tiGO wanaweza kuwa wazalendo ngoja tuone | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

tiGO wanaweza kuwa wazalendo ngoja tuone

Discussion in 'Matangazo madogo' started by ThinkPad, Dec 17, 2008.

 1. ThinkPad

  ThinkPad JF-Expert Member

  #1
  Dec 17, 2008
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 1,851
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Tigo wamepunguza mzigo kwa wananchi kwenye ghalama za matumizi ya simu.nadhani tungejiunga na tigo na kususia mitandao kama vodacom mitandao inayo nyonyapesa mpaka na wao wapunguze gharama zao maana hawafahamu makali ya maisha ya wananchi,nawapapongezi tiGO.
   
 2. F

  Franc New Member

  #2
  Dec 17, 2008
  Joined: Nov 16, 2007
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  You are very very right men!
   
 3. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #3
  Dec 17, 2008
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Ofcourse tigo wamesaidia sana kushusha garama za simu, Hata hivo bado wanayo nafasi ya kuendelea kushusha zaidi na kuvutia wateja wengi zaidi. Kwani siyo siri hata mwenye line zingine daima ana ka tigo pembeni ka kufanya mawasiliano ya muda mrefu. Tigo wametutoa, live long tigo.
   
 4. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #4
  Dec 17, 2008
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Bravo TiGo express your self yaani full kulonga ni bora utembee na battery kuliko kukosa mawasiliano.Mimi walipo niacha hoi ni kwenye huduma ya sms yaani 500 jero tu unatuma mitandao yote yaani raha tele kutoka saa 12 asbh mpaka saa 6 usiku.
   
 5. ThinkPad

  ThinkPad JF-Expert Member

  #5
  Dec 17, 2008
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 1,851
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  kweli panapo kweli lazima tuseme ni wazi kabisa tiGO kapunguza gharama.
   
 6. Mshiiri

  Mshiiri JF-Expert Member

  #6
  Dec 17, 2008
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 1,893
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  I suspect we are stupid for a country such as Tanzania kuchagua mitandao kwa sababu ya ughali wake. Tungetakiwa wote tuwe TIGO but tatizo ni coverage tu. Lakini ukiondoa maeneo ambayo bado hawajayafikia kwa mawimbi sehemu zile ambazo TIGO ipo bado watu wanakumbatia mitandao kama voda na zain ambazo ni aghali hata kushinda mitandao yote duniani. Mitandao ya USA dola 5 unaongea zaidi ya masaa 8.33 bila promotion yeyote hapa ni full rate. Sasa iweje hii mitandao ya ndani ichaji ghali zaidi na serikali isilinganishe na mitandao duniani? Je hawa TCRA kazi yao mimi kwa kweli sijaiona sioni wakifuatilia jambo lolote hata kuna kipindi nilituma lalamiko la TIGO kuhusu customer service line kuwa haipatikani na walikaa kimya kama maji ya mtungi. Sasa sijui kwa kipindi kile ni hizi 10% ziliwafanya waone kufunga ndoa na haya makampuni au la?

  Enzi zinapita na tutawahoji serikali kwa nini mawasialiano ni ghali kiasi hicho ukilinganisha na sehemu zingine duniani? Nini suluhu ya hili tatizo na si kukumbatia 10% huku tukiliua Taifa na uchumi wake.

  BIG UP TIGO!!!!!
   
 7. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #7
  Dec 17, 2008
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Sure...tiGO are doing good!
   
 8. Mambo Jambo

  Mambo Jambo JF-Expert Member

  #8
  Dec 17, 2008
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 1,100
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Have seen some boards jana 1tsh per sec, 24 hrs.

  Thats great for Tanzania, we need more TiGO

  Great Job TiGO keep grinding.
   
 9. C

  CalvinPower JF-Expert Member

  #9
  Dec 17, 2008
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 996
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 60
  tatizo gharama zikiwa chini sana baaas ujue mtandao utakuwa bize saazote. mesej ukituma asubuhi inafika mchana, ndo tatizo la bwerere. mfano nairobi ijumaa mpaka jpili ni ngumu sana kumpata mtu kwenye sim. tariff zinakuwa chini siku za weekend. wapo wanaopata matatizo gharama zikiwa chini sana na wapo wanaofurahi gharama zikiwa chini.
   
 10. ThinkPad

  ThinkPad JF-Expert Member

  #10
  Dec 17, 2008
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 1,851
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  kweli lakini gharama zikiwa chini watu watazoea maana nikweli watu wengi hawawasiani kutokana na gharama za simu kuwa kubwa lkn kama zimeshushwa na hao watu wa tiGO nadhani mwanzo wananchi watashambulia bandwidth lakini mwishoe watazoe tu na kufanya kamamatumizi yakawaida na sio tena kama sandakalawe kama tulivyozoe.Nadhani makali yatapungua ila tiGO wajizatiti maana watu wengi wataingia na kutumia mtandao wa tiGO.
   
