Time Traveling: Je, linaweza kuwa suluhisho la kifo?

Da'Vinci

Da'Vinci

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2016
Messages
20,029
Points
2,000
Da'Vinci

Da'Vinci

JF-Expert Member
Joined Dec 1, 2016
20,029 2,000
hqdefault-1-jpg.1102207

SALUTE
Mara nyingi hua nasema vitu tunavyoona ni vyakijinga havi-make sense machoni na masikioni mwetu ndio hua na maana na vimeleta mabadiriko makubwa duniani kwetu. Mfano swali la kijinga zaidi alilowahi kujiuliza mwanasayans Issac Newton leo hii limetulitea mabadiriko na maendeleo kwenye maisha , hebu fikiria kama leo hii isac newton angekuuliza kwanini apple limemuangukia kichwani halikwenda juu ungemuona vipi? Hilo swali unaloliona la kijinga limeleta maendeleo makubwa sana. Pia ndoto moja aliyoota albert Einstein waweza kuona ni ya kawaida sana au haina maana lakini ni moja kati ya ndoto iliyoleta mafanikio makubwa duniani, kupitia ndoto tu ya kawaida sana aliyoota tulipata kitu kinachoitwa Theory of Ralativity mambo ya Emc2 yote yote unaweza ona ni kitu cha kawaida ila kina impact kubwa kwenye tasnia ya sayansi

Tarehe 11/5/2019 nilibahatika kuangalia muvi hii inayoitwa Avangers: Endgame, content iliyomo kwenye muvi hii ni Time Traveling, baada ya kuangalia muvi I really admitted that Death might no longer a threat to Mankind!.. Baada ya thanos ku-wipe nusu binaadamu wote ulimwenguni (Universe) , njia pekee iliyobakia kutimka ili kuwarudisha wale waliopotea. Probably Human can stop his Destiny which is Death, Nawaza tu labda Binaadamu twaweza kukiepuka na kukizuia kifo kwa kutumia Theory ya Time Traveling.

Time Travel ni nini..?

Ni kitendo cha kusafiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine ndani ya muda, namaanisha kua mtu anaweza kusafiri leo hii kwenda miaka 5,10,20,25 nk ijayo (Future) au kusafiri kurudi miaka 10,20,30,40,nk iliyopita (Past). Hadithi nyingi za zamani zimekua zikielezea swala hili la kusafiri katika muda.

Huko India kuna hadithi inamzungumzia mfale Raivata Kakudumi ambae alisafiri kwenda mbinguni kukutana na mung wake Brahma, aliporudi alishangaa kua ni miaka mingi imepita. Japan pia kuna hadithi inaitwa Nihongi, inamwelezea kijana mmoja mvuvi anayeitwa Urashima taro ambae alitembelea sehemu iliyochini ya maji, baada ya siku tatu alirudi kijijini kwake akakuta ni miaka 300 imepita, alikuta familia yake imefariki yote. Pia kwa wayahudi mnamo karne ya 1BC mwanafunzi aitwae Honi ha-M'agel inasemekana ailisinzia kwa muda wa miaka 27 alipoamka alikuta hakuna mtu aliyemjua sehemu aliyokua anaishi. Na simulizi nyingii sana kuhusu hii nadharia zimetolewa waweza tafuta ukasoma zaidi.

Wakati watu wengi wakidhani kua muda hautofautiani lakini Mwanasayansi Albert Einstein anaelezea kua muda (Time) haupo hivyo wanavyodhani, unaweza kutofautiana kwa mazingira tofauti, kutegemeana na kasi unayotembea nayo angani (in space)…Theory of special relative ya Enstein inasema kua muda kwenda haraka au kwenda taratibu inategemea na kasii unavyo safiri, mtu akisafiri kwa kasi ya mwanga kwa chombo cha anga angani umri wake utakua mdogo kulinganisha na ndugu au wazazi wake aliowaacha angani..kama akirudi yeye atakua kijana lakini nduguze watakua wamezeeka au wakawa wameshafariki.

Pia kwenye theory ya Albert Einstein ya Theory of General relativity anaelezea kua Garvity (kani ya uvutano) inaweza kupeleka muda mbele au kurudisha nyuma. Anaeleza kua chombo cha anaga kikiwa huko anagani kikakutana na kani ya uvutano basi hua kani hiyo husababisha muda kua slow, hivyo basi hata wanasayansi wa anaga wanakubali kua wasafiri wa anga wanaporudi duniani hua wapo nyuma kimuda yaani saa ya duniani inakua mbele kwa muda microsecond 38 kwa siku. Wanahitimisha kwa kusema mfano msafiri mmoja wa anaga ana pacha wake duniani ammbae hafu akikaa huko angani labda siku 14, Yule pacha aliyebaki duniani atamshinda kwa muda wa microsecond 532 (chukua Microsecond 38 zidisha siku 14)TIME MACHINE

Ili kufanikisha kusafiri katika muda inabidi kuwe na kifaa kinachoiitwa Time machine ambacho hichi kifaa kinauwezo wa kupeleka muda mbele au kurudisha muda nyuma. Bado wanasayansi wanalifanyia kazi suala hili, muda sio mrefu inaweza kuthibishwa kua Time machine inaweza kuanza kufanya kazi. Jinsi Nadharia ya Time Machine inavyofanya kazi kiukweli inanishinda kuielezea kwa Kiswahili kutokana na Ambiguity ya lugha yetu hii. Humo ni masuala ya physics tu so nashindwa niwekeje kwa lugha yetu labda aliyesoma hii kitu akaelewa inavyofanya kazi atatuelezea lifecoded.

Kwenye hili suala la tme Travel kuna kitu kinaitwa Grandfather Paradox ambapo hiki ni kitendo ambacho Time Traveller anarudi kwenye wakati uliopita kisha anaua wazazi wake au babu zake ili yeye awe hakuzaliwa.Kwa mujibu wa wanasayansi na wanafalasafa kama Plato kwenye theory yake ya Platonism anasema kua kubadili maisha yako ya nyuma hakuwezi kuathiri maisha yako ya sasa, lakini mambo yote hayo mawili yanakuja kupingwa na nadharia ya Butterfly Effectt ambapo inasema kua mabadiriko kidogo kwenye sehemu moja yanaweza kuleta mabadiriko makubwa au utofauti mkubwa baadae katika sehemu nyingine

Hii inamaanisha kwamba kama time traveler akirudi katika maisha yaliyopita akamuua baba aua babu yake anaweza sababisha mabadiriko katika maisha yake aliyotoka au future yake.

Kwa muhtsari huu kuhusu theory ya Time Traveling iko hivo japo watafiti wengi wanasema Time Travel hauwezekani iko too theoretically ila mimi naona hiki kitu ni real kabisa kipo, kwanini? Unajua binaadamu hawezi kufikiri nje ya vitu ambavyo vipo duniani nikimaanisha kua hata mimi au wewe hatuwezi kuwaza au kufikiri nje ya vile vitu tulivyoviona,kuambiwa au viliwahi kuwepo. Utawaza Mungu kwakua ulisikia kua kuna Mungu, utawaza nyumba kwakua ushaiona nyumba nk nk. Mantiki yangu ni kwamba hata hao watu wanaosema time travel is real hawakukaa tu wakafikiri kitu amabacho hakipo, mtazamo wangu naamini hiki kitu kipo na kinafanya kazi labda kwa siri kumbuka hata Internet tunaambiwa imeletwa mwaka 1991 na Tim Berners lee lakini ni kitu kipo toka miaka ya 1950s sema Tim aliifanya kua Popular baada ya kutengeneza World Wide Web…

Lakini haya ni mawazo yangu tu kwamba labada kama Time Machine ikifanikiwa kutengenezwa watu wanaweza kuitumia kukwepa kifo labda kwa kurudisha muda nyuma na kukwepa kile kitu kilichopelekea kufariki..kwa mafano kwenye muvi inaitwa Time Trveler’s wife wameelezea tukio hili linavyoweza kufanyika.
~Da'vinci..
 
Da'Vinci

Da'Vinci

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2016
Messages
20,029
Points
2,000
Da'Vinci

Da'Vinci

JF-Expert Member
Joined Dec 1, 2016
20,029 2,000
Maelezo kidogo. Me najuaga ni movie wala hayana uhalisia
Kama unaangalia muvi tu kama muvi hivyo huwezi kuona kama ni ukweli.. iko hivi

