Tikiti maji na maziwa ya mtindi

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,299
33,082
Kua kwenye diet kunafanya nitafute namna mbalimbali ya kula na kuenjoy vyakula ninavyovipenda.Bila kuharibu juhudi zangu za kupunguza uzito.

katika glasi ni mchanganyiko wa Maziwa mgando,tikiti maji na asali


Napenda sana tikiti maji lakini baada ya kula kwa wiki tatu mfululizo ladha yake imeanza kunichosha.leo katika juhudi za kumalizia kipande kilichobaki niliamua kulichanganya kwenye maziwa mgando.
Nimependa sana Ladha yake na nime-enjoy kula.Hii imenipa sababu yakuendelea kula tikiti maji kwa wiki nyingine moja ,uku nikiendelea kuongeza namna mbalimbali za kuenjoy tunda hili.

Mahitaji
  • Maziwa mgando-Nimetumia Tanga fresh
  • Asali
  • Tikiti maji-kata vipande vidogo
Njia

1.weka maziwa kwenye glasi ,ongeza asali kisha korogo ili kuchanganya.

2.chukua glasi nyingine weka vipande vichache vya kitiki maji kisha mimina maziwa kiasi.kisha weka tena matunda na uweke maziwa juu fanya hivyo adi glasi ijae

3.Mwisho kabisa kwa juu,weka vipande vya tikiti maji kisha Nyunyuzia asali.Weka frijini kwa muda kidogo ili iwe baridi.tayari kwa kula.

Maelezo ya ziada

sikuweka vipimo kamili,kua huru kuweka kiasi utakacho.Kwa wale wenzangu tunaopunguza

uzito,jali kiasi cha maziwa unayokunywa na kiasi cha asali unachotumia.Nashauri utumie

nusu ya paketi ya maziwa (Tanga fresh) na asali kijiko kimoja cha chakula.kama kawaida

pima kiasi kwa kuzingatia diet yako.

Unaweza kutumia Nsizi mbivu badala ya tikiti maji au laa ukachanganya matunda yote mawili.
 
Ilikuwaje Mzizimkavu akala umeme? (Ban)

Mbona huwa humble sana humu.
Ma-Moderator wa Jamii forums wana ubaguzi Wamemuonea kumpiga Ban Daktari wetu na Mshauri wetu Mkuu wa Jukwaa la Afya Jamii forums. Kwa chuki zao tu Ma-Moderator wamempiga Ban Doctor MziziMkavu. Mimi Nilimuuliza Dr.MziziMkavu kwanini wamekupiga Ban ?alinijibu Eti Ma -Moderator wanasema Ninachangia Thread za watu kuchangia Topic wanazo zungumza na kuweka Matangazo ya dawa zangu . Sikuona sababu yoyote ile ya Kumpa Ban Dr.MziziMkavu zaidi ya chuki walizo kuwa nazo baadhi ya Ma-Moderator wa Jamii forums. Messege yake ya kufungiwa Jamii Forums imeandikwa hivi amenipa Doctor MziziMkavu ninaikopi na kuweka hapa

(Oops! We ran into some problems.
You have been banned for the following reason: Umekua Ukifanya matangazo ya Dawa katikati ya thread za Watu
wakati una uhuru wa kuanzisha thread Matangazo. Ni Uchafuzi. Your ban will be lifted on Oct 31, 2020 at 12:00 AM.
JamiiForums ) Huyo Moderator aliyempa Ban alichosema ni uongo mtupu kuhusu Doctor MziziMkavu eti anaweka Matangazo ya Dawa katikati ya Thread za watu ni maneno ya uongo mtupu . Ninavyo mjuwa mimi Tangu zamani kuwa Dokta Mzizimkavu ni mtu mstaarabu hatukani mtu na wala haweki Matangazo ya dawa zake kwenye Thread za watu. Ni chuki zake binafsi huyo Moderator aliye mpa Ban Dokta MziziMkavu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom