de richman
Member
- Jul 2, 2021
- 7
- 5
nimevutiwa na maelezo mkuu.
sasa labda wewe kwa unavoelewa ili mtu usafiri uende kwenye past ufanyeje..?
je uwe na spidi kali sana ukitembea huko angani ?
au uwe na spidi kali ukitembea hapa duniani ?
naamini dunia in Mengi sana na hizi tafiti za wanasayansi zinazidi kuniongezea imani yangu juu ya DINI HII YA kiislamu.
maana ninaona kabisa kwamba kuna mambo ya aabu yapo katika uislamu ambayo najiuliza hao waliyoyanukuu walikuwa na ujasiri gani kunukuu ?
ina maana hawakuhofia kwamba watu watahisi ni uongo kama vile mtume muhammad kwenda miiraji n. k
kuna hadithi inasema "katik pepo kuna daraja mia, baina ya daraja na daraja katika hizo daraja mia upishano wake ni baina ya mbingu na ardhi "
mtu anawezakuona hizi ni stori za kutunga lkini hata wanasayansi sasa hivi wanatuambia kwamba hata umbali baina ya nyota moja na nyingine unaweza kufika KM 340000 sasa angalia kuna nyota ngapi huko juu na huo umbali baina ya nyota na nyota ?
pia wanasema watu wa astronomy ya kuwa kuna madudu makubwa huko juu ambayo ukubwa wake basi jua lijirudie siochini ya mara 1000(kwa uchache) ndo linaweza kufanana na hayo madudu.
kiufupi Uislamu umeeleza Mengi sana ambayo wanasayansi ndo wanatafuta sababu zao na kuzielezea hapo.
lakini mimi najikita sana na kufatilia mambo ya astronomy huko nazidi kuamini kwamb Qurani imetoka Kw Mungu.
yani inaonesha ya kuwa dunia ni kijitu kidogo sana katika uislamu.kwa sababu mifano inayppogwa na Mafundisho ya uislamu ni mifano ambayo mtu anaweza kuona ni kujikuza lakini ipo
ndo maana KIRANGA kila siku umu anasema icho mnachokiita kitabu kitakatifu quran ni kama hadithi za kipepe au ludilofa tu kwa maana kuna contraditions nyingi sanaKwanza kabisa mimi si sheikh na nipo katika kujifunza,maelezo yako nimeyasoma na nimeyaelewa vyema na nina uhakika kila unachokisema unamaanisha.
Na hapa hakuna kufichana lazima tuwekane wazi ili tufahamiane vizuri.
Mwanzo unakumbuka ulimgusia "Makarim Shirazi" ? Nikakuuliza swali wewe ni SHIA au umeamua kumfatilia huyo sheikh wa Kishia bila kujua ?
Muda huu umetaja suala la Ufalme na Usultani,hapa najua kabisa umemaanisha japokuwa hapakuwa na haja ya wewe kuweka kauli hiyo.
Sababu najua umemaanisha na mimi nakuuliza swali je Usultani na Ufalme ni jambo baya ? Je Uislamu unakataza Ufalme ? Kwanini umeiweka kauli hiyo hapa ? Je kulikuwa na haja ?
Haya unayoyasema yako sahihi na yapo na tunayaona.
Nakupata vizuri. Hivi visa navyovitoa ingekuwa vizuri kama ukiwa unaweka na marejeo,kama unavyonituhumu mimi ya kuwa siweki ushahidi.
Nakupata vizuri.
Uko sahihi kabisa.
Kaka elimu haitaki mja uwe kama sponchi lazima uchuje kipi cha kuchukua na kipi cha kuacha. Kama mwanachuoni mkubwa alipata kuathiriwa na mtu muovu vipi mimi ambae sina elimu,unamjua Imaamu Safarini ? Mwenye kitabu kiitwacho "Aqidat as Safariniyyah" ?
Sasa kama leo hii kuna watu wanaitakidi Jibril alifanya hiyana juu ya kupeleka ujumbe kwa mtume na alipaswa apelekewe Ali,huku ni kuitukana dini ya Uislamu,mtu ambae anasema mama Aisha ni mzinifu wakati Qur'aan imewatakasa wakeze mtume,na mtu ambae anaitakidi ya kuwa Qur'aan haijakamilikana iliyokamilika iko pangoni ? Hivi mtu huyu atakueleza nini katila Dini akawa mkweli ?
Kaka ukisoma katika kitabu cha Mukadima wa Sahihi Muslimu cha Imam Muslim ameelzea maneno ya Imamu Muhammad bin Sirrin akionyesha umuhimu wa kuwajua rijali katika mapokezi ya habari anazo nasibishwa nazo mtume,na hii ni baada ya kudhihiri fitna na akasema ya kuwa kuuliza juu sanadi ndio dini basi tuangalie wapi unachukua dini yako.
Mtume ameondoka ameacha Uislamu ukiwa safi na usiku wake ni sawa na mchana wake. Kaka siwezi kuchukua dini lwa mtu mzushi na muongo kama Jahmiyyah,Ashaira,Mu'tazila ambao wapo karibu sana kiitikadi na MASHIA,Maturudiya na wengineo katika makundi potofu.
