Member
Joined Feb 11, 2019
3,989 2,000
Da Vinci nafaham Uzi huu sio wakidin.ila ninachotaka kuwaeleza hio Time travell ni Real ila haiwezi kuzuia Kifo...
Fact:Hio kitu imeelezwa waziwazi na Abal Qassim kwenye safari yake ya miraji..
1,Aliwaona wanawake wengi wamejaa motoni. .jambo ambalo hata hukumu haijapita
2,Speed ya buraq na ngazi ya miraji kama iliwezekana kwake basi ni ishara tosha ipo cku kitaundwa chombo chenye 0mass na kitakua na speed kuliko mwanga..
3,Jawabu alilotoa swahaba wake alimuuliza Kati ya Mwanamume na Mwanamke nani anaenjoy zaidi kwenye tendo la jimai...Swahabu huyu alijibu ni Mwanamke..kisa chenyewe kipo hivi..
Swahaba huyu alikua kwenye darsa la Abal Qassim jioni ya siku ya Akhamis Akamuuliza Abal Qassim hivi..Ewe Mjumbe wa Allah naomba uujulishe Umma na Wanadam kwa ujumla Kati ya M/mke na M/mme ni nani Anafaidi zaidi kuliko mwenzie katika Tendo la jimai..Kabla hajatoa jawabu muda wa swala ukawa umeingia akamwambia atamjibu kesho baada ya swala ya yaumul jumaa..
Siku ya ijumaa ikaingia na Huyu swahaba aliposikia ile adhana ya mapemama akawahi mtoni ili akaoge na kuchukua udhu kwa ajili ya swala ya jumaa na shauku ya kupata jibu la swali lake.
Akafika mtoni akavua nguo zake na kujrusha mtoni...wakati anajiandaa kupiga mbizi mtoni alimsikia muadhiini ndio anasema Maneno ya Mwanzo kabisa yaani "Allahu akbar Allahu akbar..
Swahaba huyu alipoibuka hakuona nguo zake na wala sehemu alioibukia hakuwahi fika wala kuijua kabisa na cha kushangaza aliibuka akiwa bint kigori kabisaa..na alipotoka mtoni akakuta nguo za kike akajistiri..
Alipoanza kuelekea sehem za makazi akakutana na m/mme mmoja akamueleza yeye ni mgeni na hana makazi..
Kwa Urembo na uzuri aliokua nao yule mwanaume alimpenda na kuamua kumuoa..Swahabu huyu aliebadilika na kuwa binti Alishiriki tendo la ndoa na mumewe na katika vipindi tofauti na kumzalia watoto wawili...
Siku moja akapata hamu yakwenda mtoni kuoga na kuchota maji.akaenda mtoni akavua nguo zake na kujitumbukiza mtoni..
Alipoibuka akaibukia palepale alipoziacha nguo zake za kiume na akiwa mwanamume na cha kushangaza zaidi alimsikia muadhini yuleyule akimalizia Adhana kwa maneno ya Mwisho "Laila hailallah" .
Alivaa nguo zake na kuelekea msikitini..
Baada ya swala maswahaba walimkumbusha mtume juu swali aliloulizwa jana..na kabla hajajibu alimsimamisha Swahaba yuleyule aliemuuliza swali ili atoe jibu.
Alijibu ni Mwanamke na kisha Abal Qassim alikielezea kisa kizima kilichomkuta swahaba yule kama nilivyokihadithia.
4 Kwa suleiman bin Daudi hali hii ilitokea ya Time travell.Sulemain alikua na mwanafunzi wake ambae hakupenda kufa akiwa kijana..na kifo ni siri ya Allah Sw.basi yule kijana akamuomba suleiman amuombee afe akiwa mzee..suleiman akamuombea..kijana akafurah na kua na yakini za Dua za mtume ni Makubuul.
Siku ilifuata suleimani akiwa katka misafara yake na kijana wake Malaika mtoa roho akamfikia yule kijana.kijana aliogopa sana na akaamua kumfuata Suleiman na kumueleza kuna mtu amemjia anatisha sana.akamuelekeza mahala alipo.
Suleimani alupomuona akamwambia yule ni malaika mtoa roho.na amekuja kuichukua Roho yako.kijana akapagawa na kumuuliza kama dua yake haikukubaliwa.Suleimani akamwambia Asihofu dua yake ilkubaliwa.
Alichofanya suleimani ni kuuamrisha upepo umpeleke mashariki linapochomoza jua..sehemu hio kwa mwendo wa farasi mwenye kasi sana wakati huo angetumia miaka 50 kufika..na kuuamrisha upepo popote anapotaka apelekwe huyo kijana basi upepo umtii..
Upepo ule ulimsafirisha mpaka mashariki linapochomoza jua.kwa muda mfupi sana.alipofika hakukaa hata muda mrefu akamuona tena yule malaika mtoa roho..alipoona hivyo akauamrisha upepo umpeleke magharibi jua linapozama..ukafanya hivyo.ila alupofika msgharibi jua linapozama akamkuta pia malaika mtoa roho anamgojea..baada ya kuana hakuna pa kumkwepea mtoa roho akaamua kuuamrisha upepo umrudishe palepale alipoanzia safari yake akiwa na suleimani.alipofika kwanza alishangaa mno na alipowauliza wenyeji juu ya mfalme suleimani walimjibu kwa kumwambia mfalme huyo alikuwepo miaka 200 iliopita hali ya kua yeye bado kijana .
Muda mchache baadae malaika mtoa roho alimfikia na kuichukua roho yake..
Kisa hiki kina mafunzo mawili
1Time travel ipo na inatendeka ndani ya ulimwengu huu.
2.Pamoja na kuwepo kwake haitazuia kifo na hata utaratibu wa Qadari ya Allah sw.inawezekana kabisa watu kuishi kwenye past zao na Hata future zao..
Kinachofanyika ktk uweza wa Allah sw ni kun faya kun(kuwa na inakua),
Wanachofanya wanajitihada ( wanasayansi wa mambo haya) ni kupata kifaa maalumu kitakachothibitisha juu ya Nadharia hii ambayo imekuwepo enzi na enzi.
nimevutiwa na maelezo mkuu.

