Time hii CHADEMA hawajatupa msimamo wao kuhusu nani wanaomuunga mkono katika uchaguzi wa Kenya

sultan Ali Mohamed

New Member
Dec 20, 2021
1
0
Tumezoea miaka mingi ya uchaguzi Wakenya kuona chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kikituonesha ni mgombea yupi wa kiti cha urais wa Kenya wanaemuunga mkono, lakini safari hii tunaona wameshikwa na kigugumizi hawajui wamuunge mkono mgombea yupi nadhani hii inatokana na dalili zinazo onyesha kwamba chaguzi mkuu wa Kenya wa 2022 unaweza kuwa mgumu ukilinganisha na chaguzi zote zilizo pita huko nyuma na yote hiyo inatokana na Rais aliyepo madarakani kumuunga mkono mpinzani wake ambae anaushawishi wakisiasa katika chaguzi zote zilizo pita, na kumwacha makamu wake wa urais bwana William Rutto apambane kivyake, lakini kwa mujibu wa tafiti za hivi karibuni zinaonyesha wawili hao wote wanaushawishi mkubwa na kwamba kuna uwezekano mkubwa wa kugawanyika kwa kura na kupelekea kila mgombea kutofikisha %50 ya kura na kuleta taharuki katika nchi ya Kenya na Afrika kwa ujumla, sasa tungependa kuwasikia chadema wakisema lolote ama nani wanaomuunga mkono ikiwa kama ni vyama rafiki kama ambavyo wamekuwa wakifanya miaka mingine ya nyuma ili wafuasi wao pia wapate mwelekeo wa siasa za kenya kuelekea uchaguzi wa 2022


IMG_20220704_133256_928.jpg
 
Mbowe alipoachiwa kwenye kesi yake alikwenda kuonana na Raila Odinga kwa mazingira kama hayo huenda tukabashiri uelekeo
 
..pia hakuna waziri wa serikali ya Ccm aliyekwenda kumpigia kampeni mgombea mmojawapo wa uraisi huko Kenya.

..mtakumbuka Jpm aliwahi kupanda majukwaani huko Kenya kumpigia kampeni Raila Odinga.
 
Juzi juzi tu, ujumbe kutoka kwa Raila Odinga ukiongozwa na msemaji wa Azimio la umoja (Prof Makau Mutua) ulifika Dar na na kuonana na Mbowe isitoshe inafahamika urafiki wa serikali/familia ya Uhuru Kenyata kwa ndg Tundu Lissu. Bila shaka chadema iko na Raila

Sent from my Infinix X657C using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom