Time Traveling: Je, linaweza kuwa suluhisho la kifo?

Da'Vinci

Da'Vinci

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2016
Messages
20,027
Points
2,000
Da'Vinci

Da'Vinci

JF-Expert Member
Joined Dec 1, 2016
20,027 2,000
hqdefault-1-jpg.1102207

SALUTE
Mara nyingi hua nasema vitu tunavyoona ni vyakijinga havi-make sense machoni na masikioni mwetu ndio hua na maana na vimeleta mabadiriko makubwa duniani kwetu. Mfano swali la kijinga zaidi alilowahi kujiuliza mwanasayans Issac Newton leo hii limetulitea mabadiriko na maendeleo kwenye maisha , hebu fikiria kama leo hii isac newton angekuuliza kwanini apple limemuangukia kichwani halikwenda juu ungemuona vipi? Hilo swali unaloliona la kijinga limeleta maendeleo makubwa sana. Pia ndoto moja aliyoota albert Einstein waweza kuona ni ya kawaida sana au haina maana lakini ni moja kati ya ndoto iliyoleta mafanikio makubwa duniani, kupitia ndoto tu ya kawaida sana aliyoota tulipata kitu kinachoitwa Theory of Ralativity mambo ya Emc2 yote yote unaweza ona ni kitu cha kawaida ila kina impact kubwa kwenye tasnia ya sayansi

Tarehe 11/5/2019 nilibahatika kuangalia muvi hii inayoitwa Avangers: Endgame, content iliyomo kwenye muvi hii ni Time Traveling, baada ya kuangalia muvi I really admitted that Death might no longer a threat to Mankind!.. Baada ya thanos ku-wipe nusu binaadamu wote ulimwenguni (Universe) , njia pekee iliyobakia kutimka ili kuwarudisha wale waliopotea. Probably Human can stop his Destiny which is Death, Nawaza tu labda Binaadamu twaweza kukiepuka na kukizuia kifo kwa kutumia Theory ya Time Traveling.

Time Travel ni nini..?

Ni kitendo cha kusafiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine ndani ya muda, namaanisha kua mtu anaweza kusafiri leo hii kwenda miaka 5,10,20,25 nk ijayo (Future) au kusafiri kurudi miaka 10,20,30,40,nk iliyopita (Past). Hadithi nyingi za zamani zimekua zikielezea swala hili la kusafiri katika muda.

Huko India kuna hadithi inamzungumzia mfale Raivata Kakudumi ambae alisafiri kwenda mbinguni kukutana na mung wake Brahma, aliporudi alishangaa kua ni miaka mingi imepita. Japan pia kuna hadithi inaitwa Nihongi, inamwelezea kijana mmoja mvuvi anayeitwa Urashima taro ambae alitembelea sehemu iliyochini ya maji, baada ya siku tatu alirudi kijijini kwake akakuta ni miaka 300 imepita, alikuta familia yake imefariki yote. Pia kwa wayahudi mnamo karne ya 1BC mwanafunzi aitwae Honi ha-M'agel inasemekana ailisinzia kwa muda wa miaka 27 alipoamka alikuta hakuna mtu aliyemjua sehemu aliyokua anaishi. Na simulizi nyingii sana kuhusu hii nadharia zimetolewa waweza tafuta ukasoma zaidi.

Wakati watu wengi wakidhani kua muda hautofautiani lakini Mwanasayansi Albert Einstein anaelezea kua muda (Time) haupo hivyo wanavyodhani, unaweza kutofautiana kwa mazingira tofauti, kutegemeana na kasi unayotembea nayo angani (in space)…Theory of special relative ya Enstein inasema kua muda kwenda haraka au kwenda taratibu inategemea na kasii unavyo safiri, mtu akisafiri kwa kasi ya mwanga kwa chombo cha anga angani umri wake utakua mdogo kulinganisha na ndugu au wazazi wake aliowaacha angani..kama akirudi yeye atakua kijana lakini nduguze watakua wamezeeka au wakawa wameshafariki.