sasa labda wewe kwa unavoelewa ili mtu usafiri uende kwenye past ufanyeje..?

je uwe na spidi kali sana ukitembea huko angani ?

au uwe na spidi kali ukitembea hapa duniani ?

naamini dunia in Mengi sana na hizi tafiti za wanasayansi zinazidi kuniongezea imani yangu juu ya DINI HII YA kiislamu.

maana ninaona kabisa kwamba kuna mambo ya aabu yapo katika uislamu ambayo najiuliza hao waliyoyanukuu walikuwa na ujasiri gani kunukuu ?

ina maana hawakuhofia kwamba watu watahisi ni uongo kama vile mtume muhammad kwenda miiraji n. k

kuna hadithi inasema "katik pepo kuna daraja mia, baina ya daraja na daraja katika hizo daraja mia upishano wake ni baina ya mbingu na ardhi "

mtu anawezakuona hizi ni stori za kutunga lkini hata wanasayansi sasa hivi wanatuambia kwamba hata umbali baina ya nyota moja na nyingine unaweza kufika KM 340000 sasa angalia kuna nyota ngapi huko juu na huo umbali baina ya nyota na nyota ?

pia wanasema watu wa astronomy ya kuwa kuna madudu makubwa huko juu ambayo ukubwa wake basi jua lijirudie siochini ya mara 1000(kwa uchache) ndo linaweza kufanana na hayo madudu.

kiufupi Uislamu umeeleza Mengi sana ambayo wanasayansi ndo wanatafuta sababu zao na kuzielezea hapo.

lakini mimi najikita sana na kufatilia mambo ya astronomy huko nazidi kuamini kwamb Qurani imetoka Kw Mungu.

yani inaonesha ya kuwa dunia ni kijitu kidogo sana katika uislamu.kwa sababu mifano inayppogwa na Mafundisho ya uislamu ni mifano ambayo mtu anaweza kuona ni kujikuza lakini ipo kwa hakika.
 
Z

Zurri

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2018
Messages
9,520
Points
2,000
Z

Zurri

JF-Expert Member
Joined Apr 6, 2018
9,520 2,000

Kwanza kaka kabla sijasema chochote fatilia hivi visa viwili ulivyovisimulia hapa kisha utupe marejeo yako,yaani kile cha mwanaume kwa mwanamke na hiki cha nabii Suleimani.

Pil,suala la tukio la Israa na Miiraji halihusiani na Time Travel,labda uwe umeelewa vibaya.

Ili tendo au jambo litokee linahitaji nafasi na muda. Safari ya mtume kwenda mbinguni ni kuonyesha uwezo wa Allah pili,imekuka katila Qur'aan inaonyesha ya kuwa malaika wanapochukua matendo ya waja na kuyapeleka mbinguni hutumia siku moja ambayo ni sawa na miaka elfu moja kwetu,na kuna aya imekuja ikisema siku moja sawa na miaka elfu hamsini kwa tukio lingine.

Allah aliye juu alimchukua kweli mja wake roho na kiwili wili,na ule ni uwezo wa Allah aliye juu.
 
