Tigo wanatuibia kabisa nimeprove

CK Allan

JF-Expert Member
Aug 14, 2013
2,781
6,065
Juzi nilinunua salio 1200 kupitia tigo pesa halafu nikanunua kifurushi cha Internet MB 200 kwa wiki kesho naamka asubuhi nakuta salio 02 nikawapigia tigo wakadai taarifa zangu nyingine haziko active so nipige baada ya nusu SAA nikaona isiwe tabu nikanunua 250 tena Jana.

Cha ajabu Leo asubuhi nina 152 yaani 100 nzima imesepa nikawapigia tena baada ya Dk 10 hivi akapokea mdada akadai wanaupdate waone kwanini hela zinakatwa maana amecheki kwenye system sina makato yoyote halafu akadai eti niende tigo shop.Kwakweli huu mnaofanya tigo no upuuzi hebu acheni Mara moja
 
Pole sana ndugu... Mimi tigo walikuwa wananikata 150 kila siku.. Yaani simu ilikuwa iki lala na salio tuu kosaa... Nikawapigia simu... Cha ajabu hata wao wanasema hawajuhi kwa nini inakatwa.. Nikaenda mlimani city... Hapoo ndo nilijutaa kwenda.. Maana walinikalisha foleni, mwisho wa siku naambiwa ombi lako limeshughulikiwa.... Nikasema ngoja leo nijaribu kuacha ka salio.. Hahaha... Kesho naamka nakuta wamerambaa... Yaani ilikuwa ni kama wiki mbili mfululizo... Mwisho wa siku walipoona siachi salio kwenye simu na wenyewe wakaacha hako kawizi..
 
Nimesoma kwenye gazeti moja nikaona wao ni miongoni mwa makampuni ya simu yanayotoa huduma mbovu na wanatakiwa kulipa faini ya kama Tshs 25 Mil, yawezeka kabisa moja ya sababu ni kama hizo
 
Pole sana ndugu... Mimi tigo walikuwa wananikata 150 kila siku.. Yaani simu ilikuwa iki lala na salio tuu kosaa... Nikawapigia simu... Cha ajabu hata wao wanasema hawajuhi kwa nini inakatwa.. Nikaenda mlimani city... Hapoo ndo nilijutaa kwenda.. Maana walinikalisha foleni, mwisho wa siku naambiwa ombi lako limeshughulikiwa.... Nikasema ngoja leo nijaribu kuacha ka salio.. Hahaha... Kesho naamka nakuta wamerambaa... Yaani ilikuwa ni kama wiki mbili mfululizo... Mwisho wa siku walipoona siachi salio kwenye simu na wenyewe wakaacha hako kawizi..
wewe ulikua umejiunga na huduma yao itwayo RBT ( miito ya simu). hata mi ninayo ila naifurahia kwa sababu nilifanya kwa maamuzi yangu
 
Inaweza kuwa kweli, lakini mimi sijawahi shiriki huduma yoyote ya tigo zaidi ya sms, kupiga na mtandao na hata sijawahi tumia tigo pesa, lakini ukiweka 1,500 ukajiunga na huduma yoyote ya 1,000 hiyo 500 iliyobaki wataikata taratibu mpaka itaisha.
 
Hata Mimi sijajiunga na makato yoyote na wenyewe wameprove sasa kwanini wananikata?
 
wewe ulikua umejiunga na huduma yao itwayo RBT ( miito ya simu). hata mi ninayo ila naifurahia kwa sababu nilifanya kwa maamuzi yangu
Yaani tangu nimeanza kutumia mtandao wa tigo, sijawahi kuwa na hizo huduma.. Okay, na kama zilikuwepo mbona wenyewe walishindwa kuziona kama ninazo!??
Na baada ya kushindwa kuziona wakaamua kunitoa kwenye hudumaa zootee lakini bado nikaendelea kuibiwa
 
Inaweza kuwa kweli, lakini mimi sijawahi shiriki huduma yoyote ya tigo zaidi ya sms, kupiga na mtandao na hata sijawahi tumia tigo pesa, lakini ukiweka 1,500 ukajiunga na huduma yoyote ya 1,000 hiyo 500 iliyobaki wataikata taratibu mpaka itaisha.
Watu wengi hamjui, kazi kulala mika
zingatia hili jambo nikueleze.
1. Kama unatumia smartphone au simu yoyote ambayo ina capability za kupata internet na huja disable internet yako, maana yake kila utakapo weka salio internet inaanza kutumia salio lako tena on demand ambayo ni gharama sana. Kwa hiyo utakuta kuna watu anaweka sh 1000 akitaka kununua kifurushi anakuta kuna 998 au chini ya hapo anaanza kusema ameibiwa ukweli ni kuwa internet imetumia sehemu ya vocha uliyo weka.
nini cha kufanya
kabla ya kuweka salio lako hakikisha ume diable internet kwenye simu yako, nunua kama ni kifurushi then fungulia intenet yako. hakikisha unawasha internet yako tuu pale unapo tumia, la sivyo utapata dhambi ya kusingizia mitandao ya simu inakuibia.

