Tim clarke: Hatujaona mabadiliko kwa kipindi cha miaka 20 iliyopita | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tim clarke: Hatujaona mabadiliko kwa kipindi cha miaka 20 iliyopita

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kachanchabuseta, May 14, 2010.

 1. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #1
  May 14, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Baada ya kauli ya Mr Tim clarke kuwa hawajaona maendeleo yoyote kwa wakulima kwa kipindi cha miaka 20 iliyopita. Sirikali imeamka usingizini na kuwa mbogo kuanza kumuandama Mr Tim Clarke.

  Wakiojiwa wakulima wawili na Shirika la utangazaji la BBC wamekili kwamba bado hawajaona maendeleo yoyote umasikini unawaandama na kisema kwa sera ya KILIMO KWANZA NI KAULI YA KISIASA HAKUNA LOLOTE.

  WAnajF ni Miongo miwili sasa au nusu karne bado TANZANIA tunalia na njaa, TANZANIA INAELEKEA WAPI???
   
 2. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #2
  May 14, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,945
  Likes Received: 2,091
  Trophy Points: 280
  Serikali hii imeshindwa kazi hivyo waajili wake yaani wapiga kura wanahitaji kuliona hilo na kulifanyia kazi Oktoba 2010. Wanamjia juu bw. Tim, halafu baadaye wahisani wamepunguza msaada kwenye bajeti, je bw. Tim amekosea kweli kusema hawana lolote? Serikali hii haipendi kuambia ukweli, na baada ya kuambia ukweli baada ya muda wanakiri ukweli huo hapo ndipo utakapoona kuwa ni wazito kuelewa na kuona mambo!
   
 3. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #3
  May 14, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Hapa serikali itasema saaana
   
 4. M

  Magezi JF-Expert Member

  #4
  May 14, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Nimezaliwa miaka ya 1970s nikakuta wazazi wangu wanalima kwa jembe la mkono, leo mama yangu mzazi bado analima kwa jembe la mkono sasa hayo mabadiliko wanayodai CCM eti wameyaleta ktk kilimo yako wapi???

  Balozi yuko sahihi na nampongeza kwa kutusemea kwani watanzania hatuwezi hata kusema lile linalo tukera. Silaha kubwa ya serikali ya CCM tangu uhuru ni kushangilia uwongo na kuficha/kuchukia ukweli. Na mtu yeyote anayechukia ukweli hawezi pata maendeleo.
   
 5. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #5
  May 14, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Hapo utakuwa umewagusa mana ukisema ukweli watakuandama mpaka mwisho, jiulize kwanini kesi za EPA haziishi??
   
Loading...