Pia kwenye theory ya Albert Einstein ya Theory of General relativity anaelezea kua Garvity (kani ya uvutano) inaweza kupeleka muda mbele au kurudisha nyuma. Anaeleza kua chombo cha anaga kikiwa huko anagani kikakutana na kani ya uvutano basi hua kani hiyo husababisha muda kua slow, hivyo basi hata wanasayansi wa anaga wanakubali kua wasafiri wa anga wanaporudi duniani hua wapo nyuma kimuda yaani saa ya duniani inakua mbele kwa muda microsecond 38 kwa siku. Wanahitimisha kwa kusema mfano msafiri mmoja wa anaga ana pacha wake duniani ammbae hafu akikaa huko angani labda siku 14, Yule pacha aliyebaki duniani atamshinda kwa muda wa microsecond 532 (chukua Microsecond 38 zidisha siku 14)TIME MACHINE

Ili kufanikisha kusafiri katika muda inabidi kuwe na kifaa kinachoiitwa Time machine ambacho hichi kifaa kinauwezo wa kupeleka muda mbele au kurudisha muda nyuma. Bado wanasayansi wanalifanyia kazi suala hili, muda sio mrefu inaweza kuthibishwa kua Time machine inaweza kuanza kufanya kazi. Jinsi Nadharia ya Time Machine inavyofanya kazi kiukweli inanishinda kuielezea kwa Kiswahili kutokana na Ambiguity ya lugha yetu hii. Humo ni masuala ya physics tu so nashindwa niwekeje kwa lugha yetu labda aliyesoma hii kitu akaelewa inavyofanya kazi atatuelezea lifecoded.

Kwenye hili suala la tme Travel kuna kitu kinaitwa Grandfather Paradox ambapo hiki ni kitendo ambacho Time Traveller anarudi kwenye wakati uliopita kisha anaua wazazi wake au babu zake ili yeye awe hakuzaliwa.Kwa mujibu wa wanasayansi na wanafalasafa kama Plato kwenye theory yake ya Platonism anasema kua kubadili maisha yako ya nyuma hakuwezi kuathiri maisha yako ya sasa, lakini mambo yote hayo mawili yanakuja kupingwa na nadharia ya Butterfly Effectt ambapo inasema kua mabadiriko kidogo kwenye sehemu moja yanaweza kuleta mabadiriko makubwa au utofauti mkubwa baadae katika sehemu nyingine

Hii inamaanisha kwamba kama time traveler akirudi katika maisha yaliyopita akamuua baba aua babu yake anaweza sababisha mabadiriko katika maisha yake aliyotoka au future yake.

Kwa muhtsari huu kuhusu theory ya Time Traveling iko hivo japo watafiti wengi wanasema Time Travel hauwezekani iko too theoretically ila mimi naona hiki kitu ni real kabisa kipo, kwanini? Unajua binaadamu hawezi kufikiri nje ya vitu ambavyo vipo duniani nikimaanisha kua hata mimi au wewe hatuwezi kuwaza au kufikiri nje ya vile vitu tulivyoviona,kuambiwa au viliwahi kuwepo. Utawaza Mungu kwakua ulisikia kua kuna Mungu, utawaza nyumba kwakua ushaiona nyumba nk nk. Mantiki yangu ni kwamba hata hao watu wanaosema time travel is real hawakukaa tu wakafikiri kitu amabacho hakipo, mtazamo wangu naamini hiki kitu kipo na kinafanya kazi labda kwa siri kumbuka hata Internet tunaambiwa imeletwa mwaka 1991 na Tim Berners lee lakini ni kitu kipo toka miaka ya 1950s sema Tim aliifanya kua Popular baada ya kutengeneza World Wide Web…

Lakini haya ni mawazo yangu tu kwamba labada kama Time Machine ikifanikiwa kutengenezwa watu wanaweza kuitumia kukwepa kifo labda kwa kurudisha muda nyuma na kukwepa kile kitu kilichopelekea kufariki..kwa mafano kwenye muvi inaitwa Time Trveler’s wife wameelezea tukio hili linavyoweza kufanyika.
~Da'vinci..
 
