Tigo yakata rufaa kuwalipa AY, Mwana FA TSh 2.18 Bilioni, majibu ya rufaa yao kutolewa Julne 27

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,292
Kampuni ya simu ya MIC Tanzania (Tigo) imekata rufaa kupinga hukumu iliyoamuru iwalipe Sh2 bilioni wanamuziki wawili, Ambwene Yesaya na Hamisi Mwinjuma kutokana na kutumia bila ya ridhaa yao, nyimbo za wasanii hao nyota nchini.

Yesaya, ambaye ni maarufu kwa jina la kisanii la AY na Mwinjuma anayejulikana kwa jina la MwanaFA, walifungua kesi hiyo ya madai kwenye Mahakama ya Wilaya ya Ilala kupinga kitendo cha kampuni hiyo ya huduma za simu kutumia nyimbo zao kwenye miito ya simu bila ya ridhaa yao.

Nyimbo mbili zilizotumika kwenye miito hiyo ya simu ni “Dakika Moja” na “Usije Mjini” ambazo nyota hao wameshirikiana.

Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Juma Hassan alitoa hukumu ya kesi hiyo Aprili 11, akiwapa ushindi wasanii hao maarufu katika muziki wa vijana uliopachikwa jina la Bongo Fleva.

Katika hukumu hiyo, Mahakama iliiamuru Tigo kulipa Sh5 milioni kama faini ya uharibifu na kulipa Sh2.16 bilioni kama faini ya jumla.

Iwapo wasanii hao watashinda rufani hiyo, watakuwa wameandika historia katika matumizi ya Sheria ya Haki Miliki na watakuwa wasanii wa kwanza wa muziki wa kizazi kipya kufungua kesi na kushinda.

Katika rufaa hiyo, Tigo kupitia kampuni ya Law Associates imeainisha sababu saba za rufani, ikidai hakimu wa Mahakama ya Ilala alikosea kisheria kuwapa ushindi wasanii hao kwa kuwa hawakuthibitisha madai yao wala hasara waliyopata.

Kampuni hiyo pia inadai kuwa mbali na kutoeleza hasara waliyoipata kutokana na kazi zao kutumika kwenye miito ya simu, walitakiwa kueleza faida ambayo wangepata kama kazi zao zisingetumika kwenye miito hiyo.

Sababu nyingine ya Tigo kukata rufaa hiyo ni wasanii hao hawakuwa wamesajili kazi zao Chama cha Hakimiliki Tanzania (Cosota).

Tigo inadai kuwa wakati wa usikilizwaji wa kesi ya msingi, wadai walisema wamesajili kazi hizo, lakini waliwasilisha barua ya Baraza la Sanaa (Basata) ya kutambua kupokea kazi zao na si cheti cha usajili cha Cosota.

Kwa mujibu wa Tigo, wanamuziki hao walipaswa kuwasilisha mahakamani cheti cha usajili wa Cosota ambako kuna utaratibu wa kujisajili ikiwa ni pamoja na kujaza fomu maalumu baada ya kulipia malipo ya usajili ya kila mwaka.

Kampuni hiyo inasisitiza kuwa wasanii hao hawakuwa na haki ya kudai fidia hiyo wakati hawajasajili kazi hizo Cosota na hivyo kuiomba Mahakama Kuu itengue hukumu iliyowapa ushindi.

Akizungumzia hukumu iliyowapa ushindi, MwanaFA alisema huu ni wakati wa mabadiliko.

“Wale waliokuwa wanachukulia Sheria ya Hakimiliki kama mzaha, watambue kwamba zama zimebadilika,” alisema nyota huyo wa muziki wa rap ambaye aliingia kwenye muziki akijitambulisha kama Mwanafalsafa kabla ya kufupisha jina lake na kuwa MwanaFA.

“Hakuna anayetilia maanani kutumia kazi za wasanii bila ridhaa yao huku akinufaika na wasanii kubaki wanalialia. Huu ni wakati wa kutambua kuwa inawezekana kupata haki yako iwapo utasimama kidete kuitetea kwa sababu sheria zipo.”

Akisisitiza, AY ambaye pia ni nyota katika muziki wa rap aliyeimba R&B akishirikiana na Diamond katika siku za karibuni, alisema huo ni mwanzo wa wasanii kufunguka masikio na kutambua haki zao.

Alisema wasanii wamekuwa wakilalamika juu ya haki za kazi zao, lakini hawachukui hatua.

“Wakati ni sasa, muziki ni kazi kama kazi nyingine na ni ajira pia, hivyo unastahili kuheshimiwa,” alisema AY.


Mahakama Kuu ya Tanzania leo imesikiliza mapingamizi ya awali ya maombi ya rufaa yaliyowasilishwa na kampuni ya mawasiliano nchini Tigo dhidi ya hukumu iliyotolewa na mahakama ya wilaya ya Ilala, April 11 mwaka huu ya kutakiwa kuwalipa AY na Mwana FA shilingi bilioni 2.18 kama fidia ya kutumia nyimbo zao bila ridhaa yao.

1024x576xMsando-3.jpg.pagespeed.ic.PCWHloHCDU.jpg

AY akiwa na mwanasheria wake Alberto Msando nje ya Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam
Mapingamizi hayo matatu yamewasilisishwa na Mwana FA na AY kupitia mwanasheria wao, Alberto Msando. Miaka minne nyuma, wasanii hao wawili walifungua kesi ya madai dhidi ya kampuni ya Tigo baada ya kutumia nyimbo zao ‘Dakika Moja’ na ‘Usije Mjini’ kama miito ya simu kwa wateja wake bila kuwa na mikataba nao.
Ijumaa hii, Mhe. Isaya Arufani ambaye ni Naibu Msajili wa Mahakama ya Tanzania alisikiliza utetezi kutoka kwa mawakili wa pande hizo mbili. Mwana FA na AY walikuwepo pia mahakamani hapo.
Mhe. Arufani ametaija June 27 kuwa siku ya kusikilizwa kwa maamuzi ya Mahakama Kuu kuhusiana na rufaa hiyo.
“Kilichokuwepo leo ni kusikilizwa kwa mapingamizi ya awali ya maombi waliyoleta Tigo ya kuomba kwamba kuzuia kukaza hukumu iliyotolewa na mahakama ya Ilala. Kwahiyo leo tumesikilizwa mapingamizi hayo na mahakama itatoa maamuzi yake tarehe 27 mwezi wa sita kuhusu mapingamizi ambayo tumeyaweka dhidi ya maombi yao,” Alberto Msando, mwanasheria anayewawakilisha AY na Mwana FA ameiambia Bongo5 mahakamani hapo.

“Yalikuwa mapingamizi matatu kwamba maombi yao yamekiuka baadhi ya vifungu vya sheria,” aliongeza Msando
1024x576xMsando-4.jpg.pagespeed.ic.6Tx8qxr32d.jpg


AY na Mwana FA wakiwa na mwasheria wao, Alberto Msando

Kwa upande wake Rosan Mbwambo wa kampuni ya Law Associates inayoiwakilisha Tigo kwenye kesi hiyo amedai kuwa kampuni hiyo haikuridhika na hukumu iliyotolewa na mahakama ya wilaya ya Ilala ndiyo maana imekata rufaa.

“Sheria inaruhusu ukishakata rufaa uombe hukumu isitekelezwe mpaka rufaa isikilizwe. Tigo wanasema tu wao hawajaridhika na kwasababu mfumo wa kimahakama unaruhusu mtu asiporidhika kwenda juu, wameenda juu tu kwa kuomba mahakama ya juu iangalie upya,” alisema Mbwambo.

Katika hukumu ya awali iliyotolewa na Hakimu Mfawidhi wa mahakama ya Ilala, Juma Hassan, Tigo walitakiwa kulipa shilingi milioni 25 zingine kama fidia kutokana na hasara waliyoipata wasanii hao kwa kutumiwa kwa nyimbo zao. Hiyo imekuwa hukumu kubwa zaidi kuwahi kutolewa kwenye kesi zinazohusiana na haki miliki za kazi za muziki nchini Tanzania.
Msikilize wakili wo hapa

Chanzo:Mwananchi, Bongo5
 
Katika rufaa hiyo, Tigo kupitia kampuni ya Law Associates imeainisha sababu saba za rufani, ikidai hakimu wa Mahakama ya Ilala alikosea kisheria kuwapa ushindi wasanii hao kwa kuwa hawakuthibitisha madai yao wala hasara waliyopata.
 
Sababu nyingine ya Tigo kukata rufaa hiyo ni wasanii hao hawakuwa wamesajili kazi zao Chama cha Hakimiliki Tanzania (Cosota).
 
Wasanii wanavyodharau kosota Na basata Na jua watakuwa hawana vyeti walivyosajilia nyimbo Na watakuwa awakuilipia kosota Na hawana fomu za malipo hapo Tigo watashinda pia kwenye faida Na hasara wasanii wanaficha sana mapato yao Na mikataba ya kimangungu hapo pia litawakosti maana kuna mamlaka kama za kodi zitatakiwa zithibitishe mifano ye walilipa kodi kiasi gani
 
Natamani washinde hii kesi,lakini kama kinachoelezwa hapo kiko sahihi kinahitaji kudhibitishwa basi jamaa kama watapata haizidi sh.200m.
 
Nilidhani kwenye hiyo rufaa Tigo wangesema kuwa hawakutumia hizo nyimbo za wasanii. Au walinunua hizo ringtones toka kwa producer.

Kama walizitumia, wajiandae tu kulipa. Wanachokifanya ni kupoteza muda tu.

MKUU UMEPITA MULEMULEEEEE....WASANII WA BONGO WANAWADHARAU MAPRODUCER ILA WANASAHAU KUWA HAKUNA MSANII STAA BILA BEAT AU MIDUNDO MIKALI TOKA KWA PRODUCER....MIE NINGEKUWA PRODUCER WA HIZO NYIMBO NINGEWAPIGIA SIMU TIGO NA KUWAAMBIA WAWEKE MZIGO KAMA 200M MEZANI NIWAONDOLEE GHASIA HIYO.

PIA KAMA FA NA AY WATASHINDA KESI NA KULIPWA FIDIA BASI NA PRODUCER ANATAKIWA APATE MRAHABA KUTOKANA NA MADAI YA KINA AY AU KAMA VIP NA PRODUCER NAYE AFUNGUWE KESI YA KUWADAI TIGO KUTUMIA BEATS NA MAPIGO YAKE KUTANGAZA NA KUPATA MAPATO MAKUBWA KWENYE BIASHARA YAO.

HATIMA YA KESI ALIKUWA NAYO PRODUCER NA SIO HAKIMU...AHAHAHAHA.
 
Back
Top Bottom