Kaka bora wewe unione mimi sina maarifa ila sitaki kuichanganya Itikadi yangu na uchafu.
Kuna muda nilikugusia athari walizokuwa nazo wanazuoni wa dini ya USHIA kutokana na wao kujikita na Falsafa ikawapelekea kukana baadhi ya sifa za Allah.
Nakuuliza swali,hivi Qur'aan ni maneno ya Allah au ni kiumbe ?
Pili,utata uko wapi wakati jambo hili limeshawekwa wazi karne na karne na wanazuoi wa Tafsiri ? Ndio maana nilikuuliza unatumia tafsiri gani ? Sababu nilijua tu kama wewe sio SHIA basi umeathirika na USHIA. Sasa wewe si unasema au unahimiza juu ya utafiti,je ushawahi kusoma Tafsiri za Qur'aan nje ya Tafsiri za Kishia ? Na kama umesoma ni tafsiri zipi umesoma ? na kama hujasoma kwanini mimi unataka niwe huru wakati wewe hauko huru ?
Sasa,nenda kasome Tafsiri ya Imaam Ibn Kathiir iitwayo "Al Qur'aan Adhwiim" katika kuilezea aya hiyo ya pili ya surt ar Raadi,uone je hiyoaya ina utata au utata mnauweka nyinyi ?
Kaka kwanza ulitakiwa ujue ni kwa namna gani wanazuoni walivyopambana kwa idhni ya Allah juu ya kuihudumia Qur'aan na kuweka wazi aya zote zinazohisiwa na watu kwamba zina utata,rejea pia kitabu cha Imaamu Muhammad al Amiin ash Shanwitwiy kiitwacho"Dafu'u Ihami adh Twirab 'an Ayaat al Kitaab" pia rejea kitabu cha Mwanachuoni mkubwa wa Hadithi aitwae Abdul Muhsin al Abaad al Badr kiiteacho "Ayaat mutashabihaat al Alfadh fi Qur'aan al Kariim" na namna ya kuzitofautisha. Ili uone ya kuwa kila kitu kilishawekwa wazi muda mrefu na mnayoyaleta nyinyi ni Talbisat za kuwayumbisja watu kwa makusudi wakati mambo yako wazi na dalili ziko wazi ila hamzifati kwa makusudi.
Ile ya Ysuf Ali sio Tafsir,bali ni tarjama kwa lugha ya kiingereza,tafuta Tafsir za wanazuoni wakubwa ambao wamejea maana ya aya kwa mtume na maswahaba zake. Aya hizo zimewekwa wazi. Na hapo Yusif Ali hajatafsiri bali matini ya aya ndio yanasema hivyo.
Nakuuliza swali rahisi,sasa wewe baada ya kuona aya na ukadai kwamba ina utata,je ni wewe umeliona hilo au wanazuoni wako wameliona hilo ndio wewe ukakariri ?
Je baada ya kuhisi utata huo je ulisoma vitabu vya madhehebu ngapi za Uislamu juu ya aya hiyo na madhehebu hizo zimesema kwamba aya hiyo ina utata au ?
Je kabla ya wanazuoni wako je maimamu gani wa Kishia kati ya wale 12 walisema kwamba aya hiyo ina utata ? Je kama hakuna,wewe na maimamu wa Kishia nani mwenye elimu kubwa ?
Unajua kuna ujinga mwingine huwa mnajitakia tu,muonekane mnajua kuhoji wakati mnapotea,rudini katika asili kila kitu kipo.
Sababu nimeshakujua wewe ni nani kiitikadi,nakuuliza maswali kulingana na maelezo yako,je ina maana mpaka muda huu Allah hajamteua huyo mja wa kutoa huo utata ? Na kama bado wewe umejuaje hilo na unahisi huyo mja ni nani ? Al Mahdi au ? Jamaa acheni kudanganya watu,mtakuja kuulizwa kwa huu ujinga mnaoufanya mwa kuitukanisha dini ya Allah.
Hivi hata unachokiandika huwa unakihakiki ?
Kaka katika maelezo yangu humu nimekuuliza maswali kadhaa,naomba unijibu maswali yangu yote niliyokuuliza.
Pili,marejeo yote niliyokupa naomba ukayafatilie na uyasime kikamilifu.
Ninacho kukumbusha ni kuwa dini ya UISLAMU imekamilika na USHIA sio Uislamu bali ni dini pweke inayojitegemea na hakuna hata ibada moja ya kishia inayo fanana na ya Uislamu.
Kama kuna lolote nililokosea ni kwa udhaifu wangu na Allah aliye juu ametakasika na ukamilifu ni wake yeye.
siku mkifanikiwa kusolve hizo contradictions nyinyi kwa nyinyi basi KIRANGA atawaelewa lakin nyie wenyewe hamuelewani who is KIRANG mpaka hawaelewe ahahhahaha