Tijipange UPYA - Ushindi ni wa CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tijipange UPYA - Ushindi ni wa CCM

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mwiba, Oct 17, 2010.

 1. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #1
  Oct 17, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Nasema vyama vya siasa haswa vya upinzani visiwe na tamaa ya ushindi kwani hakuna wa kuweza kuyapanga matokeo ila ni CCM ,CCM ndie pekee awezae kuyapanga matokeo na kumpa ubunge amtakae ,hilo halitaki mjadala tumeona 2005 .alipora uchaguzi na kutompa CUF kiti hata kimoja cha ubunge eti kwa kuwa CUF ilikuwa imejikusanyia viti vya ubunge kule Zanzibar.

  Nasema vyama vijipange upya na madai ya kuibadili katiba na kudai tume mpya ya uchaguzi kwa ajili ya matayarisho ya uchaguzi wa 2015 ,Katiba na tume ambayo itashirikisha vyama vyote vya upinzani vikubwa na vidogo na pia kushirikisha maoni ya wananchi katika uundwaji wa Katiba mpya ya Nchi hii ,chini ya mfumo wa vyama vingi.

  Mara tu uchaguzi huu utakapomalizika basi vyama vya upinzani visibweteke ,vizuke kwa kasi mpya yenye kudai madai ya Katiba mpya na pia Tume mpya ya Uchaguzi ,sio vikubali kuitwa na tume iliyopo ili kutoa maoni na kama kunahitajika marekebisho ,wakati kukubali au kukataa kutatokana na tume hiyo ya zamani ,huko ni kuzidiwa na kufanywa vyama vya upinzani kama wagonjwa wa uendawazimu ,maana mgonjwa wa uendawazimu amuonapo daktari huwa kimya na kusikiliza kama mwenye akili timamu,ndivyo vyama vya upinzani vinavyofanywa na tume hizi za uchaguzi.
   
 2. tartoo

  tartoo Senior Member

  #2
  Oct 17, 2010
  Joined: Jul 2, 2010
  Messages: 130
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wamekutuma!

  Mwaka huu hamna rangi utaacha ona...:dance:

  bbbbbb..bbyyeee:A S 103:
   
 3. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #3
  Oct 17, 2010
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,437
  Likes Received: 2,352
  Trophy Points: 280
  Maneno mazuri ...hasa kwa Prof Lipumba! Amegombea urais mara ngapi vile?
   
 4. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #4
  Oct 17, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Sijatumwa ila ukweli ndio huo ,inawezekana ni mara yako ya kwanza kuweza kukumbuka makelele ya uchaguzi na hivyo kuwa mgeni na hutambui ushindi wa CCM unapatikana vipi ,amini kabisa Slaa hana wapiga kura zaidi ya wapiga debe,kwa maana wengi ya wanaohudhuria si wapiga kura ,sasa unaposema Slaa atashinda Uraisi inakuwa hujielewi ,just unafuata mkumbo ,hebu Slaa aulize katika mikutano yake ni wangapi wamejiandikisha au wana shahada za kupigia kura ? Pia uelewe kuwa Chadema haikusikika kushawishi wananchi waende kujiandikisha ,hakuna hata mkutano mmoja waliwahi kusema hayo ,hivyo kujikuta wakiwa watupu ,hilo hawawezi kukuambia ,kura za Chdema ni kidogo sana na hilo Slaa analielewa ,mi msimamo wangu ni madai ya Katiba mpya na tume mpya ya uchaguzi bila ya kubadili hayo ,upinzani hakuna ushindi ,zimebaki siku chahe tu ,utashangaa kura mtakazopata Chadema ila msije mkasema mbona kwenye mikutano mlikuwa mnajaa sana hapana hata pa kutia mguu ! Kumbe pamejaa pumba.
   
 5. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #5
  Oct 17, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Mbona hajawafikia wengine ,inaonyesha wewe ni mgeni wa siasa au siasa zako ni hapa hapa Tz tena JF ,pole sana bro !!
   
 6. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #6
  Jan 5, 2015
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Hili la katiba limetekelezwa bado kupigiwa kura ya hapana ,Je TUME HURU YA UCHAGUZI mbona akina UKAWA mmeshikwa na butwaa ?
   
Loading...