Z

Zurri

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2018
Messages
9,520
Points
2,000
Z

Zurri

JF-Expert Member
Joined Apr 6, 2018
9,520 2,000
Bro Zuri mie nakukubali katika uchambuzi wa baadhi ya nadharia za kisayansi na ufafanuzi ktk uelewa wanasayansi wa kikufari.ila bado napata tabu juu ya neno la Qur an Mutashabiha.kama haya mambo mutashabiha yapo vip unakua unayafutu maswala ambayo ni mutashabia ambayo huna yakini nayo
Ili nipate pakuanzia,unaweza kuniambia ni jambo gani ambalo ni mutashabiha ?
 
JIDONDOFILA

JIDONDOFILA

Senior Member
Joined
Jan 8, 2013
Messages
176
Points
225
JIDONDOFILA

JIDONDOFILA

Senior Member
Joined Jan 8, 2013
176 225
Ili nipate pakuanzia,unaweza kuniambia ni jambo gani ambalo ni mutashabiha ?
1,Kusimama kwa mbingu saba na ardhi saba pasi na nguzo zinazoshikilia.
2.Siku za Uumbaji ni zipi.na Kati ya Maji na Àrsh kipi kilianza kuumbwa.
Hayo machache.
 
rip faza_nelly

rip faza_nelly

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2018
Messages
2,137
Points
2,000
rip faza_nelly

rip faza_nelly

JF-Expert Member
Joined Feb 19, 2018
2,137 2,000
Hii niliiona kwenye muvi ya GI Joe:Rise of cobra nkawa sielewi ni nini ile.
Technology ziko za ajabu sana

mfano hologram..ni toka mwaka 2008...mtu yuko mwanza unamleta Dar unaongea nae..
cnn walifanya live siku ile Obama anachaguliwa...

Juzi nimeona mtu anavaa nguo halafu anapaa kwenye BBC hatari sana
 
JIDONDOFILA

JIDONDOFILA

Senior Member
Joined
Jan 8, 2013
Messages
176
Points
225
JIDONDOFILA

JIDONDOFILA

Senior Member
Joined Jan 8, 2013
176 225
Kwanza kaka kabla sijasema chochote fatilia hivi visa viwili ulivyovisimulia hapa kisha utupe marejeo yako,yaani kile cha mwanaume kwa mwanamke na hiki cha nabii Suleimani.

Pil,suala la tukio la Israa na Miiraji halihusiani na Time Travel,labda uwe umeelewa vibaya.

Ili tendo au jambo litokee linahitaji nafasi na muda. Safari ya mtume kwenda mbinguni ni kuonyesha uwezo wa Allah pili,imekuka katila Qur'aan inaonyesha ya kuwa malaika wanapochukua matendo ya waja na kuyapeleka mbinguni hutumia siku moja ambayo ni sawa na miaka elfu moja kwetu,na kuna aya imekuja ikisema siku moja sawa na miaka elfu hamsini kwa tukio lingine.

Allah aliye juu alimchukua kweli mja wake roho na kiwili wili,na ule ni uwezo wa Allah aliye juu.
1.Labda nianze na mareje..sina kumbukumbu nzuri ila Kitabu kinaitwa "Ayatu al Quburatul Al Qubra.muandishi nimemsahau nikikumbuka nitakuambia na mlango wake pia.
2.Wewe hukunielewa bila shaka sikushika mantik ya kisa cha miraji kwenye safari ya isra wala ile ya miraji..maudhui nilioikusudia hata mayahudi walimuhoji..kwahio wewe kuhoji sishangai...Kusudio langu hapa niyeye kua kwenye future hali ya kuwa Hukmu ya watu wa motoni na peponi haijatokea..labda upinge na wewe kua ilikua ni ndoto.na kama unaamini alienda kama mtu kamili na basi alitangulia future kabla haijatokea..na mbali na kuwaona wanawake wengi motoni pia aliziona adhabu za ndani ya jahanam..aliwaona watu wana Ngozi kubwa kama tembo na kila walipokua wakiungua na kumalizika walivikwa tena ngozi ile.aliona vitu vingi ambavyo kwa akili ya kawaida ni ngumu kuamin...hili jambo la baadhi ya watu kuwa mbele ya wakati au kua nyuma ya wakati limeelezwa mara nyingi mnoo ndani ya Qur an na msemo wa kawaida kusikia Kwa Maulamaa kuwa"Qur an ipo mbele ya Wakati"
Amin nakuambia wapo mbele ya wakati na kuna baadhi ambao wapo nyuma ya wakati kwelikweli.
 