 11. B

  Boney E.M. JF-Expert Member

  #11
  Dec 17, 2008
  Joined: Jan 22, 2007
  Messages: 425
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Big Up for TIGO. Ukweli wao ndio wametufungua macho kuwa kumbe hizi rates kama wanavyochaji Vodacom ni wizi mtupu!!! Lakini wa kulaumiwa zaidi ni TCRA (Tanzania Communication and Regulatory Authority). Hili Shirika linafanya kazi kwa ajili ya nani? Wananchi wengi wananyonywa na hizi kampuni za simu za mkononi. TCRA walitakiwa kuelezea viwango wanavyotozwa wananchi kwa uwazi kama EWURA wanavyofanya. Mimi binafsi sioni TCRA inafanya kazi kwa maslahi ya nani. Kabla wao hawajachukua hatua zozote (kama watachukua at all- which I doubt) nakubaliana kuwa tutoke Voda na kutumia Tigo waojali wananchi.
   
 12. Ngonalugali

  Ngonalugali JF-Expert Member

  #12
  Dec 17, 2008
  Joined: Jan 12, 2008
  Messages: 658
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 0
  Big up tiGO
  Ni ukweli usiofichika kuwa tiGO wanaleta challenge kubwa kwa mitandao mingi ya simu.
  Kuna kitu kimoja ambacho wanatakiwa wakifanye ili wawe juu kwani najua wanaouwezo kama wakipenda. Wasimamishe minara mingi zaidi na pia wajitahidi kusambaza huduma zao sehemu zao. Kwa mfano nilikuwa mkoa wa Manyara mwaka jana sehemu za Mbulu ambapoo walikuwepo lakini huduma za vocha zikawa hazipatikani. Kuna sehemu nyingi za mikoani ambapo nimefika na kukuta wananchi wakiwa wameweka mambango ya tiGO kwenye vibanda vya biashara huku kukiwa hakuna mtandano huo. Hiyo inaashiria wazi kuwa wananchi wengi wanalilia huduma za tiGO ila hawazipati. Huwezi kuamini kuwa kuna sehemu hata line zinauzwa wakati hakuna mnara.

  TIGO fanyeni muwezalo ili mkamate soko na kuweka coverage nzuri kwa wateja wenu.
   
 13. KiuyaJibu

  KiuyaJibu JF-Expert Member

  #13
  Dec 17, 2008
  Joined: Aug 29, 2007
  Messages: 769
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 45
  Ni kweli kabisa Tigo wamejali kipato cha watanzania walio wengi kwa sasa,lakini watadumu kwa muda gani katika hiyo nafuu?
  Unajua hii mitandao ya kampuni za simu iko hivi katika gharama zake ambazo binafsi nilipata hesabu zake nikiwa na kampuni moja ambayo ilisimamisha/jenga transmission tower zote za Vodacom-TZ,mpaka mwaka 2006 kujenga tower 1 ilikuwa sio chini ya Tshs million 120,halafu maintenance ya tower 1@mwezi ni Tshs million 20.
  Aina hii ya mawasiliano inaitwa peer to peer communication,hapa satellite dishes zinatumika pia;bado kuna gharama nyingine nyingi tu ktk kufanya kampuni ifikie malengo yake;hapa international calls zote zinapitia tena kwenye kampuni nyingine hii gharama nyingine hiyo;kwahiyo aina hii ya mawasiliano ni gharama sana kumilikiwa na kampuni moja ya simu pekee.
  Ndiyo maana TCRA waliwakalisha chini makampuni yote ya simu kwa sharti la kupunguza gharama za simu hapa nchini;lakini,makampuni karibia yote yalikataa kwa kigezo cha gharama za uwekezaji hazijarudi bado.TCRA wakapendekeza kampuni zote zi-share miundombinu ya mawasiliano kwa pamoja ili kupunguza gharama za uendeshaji ili mtumiaji apate ahueni ktk tarriff charges,kufikia hapa kikao kikavunjika.
  Lakini technolojia latest katika mawasiliano ya simu na mtandao/internet hivi sasa ni optic fibre,ambayo hii ndiyo the fastest uki-click tu page imekwisha funguka inakusubiri u-apply command nyingine.
  Hivi sasa,SEACOM wanajenga mkonga wa mawasiliano hayo(optic fibre backbone) kutoka Cape town-South Africa kupitia Bahari ya Hindi hadi Malindi-Kenya.Na mradi huu unategemewa kukamilika June,2009.
  Kukamilika kwa mradi huu kutaleta nafuu sana kwa watanzania katika mawasiliano ya simu na internet/mtandao kuliko hivi sasa,hili ndilo suluhisho la mawasiliano.
   
Loading...