Tigray, Ethiopia: Umoja wa Mataifa waonya hali kuwa mbaya zaidi

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Miezi kumi tangu kuanza kwa vita vya Tigray, Umoja wa Mataifa umeonya hali ya kibinadamu katika mkoa huo wa kaskazini mwa Ethiopia inaelekea kuwa mbaya zaidi, ukilaumu kile ulichokiita mzingiro wa misaada kwa hali hiyo.

Mapigano yalizuka Novemba 2020 kati ya vikosi vya serikali ya shirikisho na wapiganaji watiifu kwa chama cha Ukombozi wa watu wa Tigray, TPLF, kinachoudhibiti mkoa huo wa wakaazi milioni sita. Maelfu wameuawa na zaidi ya milioni mbili wamelaazimika kuyakimbia makaazi yao.

Ingawa waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed, mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel ya mwaka 2019 aliahidi ushindi wa haraka, vita hivyo vimeendelea kwa miezi sasa, na kusababisha mzozo wa kibinadamu mkoani Tigray, ambao umewaacha watu 400,000 wakikabiliwa na mazingira yananyofanana na ya njaa kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.

Kaimu mratibu wa masuala ya kibindamu wa Umoja wa Mataifa nchini Ethiopia, Grant Leaity, alisema katika taarifa hapo jana kuwa mahitajio ya msaada, fedha taslimu na mafuta vilikuwa vinapungua au vimemalizika kabisaa, na kuongezeka chakula kiliisha tangu Agosti 20.

Leaity alisema kimsingi mkoa wa Tigray uko chini ya mzingiro fulani wa misaada, ambapo ufikishaji wa misaada muhimu unadhibitiwa vikali.

Leaity alisema malori yasiopungua 100 ya chakula, mahitaji mengine na mafuta vinapaswa kuingizwa Tigray kila siku ili kuendelea kukidhi mahitaji, lakini hadi sasa, na tangu Julai 12, ni malori 335 tu yalioingia mkoani humo, au sawa na asilimia 9 ya malori 3,900 yanayohitajika.

Kutokana na kushindwa kuingiza mahitaji ya kutosha ya kibinadamu, mwakilishi huyo wa Umoja wa Mataifa ameonya kuwa hali ya kibinadamu kaskazini mwa Ethiopia, na hasa mkoani Tigray, inaelekea kuwa mbaya zaidi, na kuihimiza serikali ya waziri mkuu Abiy kulegeza vikwazo.

Tangu kuzuka kwa mzozo huo, maafisa wa Ethiopia na waasi wa Tigray wametupiana lawama kuhusiana na suala hilo, kila upande ukiutuhumu mwingine kwa kuzuwia misafara ya msaada.

Na baada ya waasi kuingia pia katika mikoa ya Afar na Amhara, Leaity amesema hali katika mikoa hiyo imeharibika pia, ambapo watu milioni 1.7 wanakabiliwa na njaa, huku mamia ya wengine wakipoteza makaazi yao kufuatia mashambulizi makali ya waasi.

"Maisha ya mamilioni ya raia… yanategemea uwezo wetu wa kuwafikia na chakula, ugavi wa lishe, dawa na msaada mwingine muhimu. Tunahitaji kuwafikia mara moja na bila kizuizi kuepusha njaa na kiwango kikubwa cha vifo. ”

Chanzo: DW Swahili
 
Watigray wakati wanawatawala Waethiopia wenzao kwa miaka zaidi ya 20 waliona sawa, sasa kipo chama kingine madarakani cha kitaifa zaidi wao wanaleta ukabila na ukanda
 
Tigray ndio wametafuta hayo majanga kwa kufikiri wao ndo wamiliki pekee wa vyeo vikubwa Ethiopia. Vita haina adabu kabisa. It brings the worse out of human being existence
 
Back
Top Bottom