Ninachopinga ni kuepuka kifo..hicho ndicho ninachopinga...mlango wangu wa ufaham upo wazi kukubali kurudi past na hata kwenda future inawezekana isipokua haiwezi kuchange chochote katika Qadar ya Allah.
 
safuher

safuher

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2019
Messages
3,989
Points
2,000
safuher

safuher

JF-Expert Member
Joined Feb 11, 2019
3,989 2,000
1.Labda nianze na mareje..sina kumbukumbu nzuri ila Kitabu kinaitwa "Ayatu al Quburatul Al Qubra.muandishi nimemsahau nikikumbuka nitakuambia na mlango wake pia.
2.Wewe hukunielewa bila shaka sikushika mantik ya kisa cha miraji kwenye safari ya isra wala ile ya miraji..maudhui nilioikusudia hata mayahudi walimuhoji..kwahio wewe kuhoji sishangai...Kusudio langu hapa niyeye kua kwenye future hali ya kuwa Hukmu ya watu wa motoni na peponi haijatokea..labda upinge na wewe kua ilikua ni ndoto.na kama unaamini alienda kama mtu kamili na basi alitangulia future kabla haijatokea..na mbali na kuwaona wanawake wengi motoni pia aliziona adhabu za ndani ya jahanam..aliwaona watu wana Ngozi kubwa kama tembo na kila walipokua wakiungua na kumalizika walivikwa tena ngozi ile.aliona vitu vingi ambavyo kwa akili ya kawaida ni ngumu kuamin...hili jambo la baadhi ya watu kuwa mbele ya wakati au kua nyuma ya wakati limeelezwa mara nyingi mnoo ndani ya Qur an na msemo wa kawaida kusikia Kwa Maulamaa kuwa"Qur an ipo mbele ya Wakati"
Amin nakuambia wapo mbele ya wakati na kuna baadhi ambao wapo nyuma ya wakati kwelikweli.
nakubaliana na maelezo yako umefikiria vizuri sana kuhusu hilo sulala.labda tofauti ni kuwa ALLAH hakusem kuwa huyo ni time travelling.

ila kwa time travelling wanayoielzea hao wanafizikia basi hata zile za kwenye Qurani tunaqeza kuzitia kwenye time travelling kwa sababu tukio la Mbele mtu analiona sasa wakati wale anaowaona bado wako kwingine kawaacha.

Mtume kwenda miiraji alisafiri kwa spidi kubwa sana na yule mnyama alafu akaona mambo ya futuree sijui pana nini kati ya spidi na future.

ila tu ninchoamini ya kuwa Mtume alisafiri na kuona future kwa taufiqi ya Mola mlezi
 
JIDONDOFILA

JIDONDOFILA

Senior Member
Joined
Jan 8, 2013
Messages
176
Points
225
JIDONDOFILA

JIDONDOFILA

Senior Member
Joined Jan 8, 2013
176 225
nimevutiwa na maelezo mkuu.

sasa labda wewe kwa unavoelewa ili mtu usafiri uende kwenye past ufanyeje..?

je uwe na spidi kali sana ukitembea huko angani ?

au uwe na spidi kali ukitembea hapa duniani ?

naamini dunia in Mengi sana na hizi tafiti za wanasayansi zinazidi kuniongezea imani yangu juu ya DINI HII YA kiislamu.

maana ninaona kabisa kwamba kuna mambo ya aabu yapo katika uislamu ambayo najiuliza hao waliyoyanukuu walikuwa na ujasiri gani kunukuu ?

ina maana hawakuhofia kwamba watu watahisi ni uongo kama vile mtume muhammad kwenda miiraji n. k

kuna hadithi inasema "katik pepo kuna daraja mia, baina ya daraja na daraja katika hizo daraja mia upishano wake ni baina ya mbingu na ardhi "

mtu anawezakuona hizi ni stori za kutunga lkini hata wanasayansi sasa hivi wanatuambia kwamba hata umbali baina ya nyota moja na nyingine unaweza kufika KM 340000 sasa angalia kuna nyota ngapi huko juu na huo umbali baina ya nyota na nyota ?

pia wanasema watu wa astronomy ya kuwa kuna madudu makubwa huko juu ambayo ukubwa wake basi jua lijirudie siochini ya mara 1000(kwa uchache) ndo linaweza kufanana na hayo madudu.

kiufupi Uislamu umeeleza Mengi sana ambayo wanasayansi ndo wanatafuta sababu zao na kuzielezea hapo.

lakini mimi najikita sana na kufatilia mambo ya astronomy huko nazidi kuamini kwamb Qurani imetoka Kw Mungu.