2. Hakikisha simu yako imejiunga na huduma ambazo unazihitaji kama hujui tembelea duka lolote la mitandao ya simu wakusaidie kuhakiki huduma zilizopo kwenye simu yako ili uchague zile unazo zihitaji na zile ambazo huzihitaji.
 
Weka pesa hata elf 5 tu kwny tigo pesa then unanunua bundle direct kutoka kwny tigopesa mie ndo njia niliyotumia kuwatumbua,kama wizi waibe hizo dakika kwa kuzipunguza lakini uchoko wa kukata vocha nilishaukomesha.
 
huu ndio ujanja

be
 
Kuna issue ya mtu akituma sms moja tu lakini anayepokea anapata zaidi ya 20 siku nzima zinaendelea ku-flow in with the same content
Hii mie imenitokea kwa mara ya pili leo,
Af kibaya mesej ya mchepuko wangu "pole mpnz"
Imekuwa ikiingia mara 5 zaidi baada ya ile ya mwanzo ila anayenitumia yupo voda na bado inazidi kuendelea kuingia.
 
Watu wengi hamjui, kazi kulala mika
zingatia hili jambo nikueleze.
1. Kama unatumia smartphone au simu yoyote ambayo ina capability za kupata internet na huja disable internet yako, maana yake kila utakapo weka salio internet inaanza kutumia salio lako tena on demand ambayo ni gharama sana. Kwa hiyo utakuta kuna watu anaweka sh 1000 akitaka kununua kifurushi anakuta kuna 998 au chini ya hapo anaanza kusema ameibiwa ukweli ni kuwa internet imetumia sehemu ya vocha uliyo weka.
nini cha kufanya
kabla ya kuweka salio lako hakikisha ume diable internet kwenye simu yako, nunua kama ni kifurushi then fungulia intenet yako. hakikisha unawasha internet yako tuu pale unapo tumia, la sivyo utapata dhambi ya kusingizia mitandao ya simu inakuibia.

2. Hakikisha simu yako imejiunga na huduma ambazo unazihitaji kama hujui tembelea duka lolote la mitandao ya simu wakusaidie kuhakiki huduma zilizopo kwenye simu yako ili uchague zile unazo zihitaji na zile ambazo huzihitaji.
Mkuu... Naona unajitahidi kutetea na kutuelimisha..

Lakini mimi bado ntakataa tuu.. Maana haiwezekani wakate kiwango kile kile kila siku... Na zaidi simu yangu huwa ina kifurushi cha internet wakati wote.

Kwa hiyo mi kwangu bado tigo ni wezii tuu...
 
Tatizo lako unaona kama tigo wanakuibia wakati ni makosa yako. situmii tigo lakini ktk mtandao ninao tumia nilikua mlalamikaji kama wewe. Baada ya kupata elimu jinsi ya kutumia mitandao ya simu nafurahia vizuri tuu. Hakuna mtandao unao mwibia mteja, ila wateja wengi ni wazembe
 
Hii mie imenitokea kwa mara ya pili leo,
Af kibaya mesej ya mchepuko wangu "pole mpnz"
Imekuwa ikiingia mara 5 zaidi baada ya ile ya mwanzo ila anayenitumia yupo voda na bado inazidi kuendelea kuingia.

Iyo na Mimi Leo bado inanitokea, nimehamua kuzima cm yenyewe yenye line ya uho mtandao
 
Watu wengi hamjui, kazi kulala mika
zingatia hili jambo nikueleze.
1. Kama unatumia smartphone au simu yoyote ambayo ina capability za kupata internet na huja disable internet yako, maana yake kila utakapo weka salio internet inaanza kutumia salio lako tena on demand ambayo ni gharama sana. Kwa hiyo utakuta kuna watu anaweka sh 1000 akitaka kununua kifurushi anakuta kuna 998 au chini ya hapo anaanza kusema ameibiwa ukweli ni kuwa internet imetumia sehemu ya vocha uliyo weka.
nini cha kufanya
kabla ya kuweka salio lako hakikisha ume diable internet kwenye simu yako, nunua kama ni kifurushi then fungulia intenet yako. hakikisha unawasha internet yako tuu pale unapo tumia, la sivyo utapata dhambi ya kusingizia mitandao ya simu inakuibia.

2. Hakikisha simu yako imejiunga na huduma ambazo unazihitaji kama hujui tembelea duka lolote la mitandao ya simu wakusaidie kuhakiki huduma zilizopo kwenye simu yako ili uchague zile unazo zihitaji na zile ambazo huzihitaji.
Unayo yaongea yote tumeyafanyia kazi, umejiunga na intanet na una MB za kutosha, una sms na dakika kibao lakini bado wanakata salio uliloliacha.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom