Tija Katika Hotuba za JK Mwishoni Mwa Mwezi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tija Katika Hotuba za JK Mwishoni Mwa Mwezi

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mo-TOWN, Mar 1, 2011.

 1. Mo-TOWN

  Mo-TOWN JF-Expert Member

  #1
  Mar 1, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,629
  Likes Received: 140
  Trophy Points: 160
  To be honest with myself napata tabu sana kuona tija kwa wide community (obviously kwa watawala labda zinalipa sana) katika hotuba za JK ambazo huzitoa mwishoni wa mwezi kwa taifa pale inapobidi (sidhani kama ni regular).

  Nashauri utaratibu huo kama utaendelea basi uwe wa mahojiano kati ka JK na media (not staged one) or whoever juu ya kile anacholiambia taifa. Hii itamsaidia JK kujua kwanza kama anawasaidizi wa kweli au la? Kwanini? Kwa sababu wao ndio wanamuandalia ajenda za hotuba hizo. Wasaidizi wa kweli kwa maana kumhabarisha raisi JK juu ya hali halisi ya nchi si tu kwa yale anayopenda kusikia JK/na wapambe wake mfano maswala ya maandamano ya CDM.

  Independent media/wanaharakati wanapaswa kupata fursa ya kuuliza maswali ya msingi ambayo yatawassaidia wananchi kujua na kuelewa mwelekeo wa nchi. Kwa mfano ktk hotuba yake jana watu tulitarajia JK atakuja na majibu muhimu kuhusu umeme, hali inazidi kuwa mbaya lakini kwa bahati mbaya kwa JK umeme si kipaumbele kiivyo kwani yeye anatarajia kuwa mwisho wa mwaka huu hali ya upatikanaji wa umeme itakuwa nzuri (No firm action).

  Utaratibu wa sasa unamfanya raisi JK aongee anyhow kwa sababu anahutubia na kuondoka. If I were there ningependa kujua ktk safariza nje je ameshawahi waeleza hao marafiki wa TZ juu ya changamoto hiyo na kuna mkakati wa kupata ufumbuzi/msaada wa haraka (mkumbuke JK anasema asiposafiri tutakufa njaa)

  Tujadili, Kwa kifupi ni kwamba mimi sioni tija kwa JK kutoa hotuba ambazo hazigusi hasa hasa vipaumbele vya wananchi kwa wakati husika (mfano kwa sasa umeme, kupanda gharama za maisha etc). Na si swala la JK ku-acknowledge hizo changamoto bali kama raisi kuja na majawabu.

  Nafikiri kuhoji kwa maana ya kupata ufafanuzi wa hotuba zake kutamsaidia raisi kujua kama hotuba zake zina-address shida za wananchi/vilevile kujua kama hao wasaidizi wake wanafanya kazi kweli?
   
 2. L

  Losemo Senior Member

  #2
  Mar 10, 2011
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 183
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu mm nakubaliana na wewe kabisa. Hotuba hizi za JK hazina tija kabisa, Angefanya kama wenzake wanavyofanya kwa kukutana na wana habari, wasomi, wachumi n.k. na atoe fursa ya kuulizwa maswali. Wakati fulani alianza kukutana na wahariri na ulikuwa mwanzo mzuri. naona kama utaratibu huo nao umekufa, nadhani mambo mengi hayana maelezo. Hata huu ulofa wetu kwakweli hauna maelezo. Tunataka kiongozi atakayeona ukweli na kuukabili bila kuona haya.
   
Loading...