yani inaonesha ya kuwa dunia ni kijitu kidogo sana katika uislamu.kwa sababu mifano inayppogwa na Mafundisho ya uislamu ni mifano ambayo mtu anaweza kuona ni kujikuza lakini ipo kwa hakika.
Kaka jambo hili litatokea tu isipokua litatokeaje sina jibu...labda nikupe mfano mmoja miaka 1441 iliopita kuna mtu mmoja jina Muhammad alisafiri kwa kasi ya ajabu na kiumbe anaefanana na farasi lakini mwenye mbawa mbili za kuruka angani.alisafiri umbali ambao watu wa wakati wake walkua wakitumia mwezi 1 kwenda na mwezi 1 kurudi...ila yeye alitumia Robo ya usiku tu yaani masaa 3 kwenda na kurudi.alipowaambia watu wake walimbishia na kumpinga kiasi ambacho waliamua kumuweka kitimoto ili awape màjibu ya maswali ya mambo alioyaona kwenye msikiti wa Al aqsa.
Kumbuka ameenda usiku na vitu vingi kuonekana kwenye giza ni ngumu sana.hapa ndio mwanzo wa kuvumbuliwa kwa tv na live coverage.
Aliletewa msikiti wote mbele yake..na kila swali la sehemu alilokua akiulizwa.alionyeshwa na alijibu kwa ufasaha zaidi na ziada ya vitu vigine..
Hapa nakusudia kukueleza mambo makuu mawili.
1.hakuna aliejua kutavumbuliwa chombo kinachoitwa ndege ambapo itakua Kikipaa na mwendo wa kasi kama Mnyama Buraq ambacho kwa muda mfupi kinaweza kwenda km nyingi kikiwa kimebeba abiria au mizigo..
2,Kuwekewa kioo(tv),ambacho kilimuwezesha kuona eneo lote la msikiti..wengi hawakuamini isipokua wachache tu.na hili jambo kwa lugha ya malkia linaitwa "Future Past".
Miaka 1300 baadae vyombo hivyo vimekua Real...Amin hata kama Mimi na wewe hatutoshuhudia jambo hilo.
 
Z

Zurri

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2018
Messages
9,520
Points
2,000
Z

Zurri

JF-Expert Member
Joined Apr 6, 2018
9,520 2,000
1,Kusimama kwa mbingu saba na ardhi saba pasi na nguzo zinazoshikilia.
2.Siku za Uumbaji ni zipi.na Kati ya Maji na Àrsh kipi kilianza kuumbwa.
Hayo machache.
Maswali yako mazuri. Kwanza naanza kwa utangulizi mfupi kisha nitakupa mifano na marejeo ya vitabu ukapitie na ninafanya hivyo ili kuepuka kukosea.

Mwanachuoni mkubwa aitwae Imaam Shawkaniy Allah amrehemu,alipata kusema hivi "Maneno ya Allah aliye juu haya pingani kwa yenyewe,na ukihisi au kuona yanapingana basi kitu cha kitu cha kwanza ituhumu akili yako kwa kushindwa kung'amua maana ya aya hizo au ituhumu elimu yako kwa kushindwa kuidiriki maana a aya husika"

Wanazuoni wengine wakafika mbali na kusema ya kuwa mpaka maneno ya mtume hayapingani kadhalika. Kutokana na hali hiyo,katika fani ya misingi ya tafsiri ya Qur'aan utakuta kipengele cha "Kupatanisha" (Reconcile) aya ili zilete maana moja na katika katika hadithi vile kuna upatanishaji wa hadithi,na hapa kuna mifano mingi.

Tukianza na suala ya siku za uumbaji,idadi kamili ni siku sita na hili limethibitishwa katika aya zote,bali kuna wale ambao hawakuelewa maandiko na kujitia wajuaji na kusema Qur'aan imesema uongo kwamba idadi ni siku nane,hapa wao wanaosema ni siku nane nio waongo,kwani kuna kuumba na kuweka,wao wakaona kuweka ni kuumba pia,hili la idadi ya siku za uumbaji nilishamjibu mtu mmoja humu.

Ama suala la kwanza la kusimama mbingu na dunia pasi na nguzo,hili kuna mapokezi nimepata kuyasikia ya kuwa kuna malaika ambao wamepewa kazi hiyo ya kushikilia mbingu na ardhi na hawa hawawezi luwa nguzo kama mtu akisema hao ni badala ya nguzo. Hili nitalifatilia ili kuona mapokezi hayo wanazuoni wameyapatanisha vipi wakapata jibu moja.