Waterbender

Waterbender

Senior Member
Joined
Oct 2, 2018
Messages
120
Points
195
Waterbender

Waterbender

Senior Member
Joined Oct 2, 2018
120 195
Simple dissagree ndio hua nakataa.. mimi napenda kama unabisha unakuja na fact mkuu
Wale physicist walio tengeneza meli ma maginetics field ili wasionekane kwenye ladaa ya maadui walikuwa hawajui kama wanatengeneza mfano wa time machine kilicho wakumba ni matatizo tu meli ilikuwa inshift places but within the sametime vichaa wakuyosha vifo wengine hawakurudi na vilema, time travels is something natural na sio artificial
 
Bhagavan

Bhagavan

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2017
Messages
1,372
Points
2,000
Bhagavan

Bhagavan

JF-Expert Member
Joined Oct 28, 2017
1,372 2,000
Wale physicist walio tengeneza meli ma maginetics field ili wasionekane kwenye ladaa ya maadui walikuwa hawajui kama wanatengeneza mfano wa time machine kilicho wakumba ni matatizo tu meli ilikuwa inshift places but within the sametime vichaa wakuyosha vifo wengine hawakurudi na vilema, time travels is something natural na sio artificial
Hii kitu hata mimi niliwaza hivyo, kuna uwezekano Time Travel ipo ila kiroho zaidi, sina ujuzi sana wa mambo haya lakini nawaza huenda ikawa ipo hivyo na ndio maana huwezi kubadilisha tukio lolote zaidi utakuwa mtazamaji wa matukio yaliyotokea miaka hiyo.
 
Waterbender

Waterbender

Senior Member
Joined
Oct 2, 2018
Messages
120
Points
195
Waterbender

Waterbender

Senior Member
Joined Oct 2, 2018
120 195
Hii kitu hata mimi niliwaza hivyo, kuna uwezekano Time Travel ipo ila kiroho zaidi, sina ujuzi sana wa mambo haya lakini nawaza huenda ikawa ipo hivyo na ndio maana huwezi kubadilisha tukio lolote zaidi utakuwa mtazamaji wa matukio yaliyotokea miaka hiyo.
Na mara nying wanarudig nyuma na sio kwenda mbele
 
rip faza_nelly

rip faza_nelly

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2018
Messages
1,887
Points
2,000
rip faza_nelly

rip faza_nelly

JF-Expert Member
Joined Feb 19, 2018
1,887 2,000
Naam,
Philadelphia experiment iliwashinda na kusababisha crewmen kudata, ulemavu, vifo na wengine kujikuta miili yao imeungana na vyuma vya meli
Wale physicist walio tengeneza meli ma maginetics field ili wasionekane kwenye ladaa ya maadui walikuwa hawajui kama wanatengeneza mfano wa time machine kilicho wakumba ni matatizo tu meli ilikuwa inshift places but within the sametime vichaa wakuyosha vifo wengine hawakurudi na vilema, time travels is something natural na sio artificial
 
impongo

impongo

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2015
Messages
6,044
Points
2,000
impongo

impongo

JF-Expert Member
Joined Feb 18, 2015
6,044 2,000
mkuu kisa chako kimefanana na kilichomkuta na kaka angu mtoto wa mama mkubwa, yeye alienda kulala na kaka zake akapotea usiku huo. walitafuta kila kona ya nyumba walimkosa. majirani wamejaa alishaletwa hadi mtaalamu ndio akapatikana chini ya meza akiwa haongei yupo kama bubu.. yeye alisema alipelekwa ndani ya msufi!