Vampires hawezi kuzalisha kiasi cha kutosha cha hemoglobinhivyo inawafanya waipate kwa kunywa damu ya binaadamu.wanafanya hivo kwakua damu hiyo yenye haemoglobin inawafanya waweze kupata nishati mwilini mwao ili waweze kuishi. Lakini pia inasemekana kua huwa wanakunywa damu ili ku-extract vitamin D ambayo ipo kwenye damu ya binaadmu ambayo vitamin D hiyo sisi twaipata kwenye mwanga wa jua, kumbuka Vampire hawawezi kukaa kwenye mwanga wa jua kwakua jua inawakilisha nguvu ya Mungu, pia huogopa sana Msalaba,maji ya baraka na silver. Vampire mara nyingi walitoka na wafu ambao waliuawa kwa ajil ya kwenda kinyume na kanisa
 
troublemaker

troublemaker

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2015
Messages
7,216
Points
2,000
troublemaker

troublemaker

JF-Expert Member
Joined Jun 8, 2015
7,216 2,000
Unataka kusema walikuwepo au wapo?
Kama unaangalia muvi tu kama muvi hivyo huwezi kuona kama ni ukweli.. iko hivi

Vampires hawezi kuzalisha kiasi cha kutosha cha hemoglobinhivyo inawafanya waipate kwa kunywa damu ya binaadamu.wanafanya hivo kwakua damu hiyo yenye haemoglobin inawafanya waweze kupata nishati mwilini mwao ili waweze kuishi. Lakini pia inasemekana kua huwa wanakunywa damu ili ku-extract vitamin D ambayo ipo kwenye damu ya binaadmu ambayo vitamin D hiyo sisi twaipata kwenye mwanga wa jua, kumbuka Vampire hawawezi kukaa kwenye mwanga wa jua kwakua jua inawakilisha nguvu ya Mungu, pia huogopa sana Msalaba,maji ya baraka na silver. Vampire mara nyingi walitoka na wafu ambao waliuawa kwa ajil ya kwenda kinyume na kanisa
 
Da'Vinci

Da'Vinci

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2016
Messages
20,029
Points
2,000
Da'Vinci

Da'Vinci

JF-Expert Member
Joined Dec 1, 2016
20,029 2,000
Hawafi wala hawazeeki na wanaishi hata miaka 500+
miaka ya 1400s/1500s waliwindwa sana na kanisa, kulikua na timu kabisa ya kupambana nao. kwa sababu siku hizi hawaonekani twaweza sema kua hawapo ila yawezekana twaishi nao. ni kama vile Ulaya/marekani ilivyoamua kutokomeza wachawi wote, twaweza kusema waliwamaliza wote kwakua hawonekani tena ila yawezekana wapo ukizingatia science ni Modern Magic
 
Alexism

Alexism

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2011
Messages
3,049
Points
2,000
Alexism

Alexism

JF-Expert Member
Joined Aug 14, 2011
3,049 2,000
Ila ukiangalia movie unaweza kutengeneza makara nzuri
 
Alexism

Alexism

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2011
Messages
3,049
Points
2,000
Alexism

Alexism

JF-Expert Member
Joined Aug 14, 2011
3,049 2,000
stephen hawking kwenye kitabu chake cha "brief answers to the Big Question "
ameelezea posibility ya Time Travell ni ndogo kwa sasa kutokea.........
mwaka 2009 alihost party kwa ajili ya time travell lakini hakuna aliyetokea hata mmoja,,,
hakutuma kadi za mwaliko until party ilivyoisha akiamini kama kuna time traveller wa ukweli wangekuja kwenye party....
siku ya party hakuna mtu aliyejitokeza kwenye party........
Yaani tuje tu hivi hivi
 
ABiClever Junior

ABiClever Junior

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2016
Messages
941
Points
1,000
ABiClever Junior

ABiClever Junior

JF-Expert Member
Joined Dec 14, 2016
941 1,000
Hivi ushawahi kufikiri kuwa bila ya kifo watu wote walio kufa wabgekuwepo dunian tungetosha?
 
impongo

impongo

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2015
Messages
6,044
Points
2,000
impongo

impongo

JF-Expert Member
Joined Feb 18, 2015
6,044 2,000
siwezi kukupa since ushasema kimeandikwa na wanadamu...so what is your point of truth then....??

Unaamini kwenye nini hasa mkuu....?? how is reality happening kama sio mental construct coz kila ukionacho ni illusion..hivi unajuwa ni kwanini reality ipo tofauti kwa kila mtu ..? means you perceive things differently from others.....ndo mana tunasema mind reality is basing on your creation of reality.....any way ni somo pana mkuu...sio rahisi kuelewana kirahisi kwa vibandiko vya hapa JF but ni somo mkuu.....wenye ulimwengu wanatucontrol kupitia hiyo mind manipulation coz ukiweza kumanipulate mind tayari ushahamisha reality mkuu...wanacheza na mind coz mind creates reality.....I dare to make you understand lakini ushajiwekea mentality ya kutokuelewa hilo so I fail to conquer your opinion...