Nakupa mfano mmoja,kuna hadithi zimepokewa katika maana tofauti kutokana na matukio aliyo fanya mtume,hapa sitakunukulia matini bali nakupa maana,kuna hadithi moja ilionyesha ya kuwa mtume wa Allah amani iwe juu yake alisema mtu ukishika utupu udhu umetenguka,lakini kuna mapokezi mengine mtume alionekana eshika utupu wake lakini akasali bila ya kushika udhu,sasa mapokezi haya wanazuoni walivyoyapatanisha wakapata jibu moja ya kuwa "Mtu ukishika tupu yako kwa matamanio udhu unakutoka", kwa maana yanakuwa yamefanyiwa kazi mapokezi yote mawili.

Allah anajua zaidi,na popote nilipokosea basi ni kwa udhaifu ila Allah ahusiki na makosa hayo na ukamilifu ni wake.
 
JIDONDOFILA

JIDONDOFILA

Senior Member
Joined
Jan 8, 2013
Messages
176
Points
225
JIDONDOFILA

JIDONDOFILA

Senior Member
Joined Jan 8, 2013
176 225
nakubaliana na maelezo yako umefikiria vizuri sana kuhusu hilo sulala.labda tofauti ni kuwa ALLAH hakusem kuwa huyo ni time travelling.

ila kwa time travelling wanayoielzea hao wanafizikia basi hata zile za kwenye Qurani tunaqeza kuzitia kwenye time travelling kwa sababu tukio la Mbele mtu analiona sasa wakati wale anaowaona bado wako kwingine kawaacha.

Mtume kwenda miiraji alisafiri kwa spidi kubwa sana na yule mnyama alafu akaona mambo ya futuree sijui pana nini kati ya spidi na future.

ila tu ninchoamini ya kuwa Mtume alisafiri na kuona future kwa taufiqi ya Mola mlezi
Kaka sio tu alionyeshwa alikuwepo kwenye future hio na kuna mambo aliyafanya kuwaombea baadhi ya watu wa motoni..ninachokwambia alirudi dunian(Past) kutimiza Qadar.
Mf watu wengi wanachukulia katika angle moja tu baadhi ya hadithi ambazo mtume alikua akiwaambia alipokua msikitini kwake kuwa "Mtu atakae ingia sasa hivi ni mtu wa Peponi",
Alikua hatabiri bali maswahaba hao tayari alikuwa na ndani ya future...ila hakuweza kuzuia kifo chake kwa sababu kuwa mbele ya muda au nyuma ya muda hakubadilishi chochote kwenye Qadar ya Allah.
Mf ni Qadar ya Adam na Hawaa ilikua ni lazima kupitia juu ya uso wa dunia..future ya malaika kuwaona wanavyomwaga dam na kufanya ufisadi haikubadili chochote japo zilipita dahari na dahari hali ya kua ni sanam la udongo.
Mf huu niliokupa una maana hii wapo malaika na wanaadam ambao tayari wanaishi kwenye past zao na future zao.ila tunapitia present kutimiza kadar zetu.
 
JIDONDOFILA

JIDONDOFILA

Senior Member
Joined
Jan 8, 2013
Messages
176
Points
225
JIDONDOFILA

JIDONDOFILA

Senior Member
Joined Jan 8, 2013
176 225
Maswali yako mazuri. Kwanza naanza kwa utangulizi mfupi kisha nitakupa mifano na marejeo ya vitabu ukapitie na ninafanya hivyo ili kuepuka kukosea.

Mwanachuoni mkubwa aitwae Imaam Shawkaniy Allah amrehemu,alipata kusema hivi "Maneno ya Allah aliye juu haya pingani kwa yenyewe,na ukihisi au kuona yanapingana basi kitu cha kitu cha kwanza ituhumu akili yako kwa kushindwa kung'amua maana ya aya hizo au ituhumu elimu yako kwa kushindwa kuidiriki maana a aya husika"

Wanazuoni wengine wakafika mbali na kusema ya kuwa mpaka maneno ya mtume hayapingani kadhalika. Kutokana na hali hiyo,katika fani ya misingi ya tafsiri ya Qur'aan utakuta kipengele cha "Kupatanisha" (Reconcile) aya ili zilete maana moja na katika katika hadithi vile kuna upatanishaji wa hadithi,na hapa kuna mifano mingi.

Tukianza na suala ya siku za uumbaji,idadi kamili ni siku sita na hili limethibitishwa katika aya zote,bali kuna wale ambao hawakuelewa maandiko na kujitia wajuaji na kusema Qur'aan imesema uongo kwamba idadi ni siku nane,hapa wao wanaosema ni siku nane nio waongo,kwani kuna kuumba na kuweka,wao wakaona kuweka ni kuumba pia,hili la idadi ya siku za uumbaji nilishamjibu mtu mmoja humu.

