TIGO yazidi kufulia kanda ya ziwa/mwanza. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TIGO yazidi kufulia kanda ya ziwa/mwanza.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by samirnasri, Mar 1, 2011.

 1. samirnasri

  samirnasri JF-Expert Member

  #1
  Mar 1, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Kampuni ya simu za mikononi ya tigo imezidi kuporomoka kibiashara katika maeneo ya kanda ya ziwa hasa mkoani mwanza kutokana na kutokuwepo hewani kwa muda mrefu. Ni takribani wiki moja na zaid mtandao wa tigo unapatikana kwa kusuasua hapa mwanza. Wakazi wengi wa kanda ya ziwa wanatumia mtandao wa vodacom na airtel (zain). Kutokana na kulitambua hilo kampuni ya tiGO imekuwa ikitoa promoshen mbalimbali kwa wakazi wa kanda ya ziwa ili kuwavuta kibiashara. Pamoja na promoshen hizo tigo wameshindwa kuboresha upatikanaji wa mtandao wao hata maeneo ya mjini. Takriban miezi minane au zaid iliyopita kampuni hiyo ya tigo ilianzisha kitu kinachoitwa extreme kanda ya ziwa ambapo mteja anakatwa sh. 200 na kupewa dakika 20 za bure ambazo wangezitumia hadi sa 12 jioni. Baada ya kuona promoshen hiyo imeshindwa kuwateka watu wa kanda ya ziwa tigo waliamua kuongeza dakika ambapo kwa takriban mwezi mmoja sasa extreme kanda ya ziwa inampa mteja dakika 33 kwa sh. 200. Hata hivyo baadhi ya wakazi wa mwanza hivi sasa wanailalamikia kampuni hiyo kwani mara nyingi baada ya wao kujiunga na extreme hiyo mawasiliano ya simu tigo kwenda tigo au kwenda mitandao mingine yanakatika. Mpaka muda huu napoandika habari hii tigo haiko hewani tangu asubuhi, nadhani wakazi wa mwanza ni mashahidi. Kwa wale wenye ndugu, jamaa, marafiki, wake, wachumba au wapenzi walioko mwanza msishangae mtakapoona watu wenu hawapatikani kwenye namba zao za tigo ni tatizo kubwa la kimtandao ambalo limewasibu na wengine wengi wameapa kuachana na tigo na kujiunga na vodacom au airtel kwa kuhofia kupoteza fursa mbalimbali zikiwemo nafasi za kuitwa kwenye interview. Wakazi wawili niliozungumza nao walisema wametuma maombi ya kazi na wanategemea muda wowote kuitwa kwenye interview kwa njia ya simu na bahati mbaya kwenye barua zao za maombi walijaza namba zao za tigo ambazo kwa muda wa wiki moja sasa zimekua zikipatikana kwa masaa machache.
   
 2. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #2
  Mar 1, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Kweli kabisa kwa usemacho
   
 3. samirnasri

  samirnasri JF-Expert Member

  #3
  Mar 1, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Kila ukipiga simu unaambiwa erro in network connection. Ukituma sms unajibiwa meseji sending failed.
   
 4. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #4
  Mar 1, 2011
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Tigo ni taabu tupu. Hata hapa dar mara nyingi ukimpigia mtu tigo kwenda tigo unapata mwangwi (Echo) yaani unajisikia mwenyewe na mara nyingine ukiongea na mtu simu inaganda na kuwa amuwezi kusikilizana.
  nafikiri wana wakati mgumu sana katika kurekebisha matatizo hayoo na ikiwezekana kushusha bei kama walivyofanya Airtel na Vodacom.

  Tigo hiyo ni changamoto kwenu kwani ni rahisi kupoteza wateja kuliko kuwapata
   
 5. K

  Kitangawizi Member

  #5
  Mar 1, 2011
  Joined: Feb 18, 2011
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa kweli tigo imeleta usumbufu mkubwa hatuwasiliani na jamaa zetu.
   
 6. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #6
  Mar 1, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  tatizo kubwa ni nini sasa yaani hii kampuni huwa haieleweki kabisa ndio maana na bei zao huwa wanashusha sana
   
 7. samirnasri

  samirnasri JF-Expert Member

  #7
  Mar 1, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Yaani kero ya mwanza imezidi wiki nzima sasa tunawasiliana kwa kubip. Kama leo tangu sa mbili asubuhi mpaka sa tisa mchana huu hakuna mawasiliano ya tigo. Kitu cha ajabu ile bar ya network inaƶnesha network iko full. kuna jamaa yangu anasema wamekosana na demu wake ambaye anamlaumu kwa nini siku hizi anezima simu mara kwa mara bila sababu.
   
 8. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #8
  Mar 1, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  karibuni VODA WADAU swaaaaafi hakuna purukushani
   
 9. kyemo

  kyemo Senior Member

  #9
  Mar 1, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 196
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  wanafulia nao hawa,tunawabeba km JK lakini hawabebeki,dawa yao kuwatosa sasa
   
 10. samirnasri

  samirnasri JF-Expert Member

  #10
  Mar 1, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Voda tukaribie mara ngapi wakati watu tunj line mbili mbili na simu mbili! Kilichobaki ni kuitelekeza line ya tigo. Mimi kuanzia kesho simu yenye line ya tigo naweka line ya airtel for good.
   
Loading...