Nasubiri Daku mkuu bado masaa 3 ,,karibu,
Kama ungeweka hicho kitabu ingesaidia Sana kutuweka katika wakati flani kugundua utofauti na kuufanyia kazi kwa viwango vyetu lakini usipo weka haujatutendea haki
Challenges ni mhimu ili kugundua mabadiriko
 
impongo

impongo

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2015
Messages
6,044
Points
2,000
impongo

impongo

JF-Expert Member
Joined Feb 18, 2015
6,044 2,000
not proven .....kuna posibility kuwa technology ni matokeo ya kuview future kisha kuendana na mfumo huo au kuoneshwa namna ya kufanya na watu waliopo mbele ya future yetu...kwa sababu higher realm ni future katika 3D realm...probably we are visited by leople from the future( higher dimension realm)..

We can't see the future kwa sababu the distinction in time can not be measured by time scale tunayoitumia....na ndo mana future inabaki kama another plane of realm...means we have to change into morphology to view the future likewise beings who are beyond our present time are viewing us in past like experience ndo mana wanakuja kutupa technolojia mpya.....

probably kuna beings wapo beyond our present time measuring scale tuliyonayo....ni kama unampa mtu ushauri ambaye yupo jana ila wewe upo leo since he hasn't seen today....inaweza ikawa hivo make Siri nyingi bado zipo closed...

ukienda huko Alaska marekani kuna kituo kinachotoa update za ulimwengu specifically dunia inavyokwenda hasa katika mambo ya tabia nchi na mambo mengine ...kituo hicho kinaitwa HAARP na kinatoa utaratibu jinsi dunia inavyoenda kuanzia updates za kesho au mwezi ujao na mpaka next year huku matukio yote yanakuwa yashaoredheshwa chronogically what is going to happen na ndo hapo hapo tunapata utabiri wa hali ya hewa....hayo ma kimbunga Isaak sijui nani yote yanakuwa predicted kupitia HAARP technology...

hivi bado watu hawaoni tunaview future kwa aina yake....kitendo
cha kujua tukio litakalo tokea kesho kutwa midaa flani ni kuview the future mkuu ,jamaaa hawataki kusema ukweli but technolojia hii ipo na inafanya kazi kwa siri sana.
Umeeleweka sana
 
impongo

impongo

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2015
Messages
6,044
Points
2,000
impongo

impongo

JF-Expert Member
Joined Feb 18, 2015
6,044 2,000
nikweli mkuu...you are right.....the future is determined by your imagination..we need something to explain this..whatever. you imagine is whta going. to manifest into physical form. of reality......


The mind (mental) through imagination is the engine of your future....nothing comes out without mental imagination..
Mkuu kuna kitu nakifanya hapa nikimaliza natamani tuliweke sawa hili jambo...life is illusion brought by mental construct unles perceived in reality.....reality is constructed by your mental....your mental mind creates your reality of your future....
Nilikuwa napita hii andiko ina kitu cha kufikirisha ubongo zaidi.
Some ancient myths depict a character skipping forward in time. In Hindu mythology, the Mahabharata mentions the story of King Raivata Kakudmi, who travels to heaven to meet the creator Brahma and is surprised to learn when he returns to Earth that many ages have passed

.[1] The Buddhist Pāli Canonmentions the relativity of time. The PayasiSutta tells of one of the Buddha's chief disciples, Kumara Kassapa, who explains to the skeptic Payasi that time in the Heavens passes differently than on Earth

.[2] The Japanese tale of "Urashima Tarō",

[3] first described in the Nihongi (720) tells of a young fisherman named Urashima Tarō who visits an undersea palace. After three days, he returns home to his village and finds himself 300 years in the future, where he has been forgotten, his house is in ruins, and his family has died.

.[4] In Jewish tradition, the 1st-century BC scholar Honi ha-M'agel is said to have fallen asleep and slept for seventy years. When waking up he returned home but found none of the people he knew, and no one believed his claims of who he was.[5
 

Forum statistics

Threads 1,304,792
Members 501,517
Posts 31,527,141
Top