Tigray yaituhumu AU kwa upendeleo katika mzozo wa Ethiopia

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Vikosi vya waasi kutoka mkoa uliokumbwa na vita kaskazini mwa Ethiopia wa Tigray, vimeushutumu Umoja wa Afrika kwa upendeleo, siku chache baada ya Jumuiya hiyo kumteua rais wa zamani wa Nigeria, Olusegun Obasanjo, kuwa mpatanishi katika mzozo huo.

Msemaji katika chama cha ukombozi wa watu wa Tigray, TPLF, Getachew Reda, ameituhumu AU kwa upendeleo kuelekea upande wa serikali ya Ethiopia na kusema itakuwa ujinga kutarajia ujumbe huo kufanya kazi.

Siku ya Alhamisi, Jumuiya hiyo ilitangaza uteuzi wa Obasanjo kama mwakilishi mkuu wa Pembe ya Afrika, ikisema ni sehemu ya harakati ya kukuza amani, usalama, utulivu na mazungumzo ya kisiasa.

Mkoa wa Tigray umekumbwa na machafuko tangu mwezi Novemba, wakati waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed alipovituma vikosi vya shirikisho huko Tigray kwa ajili ya kukiondoa chama cha TPLF.

Chanzo: DW Swahili
 
Back
Top Bottom