Msemajiwao
JF-Expert Member
- Sep 12, 2016
- 639
- 1,532
Mnamo tarehe 10 January 2017;
Nilifanya muamala kwa kumtumia Kijana Wangu Tsh 180000/= kwa Tigo Pesa.
Punde baada ya Kutuma; nikampigia simu kupitia Namba yake nyingine kumtaarifu akatoe;
Kijana Wangu akanambia ile laini niliomtumia Pesa imeharibika, kwahiyo hadi ali-renew! Kwakuwa alikuwa mbali; akaniambia ni bora niwapigie Tigo wairejeshe ! Halafu nimtumie kwenye namba yake! Nikawapigia Tigo wakani jibu wameizuia na itarejea baada 24hrs; Massa Yale yakapita Tigo wapo kimya; ikabidi niwapigie tena wakanijibu
"Hatuwezi kurejesha Pesa yako hadi tuwasiliane na third party yaani huyo niliyemtumia" nikawajibu hapatikani mtampataje? Wakajibu hadi atakapopatikana! Duh! Nikauliza sasa hapo mnafanyakazi kitaaluma kweli kama mtu ambaye hapatikani mnamngojea?
Nikamshauri yule Kijana awapigie Kwa Namba yake nyingine ili awape vielelezo kuhusu Namba yake ili wajiridhishe; alipowapigia wakamjibu watairejesha na hawakufanya hivo hadi siku ikapita; ijumaa nikamwambia yule Kijana aje mjini toka mkoa Wa pwani - alipofika tukaenda hadi branch ya ofisi za Tigo nikiwa na yule Kijana; akarenew namba yake; tukawaelezea ilivyo; kwamba hiyo Pesa ni either iende au irudisheni ! Wakajibu sawa watairesha haraka iwezekekanavyo!
Lakini cha ajabu tangu Jana kimya! Tumewapigia kuwambia warejeshe wanasema bado wanalifanyia kazi; yule Kijana anawapigia simu kuwasisitiza wanasema wanalifanyia kazi!
Na Mimi Nimewahoji kile kidada kinajibu hela yenyewe laki na themanini tu povu linakutoka; yaani nimekasirika hapa sijui nifanyeje ili ile Pesa irudi yule Kijana aende shule!
" nimewaza hivi kama Pesa tunafatilia tukiwa wote wazima; inakuaje Kwa ndugu ambao hufatilia Pesa za marehemu waliofariki na kuacha Pesa kwenye simu zao huwa wanapatiwa kweli?
Kumzungusha MTU ambaye haombi mkopo hii ni ishara ya utapeli.
Nani atutetee jamani?
Yaani hapa nina hasira Pesa ikirudi nachoma laini yao siitaki huduma yao tena!