Uchawi wa kiafrika ni teknolojia isiyo na manufaa kwetu ila wazungu kwao wanatumia kwa manufaa... Kwenye Intelligence,afya,ujenzi kote huko wao wana back up ya Magic ila sisi huku duuh. labda kulimishana
Sijui kwanini wenye taaluma hii wameshindwa kuifanya ya kisasa?
 
smigo4u

smigo4u

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2015
Messages
2,225
Points
2,000
smigo4u

smigo4u

JF-Expert Member
Joined Jun 19, 2015
2,225 2,000
Time travel fikiria km relocation through time, sio travelling km unatoka dar kwenda mwanza, ni physical relocation in time, au time and space, mfano sahv uko 2019 ila ikija kuwa possible kurelocate mwaka 1098 au 2020 unakuwa umesafiri through time na kuwepo physically ktk hiyo miaka na muda huo, so still theoretically not possible ila ikija kufanikishwa itaruhusu objects na individuals kufanya hayo,
"why there are no tourists from the future?"
 
Wordsworth

Wordsworth

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2019
Messages
342
Points
1,000
Wordsworth

Wordsworth

JF-Expert Member
Joined Jan 14, 2019
342 1,000
Umetishaa sana aisee, big up to you... Wadada zetu wanafatiliaga Kyle jenner/Kardashians wakati na uwigo mkubwa sana of very interesting subjects..
Kuna series inaitwa Bing Bang theory napenda wana yo discuss hizi concepts in a very scientific way
Yaani hadi hao Kardashians nawafuatilia. Hamna nisichofuatilia.
Hiyo Big Bang theory nikajua ipo kama Parks and Rec kumbe ni scientific hivyo? Nitaifuatilia.
 
Wordsworth

Wordsworth

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2019
Messages
342
Points
1,000
Wordsworth

Wordsworth

JF-Expert Member
Joined Jan 14, 2019
342 1,000
"why there are no tourists from the future?"
Are you sure?
And what is so special about 2019 or this decade over other years, that a time tourist should visit?
What if time travel in the future is not some leisurely activity and it's highly restricted?
 
Kiranga

Kiranga

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2009
Messages
43,468
Points
2,000
Kiranga

Kiranga

JF-Expert Member
Joined Jan 29, 2009
43,468 2,000
According to Einsteins Relativity, one needs to travel faster than the speed of light in a vacuum to go back in time.

But even for an infinitesimally small subatomic particle, the speed of light is the speed limit of this universe.

As something approaches the speed of light, no matter how small its mass, the energy it needs to move it furtheqr approaches infinity.

So, in order to transport even the smallest imaginable mass back in time, one will need infinite energy

That is why, according to Einstein's Relativity, time travel to the past is not possible.
 
Da'Vinci

Da'Vinci

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2016
Messages
20,027
Points
2,000
Da'Vinci

Da'Vinci

JF-Expert Member
Joined Dec 1, 2016
20,027 2,000
According to Einsteins Relativity, one needs to travel faster than the speed of light in a vacuum to go back in time.

But even for an infinitesimally small subatomic particle, the speed of light is the speed limit of this universe.

As something approaches the speed of light, no matter how small its mass, the energy it needs to move it furtheqr approaches infinity.

So, in order to transport even the smallest imaginable mass back in time, one will need infinite energy

That is why, according to Einstein's Relativity, time travel to the past is not possible.
How about the future????????
 
Kiranga

Kiranga

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2009
Messages
43,468
Points
2,000
Kiranga

Kiranga

JF-Expert Member
Joined Jan 29, 2009
43,468 2,000
How about the future????????
Time travel to the future is possible.

It can be arranged to be essentially governed by time dilation due to the difference between to frames of reference, one supposedly stationary (such as the earth) and another moving near relativistic speeds.

If one were to go to Alpha Centauri, our neighbouring star system, at speeds approaching the speed of light in a vacuum, the time dilation effect could make it such that, to the person on the spaceship, the trip could take only 10 years, going and returning to earth, while on earth a much longer time, perhaps 100 years will have passed.

The exact time dilation chart is given in the link below.

The person making this trip will age only by 10 years, the passage of time on the spaceship will only be 10 years, while on earth, upon returning, he will possibly be around the same age as his grandchildren. If his children are surviving, they will possibly be older than their father.100 years will have passed on earth.

Still, achieving this, while not impossible, is nearly impossible by current technology due to the huge energies and technological challenges.

The more exact time dilation chart is below.

 

Forum statistics

Threads 1,304,176
Members 501,290
Posts 31,505,290
Top