Ama suala la kwanza la kusimama mbingu na dunia pasi na nguzo,hili kuna mapokezi nimepata kuyasikia ya kuwa kuna malaika ambao wamepewa kazi hiyo ya kushikilia mbingu na ardhi na hawa hawawezi luwa nguzo kama mtu akisema hao ni badala ya nguzo. Hili nitalifatilia ili kuona mapokezi hayo wanazuoni wameyapatanisha vipi wakapata jibu moja.

Nakupa mfano mmoja,kuna hadithi zimepokewa katika maana tofauti kutokana na matukio aliyo fanya mtume,hapa sitakunukulia matini bali nakupa maana,kuna hadithi moja ilionyesha ya kuwa mtume wa Allah amani iwe juu yake alisema mtu ukishika utupu udhu umetenguka,lakini kuna mapokezi mengine mtume alionekana eshika utupu wake lakini akasali bila ya kushika udhu,sasa mapokezi haya wanazuoni walivyoyapatanisha wakapata jibu moja ya kuwa "Mtu ukishika tupu yako kwa matamanio udhu unakutoka", kwa maana yanakuwa yamefanyiwa kazi mapokezi yote mawili.

Allah anajua zaidi,na popote nilipokosea basi ni kwa udhaifu ila Allah ahusiki na makosa hayo na ukamilifu ni wake.
M/mungu akuzidishie maarifa inshallah ila bado nadhani hatujawa pamoja..
1.Nimekueleza vitu ambavyo ni mutashabiha sio kwa Allah sw ila kwa sisi wanaadam.
Kuhusu siku za uumbaji sikukusudia kama zilivyoelezwa ndani ya Qur an .yaan baada ya majumuisho mbili mbingu mbili ardhi na nne viumbe hai na vyoote vinavyoonekana na visivyoonekana..sikukusudia hilo maana limeishajibiwa na qur an yenyewe allah aliposema kuwa "hawakuona makafiri kua mbingu na Ardhi vilikua kitu kimoja kisha Tukavibandua"sayansi imethibiti kwa Thiori ya Big bang..sikumaanisha hivyo.nilimaanisha hivi kabla ya uumbaji hakukua na jua wala hii dunia kwa hio usiku na mchana haukuwepo.hivyo ni siku zipi zilizotumika...ndio sbb nikakwambia kitu hicho mutashabiha..
2.swala LA mbingu kussimama bila nguzo ni lenye kutatanisha ndio sababu linaingia kwenye mambo ambayo ni mutashabiha.
3,niongezee Mtume (saw) alipoenda Safari ya Miraji Alimuona Allah sw au Hakumuona.
 
Amiin, Allah atuzidishie sote elimu na maarifa katika dini.

Hapa niseme sasa wewe ndio hunielewi mimi ila unacho kizungumzia ndio nilicho kielezea mimi na nimekupa msingi wa wanachuoni ambao huwa wanautumia kupata maana moja ya maandiko ambayo watu uhisi yana utata au kupingana.

Nukta zote unazozitoa weww laiti kama ungeelewa nilicho kiandika usinge uliza tena maswali haya. Hizo nukta tatu hazina utata,ndio maana nilinukuu kauli ya Imaamu ash Shawkaniy.

Msingi wa hoja zako ni utata katika maandiko na huu ndio msingi wangu pia,nikakwambia maandiko hayana utata bali ni elimu yako kuwa ndogo.

Nakuuliza wewe,suala mbingu kusimama bila nguzo utata wake uko wapi ? Na je kuna andiko lolote linapingana na hilo ? Na kama linapingana wewe huwa unaumia njia gani kuondokewa na utata huo ?

Mtume hakumuona Allah alipoenda Miiraji.

Pili,nakusahihisha usilinganishe kitendo cha Allah aliye juu kuibabandua dunia na mbingu ukalinganisha na Big Bang Theory hivi ni vitu kando kabisa. Labda kama uwe huijui hii nadharia vizuri.

Kabla ya uumbaji alikuwepo Allah peke yake. Na akasema Allah aliye juu :

36. Hakika idadi ya miezi kwa Mwenyezi Mungu ni miezi kumi na mbili katika hukumu ya Mwenyezi Mungu tangu alipo umba mbingu na ardhi. Katika hiyo iko mine mitakatifu. Hiyo ndiyo Dini iliyo sawa. Basi msidhulumu nafsi zenu humo. Na piganeni na washirikina wote kama wao wnavyo pigana nanyi nyote. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu yu pamoja na wachamngu. (at Tawbah : 36)
 
Z

Zurri

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2018
Messages
9,520
Points
2,000
Z

Zurri

JF-Expert Member
Joined Apr 6, 2018
9,520 2,000
sikumaanisha hivyo.nilimaanisha hivi kabla ya uumbaji hakukua na jua wala hii dunia kwa hio usiku na mchana haukuwepo.hivyo ni siku zipi zilizotumika...ndio sbb nikakwambia kitu hicho mutashabiha..
Kaka naomba nikusaidie kitu kimoja,huu utata unaojaribu kuuleta ni kutokana na wewe kuhoji au kujiuliza ila hujatoa andiko lolote linalo onyesha utata huo. Hili ni tatizo lako binafsi na linaonyesha kuna misingi umekosa misingi ya elimu bali una uchache wa maarifa juu ya Mola wako na maumbile,hizi huwa tunaziita "Talibisaat" kwa wingi na "Talibis" kwa umoja na mara nyingi huletwa na Shetani. Ukisoma kitabu kiitwacho "Talbisi Ibilis" cha Imaamu Ibnul al Jawziy utaona.

Unachotakiwa kujua ni kuwa Allah hafungwi na wakati,na muda ni miongoni mwa viumbe vyake,ndio maana tukaambiwa kwake yeye siku moja ni sawa miaka elfu moja,na jua na mwezi kwetu sisi na kuwepo kwa usiku na mchana ni kwa ajili ya kujua idadi ya miaka na kudhibiti mahesabu.

Kwahiyo aya hazina utata bali utata unatokana na wewe kuwa na maarifa machache.

Pili,naomba nikuulize swali la msingi sana,huwa unatumia Tafsiri gani miongoni mwa Tafsiri za Qur'aan. Naomba untajie jina la Tafsiri na muandishi wake.
 
JIDONDOFILA

JIDONDOFILA

Senior Member
Joined
Jan 8, 2013
Messages
176
Points
225
JIDONDOFILA

JIDONDOFILA

Senior Member
Joined Jan 8, 2013
176 225
Amiin, Allah atuzidishie sote elimu na maarifa katika dini.

Hapa niseme sasa wewe ndio hunielewi mimi ila unacho kizungumzia ndio nilicho kielezea mimi na nimekupa msingi wa wanachuoni ambao huwa wanautumia kupata maana moja ya maandiko ambayo watu uhisi yana utata au kupingana.

Nukta zote unazozitoa weww laiti kama ungeelewa nilicho kiandika usinge uliza tena maswali haya. Hizo nukta tatu hazina utata,ndio maana nilinukuu kauli ya Imaamu ash Shawkaniy.

Msingi wa hoja zako ni utata katika maandiko na huu ndio msingi wangu pia,nikakwambia maandiko hayana utata bali ni elimu yako kuwa ndogo.

Nakuuliza wewe,suala mbingu kusimama bila nguzo utata wake uko wapi ? Na je kuna andiko lolote linapingana na hilo ? Na kama linapingana wewe huwa unaumia njia gani kuondokewa na utata huo ?

Mtume hakumuona Allah alipoenda Miiraji.

Pili,nakusahihisha usilinganishe kitendo cha Allah aliye juu kuibabandua dunia na mbingu ukalinganisha na Big Bang Theory hivi ni vitu kando kabisa. Labda kama uwe huijui hii nadharia vizuri.

Kabla ya uumbaji alikuwepo Allah peke yake. Na akasema Allah aliye juu :

36. Hakika idadi ya miezi kwa Mwenyezi Mungu ni miezi kumi na mbili katika hukumu ya Mwenyezi Mungu tangu alipo umba mbingu na ardhi. Katika hiyo iko mine mitakatifu. Hiyo ndiyo Dini iliyo sawa. Basi msidhulumu nafsi zenu humo. Na piganeni na washirikina wote kama wao wnavyo pigana nanyi nyote. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu yu pamoja na wachamngu. (at Tawbah : 36)
Nadhani tofauti iliopo kati yangu na wewe ni wakimantik zaidi..Ninakuelewa..ila kiukweli sijatosheka na sababu kubwa ya Mimi kutotosheka nikua nimeisahau kabisaa Aya inayozigawa aina za aya zilizopo ndani ya qur an...nimekumbuka aina 2 tu.Mutawatil na Mutashabiha ya 3 nimeisahau na aya yenyewe pia nimeisahau..ningejenga msingi wa tofauti yangu na yako kupitia aya hio..
"Itoshe tu kusema kua "Kwa hakika M/mungu alikua nae yu vilevile alivyokua kabla hajaumba mambo haya. Inshallah nikikumbuka nitajenga hoja hii.
 
Forum statistics

Threads 1,336,215
Members 512,562
Posts 32,530,918
Top