R.B
JF-Expert Member
- May 10, 2012
- 6,296
- 2,573
Kuwatenga wazawa suala la kuanzisha viwanda na kukumbatia vietnam ,china ,naliona anguko la awamu ya tano kama awamu ya 3 sekta ya viwanda.
Naona serikali ya awamu ya tano si rafiki wa wafanyabiashara wa kitanzania. Naona wametengwa wamekuwa wapweke , tukitegemea wageni .
Wazawa ni rahisi kuwa control , tumeona kwenye ukwepaji kodi wamerudisha pesa, swali je wangekuwa wageni hizo pesa zingerudishwa?
Naamini katika watanzania na wanaweza.
Tanzania ya viwanda hii hapa.
Wenye viwanda wazawa kwanza wachambuliwe historia zao , uzoefu wao katika biashara , ubinifu wao katika masoko ya tanzania. Wapewe mikoa na mitaji wafungue viwanda vya ubia na serikali. Hata wakiwa 7 wanatosha .
Mbona bakhresa ana viwanda nchi tano (kigali, kenya , zimbabwe, uganda ) mashamba zambia. Kwanini ashindwe kuvijenga tanzania. Awe anasafirisha bidhaa huko?
Ata uchumi wa marekani unaendeshwa kwa 1% ambao ndo matajiri.
Mfano.
Bakhresa, mo, nyati, tembo cement, asas, alsco holding . Wameshapanga kufungua viwanda kila jiji , proposal wanazo. Tatizo ni mtaji
Ni suala la waziri wa viwanda kuitisha proposal zao za uwekezaji za miaka 50.
Na serikali kuwadhamini katika benki ya kilimo .BOT Au biashara na kuwapa mtaji wa kununua viwanda hiyo kwa ubia na serikali ; serikali iwe ni 60, wazawa ni 30, 10 ni hisa za watanzania.
Sharti kuu wazawa(bakhresa, mo, nyati, tembo cement, asas, alsco holding .) Wapewe kuweka management. Serikali iwe watch dog.
Ata reli ya dar es salaaam ya abiria , wapewe wazawa kwa ubia na serikali 60 kwa 40 mzawa lakini awe mmoja ili kuondoa conflict. Na apewe kuweka management yake mzawa bila kuingiliwa. Serikali iwe watch dog kwa kutumia system .
Hii.
Serikali ipigane kwa kila hali hii, serikali isitake ubia suala la umeme ; ikae na wataalamu 100% izalishe umeme yenyewe kufikia mwaka huu iwe 15,000w badala ya sasa 1500w.
Hili litasaidia wenye viwanda kuwa na umeme wa uhakika , bila masharti na ni rahisi kunegosiate na serikali juu ya bei , kwani serikali itakuwa inamiliki umeme kwa kutumia kampuni yake 100%
Tanzania ya viwanda itakuwa ndoto kama umeme tutubinafsisha kama sasa, iptl ,pap n.k
Kuhusu suala la nyumba za bati ;
Rais , kiwanda kinauzwa 5,000,000(bati za kawaida) - 12,ooo,0000 (mabati ya kisasa) lete hivyo viwanda tawanya kwenye veta zote kila wilaya . Hizo veta ndo ziwe zina tengeneza na kuuza mabati.
Halmashuri zitenge fungu kwa ajiri ya kununua viwanda hivyo ; sio mpaka seikali kuu.
Ni mawazo kama mtanzania mwingine.